Mommadou Keita
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 230
- 238
Imetungwa na Mommadou Keita
NIMECHOKA kukaa ofisini lakini nalazimika kundelea kuwepo kutokana na kile nilichokuwa nikikisikia kutoka kwa wafanyakazi wenzangu waliofanikiwa kutoka nje na kurejea ndani ya ofisi bila ya kupenda.
Huko nje hakufai, foleni iko hapo getini alisema @Mbimbinho na kurudi kukaa kwenye siti yake huku akijiandaa kufungua kompyuta yake.
Mara anaingia malimingiii naye aliendelea kusema kile kilichokuwa nje, nikajua kuwa huku nje hakufai.
Yaani malori yamejaa njia nzima halafu wala hayatembei, madereva wameshuka na kukaa nje wakipiga soga huku wakivuta sigara, alisema malimingiii.
Sikuwa na sababu ya kutoka nje kwenda kuhakikisha kwani ujio wa ram ulitosha kabisa kunithibishia kwamba foleni ya Barabara ya Sam Nujoma ilikuwa imefika hadi ofisini kwetu.
Sijui nitaendaje nyumbani katika hali kama hii, alilalamika ram na kuungana na wenzake hao katika kuisema serikali kwa kushindwa kujenga njia mbadala kwa ajili ya malori tu.
Haya yalitakiwa yapite ndani kwa ndani kisha yakaibukie Chalinze, sijui kwa nini yanapita huku, alisema malimingiii.
Nadhani nilichokisikia kilikuwa kimetosha, nilichukua headphone zangu na kuziweka masikioni na kuendelea kuburudika kwa muziki niupendao ndani ya nafsi yangu.
Nilifanya hivyo huku nikifikiria cha kuandika kwa washikaji wa Jamii Forums, niliamini kwamba sikutakiwa kuandika kitu kigumu bali laini ambacho kitawakonga nyoyo zao.
&&&&
Niliangalia saa yangu ya kwenye simu iliniambia kuwa ilikuwa ni saa saba za usiku, bado nilikuwa ofisini nikingoja foleni iishe.
Nilimuwaza mke wangu, najua huwa hana tabia ya kusemasema kutokana na kuchelewa kwangu lakini sikuhiyo nilihisi lazima angenifikiria vibaya.
Ndio, angenifikiria vibaya kwa kuwa siku zote huwa anapenda nimtaarifu ninapokuwa ninachelewa kurudi nyumbani.
Lakini kwa muda huo nalihisi nimechelewa kumtaarifu, nilitakiwa nimwambie mapema, Saa saba hii si atajua ninajihami ? nilijiuliza.
Sikuona umuhimu wa kumpigia simu na kumwambia kwamba nitachelewa kwa kuwa nilishachelewa. Kupiga kwangu siku kungekuwa ni kumwamsha kutoka katika lindi la usingizi na kuanza kumfanya aanze kuhisi vibaya.
Sikutaka kuanzisha malumbano mapema, nilikata shauri kwamba tutakutana hukohuko na nitamweleza hali halisi.
Nilizima kompyuta na kuweka kila kitu sehemu yake na kukusanya kilichokuwa cha kwangu na kutoka zangu nje ya ofisi.
Kwanza niliona ni heri nihakikishe kama foleni imeisha au bado, ilikuwepo, sikuona haja ya kuwasha gari langu kwanza, nikashika mwelekeo wa kwenda nje.
Bosi leo ni heri utembee kwa miguu, maana huko hakuendeki, alisema mlinzi wa ofisini kwetu aliyeitwa kinubi.
Kweli kulikuwa hakuendeki, kila kona ilikuwa imefunga malori yalikuwa yameziba njia nilishuhudia na kunifanya nikate shauri la kuondoka bila ya gari langu.
Pamoja na kwamba nilitakiwa kukaa katika mwelekeo wa kwenda Ubungo ili nipate njia ya kwenda Kimara ambako ndiko malori mengi yalikuwa yakielekea, nikavuka Barabara ya Sam Nujoma na kukaa usawa wa kwenda Buguruni.
Madereva wengi wa pikipiki walinifuata na kutaka kunibeba kwa malipo lakini niliendeleza kile kiapo changu cha kutokupanda pikipiki katika njia kubwa hususan nikiwa Dar.
Sitaki hata siku moja, maana huwa siwaamini hawa madereva, wengi wa badaboda ambao wamejufunza pikipiki juzijuzi na wanajifanya wanaijua kuliko hata mtu aliyeitengeneza. SITAKI kuhatarisha maisha yangu.
&&&&
Nikiwa kituoni, nikaona daladala moja likigeuza na kurudi Buguruni, nikalipunguia mkono na liliposimama nikaingia. Nilikuwa abiria pekee ndani ya daladala hilo aina ya Toyota Hiace.
Abiria waliokuwa wakienda nao Ubungo walishuka na kuamua kutembea kwa miguu na wengine kupanda bodaboda.
Nilifika Buguruni na kupanda gari la kwenda Kariakoo, nilipofika Kariakoo ilikuwa ni saa saba unusu, kulikuwana daladala lingine lilolokuwa linaenda Mwenge, nikaona ni heri nipande, nikaingia.
Ile kuingia tu, ndani ya gari hilo nikamuona mwanamke mmoja mrembo sana. Alikuwa na kila kitu cha kuweza kumfanya aonekane kuwa mrembo kuanzia sura, mavazi yake na umbile lake.
Nilimptupia jicho la wizi naye akaniangalia kwa dharau ya kimjinimjini, pembeni yake alikuwa amekaa binti mwingine. Sijui kwa nini, sikutaka kukaa naye mbali kwa kuwa upande wa pili kulikuwa na siti iliyokuwa haina abiria, nikaa hapo na kuendelea kumwangalia kwa wizi.
Baada ya muda daladala lilijaa na kondakta kuamuru liondoke, lilishika njia na kuelekea Faya, Magomeni na kisha likashika njia ya kwenda Konondoni.
Tulikuwa tumefika Kinondoni Manyanya, ndipo kioja kilitokea, simu ya mwanamke yule mrembo ikaita. Kabla hajaipokea alimwambia kitu mwanamke aliyekuwa amekaa naye jirani.
Anapiga alisema huku akiiangalia simu yake.
Ipokee mwenzake alisema.
Haloo alisema kwa sauti yenye mamlaka fulani hivi.
Sikuwa nasikia maneno ya mpigaji simu lakini niliweza kuhisi kile kilichokuwa kikizungumzwa na upande huo wa pili, nitakuwa nakisia tu.
(Uko wapi?) Si nilikuaga kuwa nitakwenda kwa shangazi Mburahati hali yake ni mbaya
(Mbona hujarudi mpaka muda huu?) Hali ya shangazi imekuwa mbaya, tunampeleka hospitali
Hospitali gani) Mwananyamala niko naye hapa hali mbaya sana tunakodio teksi halafu hela haitoshi, alisema kwa sauti ya majonzi.
(Mmefika wapi?) Ndiyo tuko Magomeni, hatujui hata tutarudi saa ngapi?
(Nakuja) Aiiiiii, unataka uonekane mwema sana? We tuma mchango wako kwa tigo pesa kisha unisubiri hapo nyumbani.
(Ngoja nije nitakupa .) Unakuja ili iweje mbona unangangania? Wenzio wametupa pesa, tena simuyangu inaisha chaji we nitumie pesa tu.
(Kama inaisha chaji nikituma pesa utaipataje?) Nitaibusht wee nitumie bwana mbona unachelewa
(Simu yangu haina pesa) Kwani hapo dukani kwa Richard huwa wanafunga? Hebu nitumie bwana, acha utani kama sivyo sijui tutarudi vipi?
(Nitaingiaje ndani nawe mlango umefunga?), Ufunguo nimeuacha hapo chini ya mlango na chakula nimekuachia ndani, nitumie hiyo hela basi..
(Haya nitatuma), Asante mpenzi wangu nakupenda mume wangu alisema mwanamke huyo kisha akachia busu la kiutu uzima mwaaa.
Daladala lilifika Kituo cha Victoria. Akaangaliana na mwenzake na kucheka Halooooo oooh Kantangaze kisha akaachia msonyo.
Alaaaa anataka kuniharibia mingo zangu saa hizi, alisema yule mwanamke na kumfanya mwenzake amsapoti.
Shosti wee sikuwezi .
Yule mwanamke akachukua simu yake na kisha akaitafuta namba nyingine na kuipiga.
Halooo..baby nashukia wapi?
(Sayansi), haya nashuka muda si mrefu.
Kweli daladala lilipofika Sayansi yule mwanamke na mwenzake wakashuka. Nikageuza macho yangu kuwaangalia abiria wengine wachache waliokuwemo ndani ya daladala, wote waligeuka na kuniangalia.
Anachepuka huyu alisema alibiria mmoja ambaye naye alikuwa akifuatilia mazungumzo ya mwanamke yule na kuwafanya abiria wengine kuangua vicheko.
Nilijiuliza maswali mengi sana kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa mwanamke yule na alivyotengeneza nywele zake kama inaweza kukubalika na mwanaume wake aliyemuacha nyumbani, nilitamani kumfahamu huyo mwanaume mwenzangu kwa kuwa ameoa Mchepuko.
Based on true story
.

Last edited by a moderator: