Hadhi ya nafasi ya ubunge inazidi kushuka

Hadhi ya nafasi ya ubunge inazidi kushuka

Mwakanshahala

New Member
Joined
Mar 31, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Ndugu zangu najaribu kuwaza kwa sauti baada ya mchakato wa chama cha mapinduzi wa kuchukua form kuanza leo, nimeona mambo ambayo yanatafakarisha sana.

KUmekua na wimbi kubwa la watu maarufu kifedha ama kisanii lakini pia familia maarufu kuchukua form za ubunge.

Ni sahihi kwa sababu wana haki ya kikatiba kufanya hivyo, lakini kwa ujinga wangu naona kama nafasi ya ubunge inazidi kukosa maana hata wale wenye sifa ndogo kabisa nao wanajitokeza, either kwa kutafuta umaarufu au wakiwa na dhamira halisi.

Vip endapo watu hao wakapita kwenye mchakato na kupata ubunge tutakua na bunge la aina gani?
Kuna namna jamii imeanza kuona nafasi ya ubunge kama nafasi a udiwani au uenyekiti wa mtaa jambo ambalo naona litaleta shida kwa taifa.

Tutajikuta tuna bunge la wasanii na watu wengine wa hovyo ambao wameenda kutafuta status na ulinzi wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom