Habibu Mchange njiapanda

Habibu Mchange njiapanda

HABIBU MCHANGE aka Mdude ambaye pia alikuwa kiongozi mkuu wa kikundi haramu cha MASALIA aka PM7 yuko njiapanda kuhusu hatma yake ya kisiasa.

Tangu kundi hili liliposambaratishwa (mwezi desemba mwaka jana), na kufia mbali (januari mwaka huu), kundi hili liliangukia katika mgogoro wa kuchagua mahali sahihi pa kwenda wote kwa pamoja lakini hawakuafikiana. Mazungumzo yao ya kawaida, mawasiliano yao na Vikao vyao vilikuwa na maeneo matatu ya kwenda: 1. Kuanzisha CHAUMA; 2. Kuhamia CCM 3. Kuhamia NCCR mageuzi. Pendekezo la kurudi CHADEMA na kuomba radhi lilipingwa na wengi, hasa Eddo, Mtela na Shonza.

  • Wazo la kuanzisha chama cha siasa (CHAUMA) - lilionekana kuwatisha wengi kwa kuhisi kuna kazi kubwa ya kukijenga chama hicho ili kiaminiwe na watanzania wengi!.

  • Wazo la kuhamia NCCR lilitolewa na EDDO ambaye amekuwa akitoa sababu za kwamba angependa aendelee kuwa mpinzani na tena vijana wengi walioenda NCCR wengi wao wamefanikiwa sana kisiasa. Wenzake walilikataa wakihofia kwamba chama hicho kitawapa wakati mgumu saana kujiuza.

  • Wazo la kuhamia CCM lilionekana kuungwa mkono na BWANA fedha na bibi fedha (FEDHA MAALUMU) za kutoka CCM (kuibomoa CHADEMA) na wengine kusitasita.

Tangu mwanzo Shonza na Mtela wao walionekana kuchagua kwenda CCM wakiwa na sababu:

1. Kimewasaidia sana kuwaweka mjini kwa zaidi ya mwaka mmoja. Hela hii imekuwa ikiwafikia wengine hata kabla ya kufukuzwa CHADEMA kupitia MTELA na mara nyingine SHONZA.

Hela za kutoka MASWA (ambapo katika awamu zote mpaka jumapili ya tarehe 24/2/2013 nilipowasiliana na mtela zinawafikia kupitia MTELA). Mtela alikuwa anapewa hela za maswa na muda mwingine za LUMUMBA na kuwafikishia wengine. Kwa mfano EDDO amekuja DAR zaidi ya mara 5 mwezi januari na februari akiwa hajalipwa mshahara miezi mi 3. Hapa ndipo alikuwa anatokea;

2. Wote walikuwa wameahidiwa AJIRA, ambapo mpaka sasa taarifa za ndani zinaonyesha kuwa atafanya kazi LINDI au MTWARA (siyo ualimu aliousomea wala si ukuu wa wilaya-kulingana na makubaliano ya awali na ya sasa). Shonza ameahidiwa kubaki Dar!.. AJIRA hizo wameahidiwa kupewa rasmi baada mizunguko ya kisiasa kuibomoa CHADEMA.

3. Ndani ya CCM watatafuta namna ya kujisafisha na kujitofautisha na mafisadi papa ili wagombee ubunge na kushinda. Mtela anaona akiwa CCM anaweza kuwa na nguvu MBOZI MASHARIKI kuliko kuwa NCCR. Vivyo hivyo Shonza analenga viti maalumu, jimbo la ubungo na jimbo la MBEYA mjini.

HABIBU Mchange kwa upande wake alisita sana kuhamia mapema kwa kuhofia kuchuja ZAIDI. Alibaki kuongoza chama cha wanamuziki wa kigoma LEKA DUTIGITE na kueandelea kula kwa jasho lao!. Hivi sasa yupo tayari kujiunga na CCM lakini ANASEMA KUWA anahofia kuporomosha IMAGE yake mbele ya jamii. Washauri wake wamemuambia akiamua kwenda CDM kuoma radhi muda huu hatapokelewa!. Wamemshauri aende CCM akatumie majukwaa yake kuisakama CDM na baadaye mwaka huu arudi na kuomba radhi kwenye mkutano mkubwa wa CDM!.. Huyu bro anaonekana kuukubali ushauri huu!..

MTIZAMO WANGU: Ni heri aende kuomba msamaha sasa (kama kweli ana nia ya kurudi) kuliko kuitukana CDM majukwaani na baadaye kuomba kurudi. Naona hataaminiwa kabisa kuliko sasa.

SOURCE: Mimi mwenyewe kwakuwa nipo nao katika mambo mengi.

Halima mdee amesema hawa ni Sisimizi na hawana madhara ndani ya Mchwa.
 
Mh! Naamini kuteleza si kuanguka, kama anahisi alipotoka basi
aombe radhi kwa viongozi wake ili waanze upya, la kama anaona
alikuwa sahihi basi aende CCM ambako ataendelea na mikakati
yake kumchafua Dk. Slaa na Chadema. Sioni kitu cha kumuweka
njia panda muda wote huu..

Mbona ni kama mnataka kumsemea si muache aamue mwenyewe.
 
Japo simjui vizuri mchange ni vema atulie kama best yangu chacha okong na dada zaituni(ex-katibu wa cdm nyamagana)[/QUOTE

Hawa jamaa inaonekana ni tishio kutoka kwao CDM, hadi inafikia wanaombwa watulie? Nadhani kuna mambo makubwa wamekifanyia chama lakini hakikuajali.
 
Mkuu, aina ya uzalendo wanaouonyesha vijana hawa si ile ambayo watu wengi wanaamini kuwa ni moja ya njia kuu za ukombozi.
Uzalendo wa kutumikia makundi ni lazima uwatie mashaka watu wenye lengo la kuijenga nchi


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Vijana wenye uzalendo wote walioko CDM lazima wataondoka na kutafuta mahali penye uhuru wa kuelezea hisia na malengo yao kwa taifa.
 
Mkuu sijawasumbua!.. Kama huamini haya niyasemayo basi tafuta namba ya simu ya mchange au mtembelee TABATA, utagundua yupo ktk wakati mgumu sana kisiasa. Pamoja na kuongoza UASI, lakini hakujua madhara yake yatakuwa ni kufukuzwa!...

Mbona malezezo yako yanonesha waziwazi unapiga propaganga tu, kama kweli una namba zao za simu si uweke hapa tujiridhe wenyewe, majungu ya nini mbona Mnyika anaweka za wabunge wenzake na mawaziri ili wananchi wawatukane.
 
Kwa nini toka mwanzo hakufanya hivi,Akili zako changanya na za kuwambiwa..........
 
Huyu Mchange ni ujinga tu unamsumbua. Atubu na kuomba radhi arudi Chadema. Vinginevyo, amepotea jumla.
Laiti wangejua kwamba akina Mwigulu na Nape wako pale kwa sababu ya kuishughulikia vizuri Chadema kupitia vijana hao wa masalia.
 
Nadhani bado Mchange ana nafasi ndani ya CHADEMA
 
Mleta uzi ni mnafiki tu,kwanini asiingie na jina lake la kweli?
 
Mbona malezezo yako yanonesha waziwazi unapiga propaganga tu, kama kweli una namba zao za simu si uweke hapa tujiridhe wenyewe, majungu ya nini mbona Mnyika anaweka za wabunge wenzake na mawaziri ili wananchi wawatukane.

Naheshimu sheria za JF: Namba ninazo siwezi kutoa, wewe tafuta.

  1. If you participate in any forum on the site, you warrant that you will not:
    • Defame, abuse, harass or threaten others
    • Make any bigoted, hateful, or racially offensive statements
    • Advocate illegal activity or discuss illegal activities with the intent to commit them
    • Post or distribute any material that infringes and/or violates any right of a third party or any law
    • Post or distribute any unethical, pornographic, vulgar, obscene, discourteous, or indecent language or images
  2. You are responsible for ensuring that any material you post on JAMIIFORUMS (text, images, or other multimedia content) does not violate or infringe upon the copyright, patent, trademark or any other personal or proprietary rights of any third party, and is posted with the permission of the owner of such rights.
 
Vijana wenye uzalendo wote walioko CDM lazima wataondoka na kutafuta mahali penye uhuru wa kuelezea hisia na malengo yao kwa taifa.

Sehemu ipi ya kusemea ambayo inanuka rushwa, ufisadi??? Ni sawa na kukataa kula chakula kwenye choo cha kuflash kisha ukakubali kula kwenye choo cha shimo!!!
 
Japo simjui vizuri mchange ni vema atulie kama best yangu chacha okong na dada zaituni(ex-katibu wa cdm nyamagana)[/QUOTE

Hawa jamaa inaonekana ni tishio kutoka kwao CDM, hadi inafikia wanaombwa watulie? Nadhani kuna mambo makubwa wamekifanyia chama lakini hakikuajali.

Unajustify kutaka kurudi nadhani umeona mlango unakufuri zito waombwa na nani masalia ,watu kama wanatoa maoni ni kukuomba embu tupe barua uliyoandikiwa kuombwa akina Mawazo wana impact ya papo kwa papo itakuwa masalia wachumia tumbo wanaotumiwa na wanaume wenzao
 
Back
Top Bottom