Habibu Mchange njiapanda

Habibu Mchange njiapanda

Vijana wenye uzalendo wote walioko CDM lazima wataondoka na kutafuta mahali penye uhuru wa kuelezea hisia na malengo yao kwa taifa.
Uzalendo wa kukosa adabu,kutukana watu wazima mpaka maumbile ya mwili wanamtukana Dr Slaa kilema cha mkono alichopata akiwa kazini lakini wakisahau mama mzazi wa mmoja wa kiongozi wa masalia amezaliwa mlemavu hakuna hata mtu mmoja amewahi kumtukana,masalia uzalendo wao uko matumboni mwao wenye uzalendo wamepotezea viungo,wengine wamekufa wengine wako mapolini wakieneza sera hao masalia waende wakatumiwe
 
Huyu brother, ameamua kutulia kwa muda na kujiepusha na ile mivutano ya kisiasa ya awali ili apate muda wa kujipanga upya..
Ndio tabu ya kufanya mahesabu vibaya,aliyemtuma yeye kabanishi kimya anaendelea na unaibu katibu mkuu,yeye taswira imevurugika dhamira inamsuta atulie asitulie is none of our business si mali kitu kwa taifa hili
 
Kama anachagua kuitukana CHADEMA ajue anapambana na NGUVU YA UMA na ni lazima itakuja kumjutisha,ni vyema aombe radhi CHADEMA ni watu wa kusamehe,akisamehewa ni lazma apige mzigo unaoonekana dhahiri shahiri.WELLCOME BACK brother.
 
Mleta uzi ni mnafiki tu,kwanini asiingie na jina lake la kweli?

Kumbe nyani haoni kundule!... Hivi wewe MAJEBELE, mdini - unaamini wewe si mnafiki?.. Mbona wewe hujaingia kwa jina lako?.. Kama hiki ni kigezo cha UNAFIKI, umepona?
 
HABIBU MCHANGE aka Mdude ambaye pia alikuwa kiongozi mkuu wa kikundi haramu cha MASALIA aka PM7 yuko njiapanda kuhusu hatma yake ya kisiasa.

Tangu kundi hili liliposambaratishwa (mwezi desemba mwaka jana), na kufia mbali (januari mwaka huu), kundi hili liliangukia katika mgogoro wa kuchagua mahali sahihi pa kwenda wote kwa pamoja lakini hawakuafikiana. Mazungumzo yao ya kawaida, mawasiliano yao na Vikao vyao vilikuwa na maeneo matatu ya kwenda: 1. Kuanzisha CHAUMA; 2. Kuhamia CCM 3. Kuhamia NCCR mageuzi. Pendekezo la kurudi CHADEMA na kuomba radhi lilipingwa na wengi, hasa Eddo, Mtela na Shonza.

  • Wazo la kuanzisha chama cha siasa (CHAUMA) - lilionekana kuwatisha wengi kwa kuhisi kuna kazi kubwa ya kukijenga chama hicho ili kiaminiwe na watanzania wengi!.

  • Wazo la kuhamia NCCR lilitolewa na EDDO ambaye amekuwa akitoa sababu za kwamba angependa aendelee kuwa mpinzani na tena vijana wengi walioenda NCCR wengi wao wamefanikiwa sana kisiasa. Wenzake walilikataa wakihofia kwamba chama hicho kitawapa wakati mgumu saana kujiuza.

  • Wazo la kuhamia CCM lilionekana kuungwa mkono na BWANA fedha na bibi fedha (FEDHA MAALUMU) za kutoka CCM (kuibomoa CHADEMA) na wengine kusitasita.

Tangu mwanzo Shonza na Mtela wao walionekana kuchagua kwenda CCM wakiwa na sababu:

1. Kimewasaidia sana kuwaweka mjini kwa zaidi ya mwaka mmoja. Hela hii imekuwa ikiwafikia wengine hata kabla ya kufukuzwa CHADEMA kupitia MTELA na mara nyingine SHONZA.

Hela za kutoka MASWA (ambapo katika awamu zote mpaka jumapili ya tarehe 24/2/2013 nilipowasiliana na mtela zinawafikia kupitia MTELA). Mtela alikuwa anapewa hela za maswa na muda mwingine za LUMUMBA na kuwafikishia wengine. Kwa mfano EDDO amekuja DAR zaidi ya mara 5 mwezi januari na februari akiwa hajalipwa mshahara miezi mi 3. Hapa ndipo alikuwa anatokea;

2. Wote walikuwa wameahidiwa AJIRA, ambapo mpaka sasa taarifa za ndani zinaonyesha kuwa atafanya kazi LINDI au MTWARA (siyo ualimu aliousomea wala si ukuu wa wilaya-kulingana na makubaliano ya awali na ya sasa). Shonza ameahidiwa kubaki Dar!.. AJIRA hizo wameahidiwa kupewa rasmi baada mizunguko ya kisiasa kuibomoa CHADEMA.

3. Ndani ya CCM watatafuta namna ya kujisafisha na kujitofautisha na mafisadi papa ili wagombee ubunge na kushinda. Mtela anaona akiwa CCM anaweza kuwa na nguvu MBOZI MASHARIKI kuliko kuwa NCCR. Vivyo hivyo Shonza analenga viti maalumu, jimbo la ubungo na jimbo la MBEYA mjini.

HABIBU Mchange kwa upande wake alisita sana kuhamia mapema kwa kuhofia kuchuja ZAIDI. Alibaki kuongoza chama cha wanamuziki wa kigoma LEKA DUTIGITE na kueandelea kula kwa jasho lao!. Hivi sasa yupo tayari kujiunga na CCM lakini ANASEMA KUWA anahofia kuporomosha IMAGE yake mbele ya jamii. Washauri wake wamemuambia akiamua kwenda CDM kuoma radhi muda huu hatapokelewa!. Wamemshauri aende CCM akatumie majukwaa yake kuisakama CDM na baadaye mwaka huu arudi na kuomba radhi kwenye mkutano mkubwa wa CDM!.. Huyu bro anaonekana kuukubali ushauri huu!..

MTIZAMO WANGU: Ni heri aende kuomba msamaha sasa (kama kweli ana nia ya kurudi) kuliko kuitukana CDM majukwaani na baadaye kuomba kurudi. Naona hataaminiwa kabisa kuliko sasa.

SOURCE: Mimi mwenyewe kwakuwa nipo nao katika mambo mengi.

Atabaki Dar kama chakula ya wenye chama. Nina hakika atakuwa na kazi ya kuikanda kila siku.
 
mchange huwa na chat naye sana na kumweleza mdogo wangu ulichemka sana
Cha msingi hapa ni ww kurudi chadema ukatubu dhambi zako jimbo la kibaha mjini bado ni lako na wana nchi wako badi wanakuamini sana utaingia bungeni kupitia kibaha mjini mchange rudi tubu dhambi zako utasamehewa



ushauri mzuri
 
Mleta uzi ni mnafiki tu,kwanini asiingie na jina lake la kweli?

wewe mwenyewe ni mnafiki,mbona pia umeshindwa kuingia na jina lako halisi na kuishia kutuhadaa na majebere?
 
Last edited by a moderator:
Chacha daniel okong tangu jina lake liondolewe kugombea ubunge nyamagana hajapanic km masalia ambao wanajimaliza wenyewe
 
chadema imegeuka..Mungu sasa;

naona wazee wa kanisa mkitoa comment zenu....ama kweli, no wonder matokeo ya form four vile

chadema bana.....mtafika muda mnapangia watu waoane na kuachana......
 
Mchange, kukosea kaumbiwa binadamu. Usife wala kuvunjika moyo kwa kugundua umekosea. Simama ueleze umma wa wapenda mabadiliko wa nchi hii ulivowasaliti na vile unajutia nafsi yako kwa makosa ulofanya.

Naamini, ukiomba msamaha wa kumaanisha mbele ya walalahoi tusioijua kesho yetu km makinda ya kuku, tunaovuja jasho usiku na mchana kujikwamua kiuchumi bila mafanikio kutokana na mifumo duni ya utawala wa ccm na tuliowekeza imani zetu kwenu tukiamin ni wapiganaji wa kwel ktk kutukomboa kutoka hali duni za kimaisha, utasamehewa.

natamani nijaze kurasa kukushauri lkn pokea hilo kwa leo na nitoe nafasi kwa wengine watoe yao ya moyon.

yes u can habib mchange
 
Last edited by a moderator:
Mchange , hakuna mkamilifu na wakati mwingine tamaa huzidi mtu na hata kukengeuka .Kama unadhani una nia ya dhati ya kufanya kazi kwa amani basi rudi Chadema .Nitafute mimi mimi hapa nitakushika mkono na nitaongea mbele zao nawe uwaangukie urudi kundini .Acha mahangaiko ya kimwili na kiroho muda una enda .Ukitoka Chadema hutakuwa salama .Wenzako hawako salama na kama huamini tulia utaona siku za karibuni .Laana kubwa inakuwakumbuka wale .Chadema watu wamepoteza maisha, wamekuwa masikoini kuichangia Chadema kwa matumaini leo unaanza kuwageuka wavuja jasho la kweli hakika huwezi kuwa salama .Rudi Chadema utakiwa salaama.
 
Back
Top Bottom