HabariLeo kufungiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HabariLeo kufungiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masatu, Nov 7, 2008.

 1. M

  Masatu JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimekutana na habari hii kwenye Gazeti la Mwananchi inayotaja jina la Mh Mkuchika na kujiuliza kama ule "mgomo" umekwisha au laa

   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  .....Subiri akina FMES, Mwanakijiji na akina Halisi walete uthibitisho na the dataz, otherwise huu utakuwa "udaku!"
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu SteveD

  Udaku kivipi? nimeweka bandiko la gazeti la Mwananchi na kumalizia na swali sasa udaku unatoka wapi?

  Hii ni standard mpya hapa JF.....
   
 4. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Say whaaaaat ?

  I don't know if it is the drugs you are taking or the drugs you need to be taking!

  But do something!
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hapana Mkuu Masatu, kamwe hii siyo standard mpya. Nami, na naamini wengi wetu pia hatupendelei yeyote yule aiendekeze. Ahsante.
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  It hurts my friend. It does hurt.

  To be told ''huo ni udaku," it does hurt.

  Baadae mkuu. Thanks for your objection.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Nov 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mbona swali haliendani na unachozungumzia... liulize swali lako vizuri. Vinginevyo nikisema "haujakwisha" utasema mbona "mwananchi".. na nikisema umekwisha utaluliza "mbona".. nikisema kuwa bado upo ila mwananchi wameamua kuuvunja (inaitwa crossing the picketing line) utasema "kumbe wahariri.."..

  so.. swali zuri ni kuwaandikia "mwananchi" na kuwauliza hili swali..
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,702
  Trophy Points: 280
  Date::11/7/2008
  Serikali yajikuta katika mtego wa kuliadhibu gazeti lake
  Na Daniel Mjema, Dodoma
  Mwananchi

  SERIKALI imekiri kuwa gazeti lake la Habari Leo liliandika habari ya uchochezi na kuliahidi Bunge kuwa italichukulia hatua zinazostahili gazeti hilo.

  Hatua hiyo ya serikali inafuatia agizo la Bunge kwamba ilichukulie hatua kali gazeti hilo kwa kuchapisha habari za uchochezi dhidi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali na Rais Jakaya Kikwete.

  Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo baada Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, kulalamika kuhusina na kitendo cha gazeti hilo la serikali kuchapisha habari hiyo.

  Awali mbunge huyo aliomba mwongozo wa Spika jana kuhusiana na habari hiyo akisema kuwa ni nzito na ya uchochezi kuliko iliyoandikwa na gazeti la MwanaHALISI lililofungiwa miezi mitatu hivi karibuni na waziri huyo.

  Habari hiyo iliyochapwa Jumatano wiki hii katika toleo namba 636 ilikuwa na kichwa cha habari likichosema ‘Kundi la wabunge wa CCM lasuka zengwe la EPA” na kuelezea njama za wabunge hao wa CCM kumpinga Rais kuhusu hatua zake dhiti ya watuhumiwa wa EPA.

  Ole Sendeka alisema habari hiyo ni ya uchochezi mkubwa, hasa inapodai kuwa zipo njama za wabunge wa CCM za kumpinga Rais Jakaya Kikwete kuhusu uamuzi wake katika sakata la kashfa ya fedha za EPA.

  Mbunge huyo alisema gazeti hilo limejenga hoja kuonyesha kwamba wabunge hao wa CCM wamekuwa wakitumiwa na watu waliopo nje ya Bunge kupinga maamuzi ya Rais baada ya kuagiza kuwa watuhumiwa wafikishwe kortini.

  Ole Sendeka alisema habari hiyo ni nzito na ya uchochezi kuliko ile ya gazeti la MwanaHALISI, kwa sababu inawagombanisha wabunge hao na Serikali pamoja na Rais na kutaka mwongozo wa Spika ni hatua gani zitachukuliwa.

  Baada ya maelezo hayo, Spika Samwel Sitta aliungana na Mbunge huyo na kusema kuwa hata yeye alishtuka sana aliposoma habari hizo na kuongeza kuwa huo ni mchezo mchafu ambao serikali inapaswa kuuchukulia hatua kali.

  “Hata mimi nilishtuka sana niliposoma habari hiyo, kwa kweli ni mchezo mchafu sana, ingekuwa imeandikwa na gazeti hovyo hovyo hivi tusingeshangaa sana, lakini hili ni gazeti la Serikali,” alisema Sitta.

  Sitta ambaye alionekana kukerwa na habari hiyo aliongeza kusema kuwa: “Linapokuwa limechapisha gazeti la Serikali, hili ni jambo zito sana, hivyo naagiza wahusika waliotajwa na gazeti hilo waandike malalamiko rasmi kwa waziri husika”.

  Spika alisema pamoja na wahusika ambao ni wabunge wa CCM, kuwasilisha malalamiko hayo na kupeleka kwa waziri nakala za gazeti hilo, Bunge litafuatilia kujua hatua zilizochukuliwa dhidi ya chimbo hicho cha habari cha serikali.

  Mara baada ya maelezo hayo , Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, ambaye ndiye aliyelifungia gazeti la MwanaHALSI alisimama na kukiri kuwa gazeti hilo la serikali kuandika habari hizo za uchochezi.

  Hata hivyo, alisema kuwa wizara yake imekwishachukua hatua kwa kuwaandikia wahusika kuwataka wajieleze kuhusu ukweli wa habari hiyo na baada ya kupokea maelezo hayo serikali itachukua hatua zinazostahili.

  Pamoja na maelezo hayo, Spika alimweleza waziri huyo kuwa ni vyema taarifa ya jinsi serikali ilivyolishughulikia suala hilo iwasilishwe katika ofisi ya Spika ili naye aishirikishe Kamati ya Bunge ya Maadili.

  Mwezi mmoja uliopita serikali ililiufnugia kwa miezi mitatu gazeti la MwanaHALISI kwa maelezo kwamba limeandika habari ya uchochezi iliyokuwa na kichwa kisemacho: ‘Njama za kungoa Kitwete zafichuka’, ambayo ilieleza kwamba ndani ya CCM kuna watu wanataka kumzuia Rais Kikwete asigombee urais tena kipindi cha pili.

  Waziri husika alisema serikali imechukua hatua kwa sababu gazeti hili imeandika habari yenye lengo la kumchonganisha Rais na mtoto wake aliyedaiwa kutumiwa na kundi la baadhi ya vigogo wa CCM wanaotaka kumwengua ili asigombee kipindi cha pili.

  Hatua ya waziri huyo kulifungia gazeti hilo kilipingwa na wadau mbali mbali wa habari na kufuatiwa na maandamano ya amani ya wahiri wa vyombo vya habari nchini hadi katika ofizi za wizara hiyo wakiwa wameziba midomo na gundi ya karatasi au plasta.
   
 9. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Acha ku obfuscate.

  Unaweza kusema ni udaku, kinachonishangaza ni pale unaposema tusubiri FMES, Mwanakijiji na Halisi waje wathibitishe.

  Kama nilivyosema, sijui leo ume consume nini, au umesahau ku consume ambacho huwa inabidi u consume ili uwe Ok.
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wewe wasema.
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hivi mbunge mmoja atajuaje kwamba hakuna kikundi cha wabunge chenye mkakati, hususan wa siri, wa kumpinga rais?

  Kinachopingwa hapa si uchochezi, bali ni uhuru wa vyombo vya habari.
   
  Last edited: Nov 7, 2008
 12. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  duh! aste, aste kuhani
   
 13. M

  Masatu JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Si usemi halafu tuulize unajibu ndio maana ya mjadala majibu yanaleta maswali mengine
   
 14. M

  Mama JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  ha ha ha haaaaa; Steve mwanangu, you've made my day! !! LoL!
   
 15. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hawa Mwananchi wanaweza kuwa hawajavunja yale makubaliano ya kususia habari za Mheshimiwa Mkuchika, lakini kuna habari huwa ni muhimu kuziripoti, na huwezi kuziripoti bila kutaja source ya hiyo habari. Hapa kikubwa wanachoonesha Mwananchi (kama nao wamemsusia) ni habari kama ilifanya Gazeti la Kubenea lifungiwe, imeripotiwa katika gazeti la Serikali. Na kuonesha majibu ya Waziri amabayo yanatupasa sasa sisi wasomaji tukumbuke hatua za Waziri kwa yaliyolikuta gazeti la Kubenea. Hivyo bila kumtaja hapo Mkuchika, habari itakosa ladha.
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa Mwananchi hawajavunja makubaliano ya mgomo. lengo hasa la mgomo ni kumnyima Mkuchika sauti ya kufikishia ujumbe ambao ni advantage kwake, Ila jambo lolote ambalo ni negative kwake linaloweza kumbomoa litakuwa ni good shot for media, "Mfano Mkuchika akishikwa ugoni", au kama hii ya kuonesha kuwa yupo biased na hafai. Kwa ujumla ni kwamba anything on postive of Mkuchika ni kuvunja makubaliano ila negative ni kuendeleza makubaliano.
   
 17. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wenzao wa Nipashe waliandika habari ya Mkuchika lakini wakataja cheo chake tu. Kwenye jina wakaweka XXXX. Tena walikuwa wanafanya reference ya viongozi wa CCM walioingia ambao wabunge wa CCM wanataka waondolewe pamoja na Makamba.

  PM
   
 18. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  This is very interesting. I can't wait to see the government punishing itself. Sasa hili la kutaja Mkuchika, I guess it was inevitable. You want to report a piece of exciting news, and to make the news more exciting, you have to mention the name of the person who is responsible kufungia magazeti. It was really inevitable. Naomba hoja hapa isiwe kuhusu kutajwa kwa Mkuchika, bali kama kweli serikali italifungia gazeti lake.
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mimi nimegundua kitu kikiletwa humu Asipo ongea MMJ au FES basi ni udaku au watu hawachangii hii ni uwazi kabisa jaribu kufuatilia hizi bias inabidi ziangaliwe hapa JF,.
   
 20. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nadhani hujaelewa mantiki ya SteveD.It's satirical!
   
Loading...