Habari zenu

Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,422
91
Napenda kuchukua fursa hii kuandika kwa mara ya kwanza kuwaomba mnipokee kwenye forum.
 
Ni kweli nimegundua kuwa hapa yanaandikwa mambo ya mapenzi. Nadhani nitakuwa sijakosea tena kana nitaweka kisa changu cha mapenzi.

Ni mama wa watoto kadhaa. Nina work mate wangu (baba wa watoto kadhaa) ambaye tulikuwa tukiflirt kwa muda wa miaka 2, ila saa za kazi tu, kuanzia saa mbili hadi saa kumi jioni, na wakati mwingine usiku kama tupo safarini. Hatuendi lunch pamoja wala hatuna tabia ya kuwa pamoja. Mara nyingi tunakutana kwenye vikao. Mapenzi yetu ni kwa simu tu.

Majuzi kati hapa aliomba kuvunja amri ya sita. Moyo unataka ila mwili unakataa. Nimeamua kumwambia tusitishe mawasiliano, tunajaribu lakini inashindikana kwa vile tuko ofisi moja. Tukionana tu ndo unakuwa mwanzo wa kuanza kupigiana simu za mapenzi. Je kuna mapenzi kati yetu au ni tamaa za mwili? Ntajuaje au nimpe test gani kugundua kuwa ananipenda kweli.
 
Jamani Umpe test??sumu haijaribiwi kwakunywa!!
Wewe kama unamtaka msikilize kwani yakufaa kujua kama yeye anamwelekeo gani kwani hakawii kula tunda akaanza mkabaki kwenye simu!!ila kama unampenda mpeee kibrudisho!!
 
Jamani Umpe test??sumu haijaribiwi kwakunywa!!
Wewe kama unamtaka msikilize kwani yakufaa kujua kama yeye anamwelekeo gani kwani hakawii kula tunda akaanza mkabaki kwenye simu!!ila kama unampenda mpeee kibrudisho!!

Nadhani sio busara 'kumburudisha' tu kwa vile najihisi kumpenda. Nitajuaje kama ananipenda?
 
Wewe umesema una watoto, umeolewa?
Huyo naye ana watoto, ameoa?
If majibu ya juu yote ni YES, you are in trouble my friend,
If majibu ya juu yote ni NO, then you can Go ahead, not only with office love but NDOA,
If one of the answers above is YES, MY DEAR "DO NOT TRY THAT AT HOME"
 
lady amemaliza kila kitu hapo mie sina cha kuongeza ila unakaribishwa kuchangia na post zingine
 
Wewe umesema una watoto, umeolewa?
Huyo naye ana watoto, ameoa?
If majibu ya juu yote ni YES, you are in trouble my friend,
If majibu ya juu yote ni NO, then you can Go ahead, not only with office love but NDOA,
If one of the answers above is YES, MY DEAR "DO NOT TRY THAT AT HOME"

Kwanini unaamsha waliolala bwana, huyo ni mwanachama wetu mpya kwenye ISC
 
Ndo mana wapemba na waunguja wanaenda wao sokoni na kwenye kazi zao wenyewe..!
masokonina maofisini kuna mambo.!
 
Wewe umesema una watoto, umeolewa?
Huyo naye ana watoto, ameoa?
If majibu ya juu yote ni YES, you are in trouble my friend,
If majibu ya juu yote ni NO, then you can Go ahead, not only with office love but NDOA,
If one of the answers above is YES, MY DEAR "DO NOT TRY THAT AT HOME"

Wote tupo na kenye ndoa zenye furaha na kujali familia.

Kinachonitatiza sio kujua madhara ya huu uhusiano, no. Kinachonitatiza ni jnsi ya kujitoa. Huyu mwenzangu wa pili ni kijana ambaye hakuna mwanamke atamkataa, hana kashfa na mapenzi wala hajui ugomvi kwa miaka 5 niliyomjua, mchapakazi, anayejali familia, mwenye upendo, mwenye heshima, si mlevi wala mvuta sigara. Siku hizi amnientitlle mke wake (kwenye simu).

Naomba ushauri au msaada wa kumzuia uhusiano usianza. Natamani ningeisoma hii thread miaka miwili iliyopita.

Nakikiria kuacha kazi hapa - ila ninafanya kazi ya ndoto yangu, ninaipenda kazi yangu.

Nikifikiria kuhama mji - mume wangu hatokubali.

Sijalala kabisa kama wengine wanavyofikiria hapa. Nina uzoefu wa purukushani za mapenzi na ndoa.
 
karibu kundini ila unatakiwa ujue sheria zote za INFIDELATORS/INFIDELETEES

Naomba kinukuu kama Mwenyekiti alivyo ainisha kwenye KATIBA role number 6. lazima awe na ''defined-marital status'',lazima awe ameoa/ameolewa (huwezi kufanya infidelity wakati wewe hujaoa-hapo unakuwa unafanya zinaa tu!...infidelity kwa ujumla wake lazima kwanza uoe/uolewe .
 
Si conduct infidelity, kundi lenu lishindwe na lilegee kwa jina la Bwana.
 
role number 2-INFIDELATORS/INFIDELETEES wanatakiwa kufanya wanaloliweza kuhakikisha hakuna leakage ya taarifa yoyote ya INFIDELITY juu yako kwenye familia zao(hasa hasa wake/waume zao waliowaacha nyumbani)

role number 8: watahakikisha wanapigana kufa na kupona kuzilinda na kuzitetea ndoa za infidelators/infideletees wenzao!(ndoa na iheshimiwe na watu wote).naomba hii sheria muiangalie kwa umakini mkuu!hakikisha kufa kupona unafanya unaloweza kuhakikisha ndoa ya mwanachama haitetereki.

role number 9:INFIDELITY itafanyika NYUMBA ZA KULALA WAGENI TU!.... tena itafanyika kilometa kadhaa kutoka maeneo yako ya nyumbani(otherwise unatakiwa uproove kwamba mkeo/mumeo kasafiri umbali usio pungua kilometa mia saba kutoka nyumbani kwenu).

role number 10: INFIDELITY KAMWE HAIFANYIKI USIKU KUCHA-fanya unalofanya lakini make sure umerudi nyumbani kwa waif/husband.ukilifanya hili utakuwa umeheshimu na kuitekeleza sheria namba 7 na namba 9 tajwa hapo juu

UKIZINGATIA KANUNI HIZI UTAKUWA UMEKATA KIU YAKO
 
wewe una mke au girlfriend? acha kudandia meli za watu zingine zina sumu "kila ngedere umuonaye mjini ujue anamweyewe"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom