Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 871
Hakimu wakati anaikaribia nchi ya kusadikika..
Ndugu zangu,
Naziona ishara za wakati unaokaribia. Ni wakati utakaotoa hukumu isiyobakisha maswali kwa watu wa kusadikika.
Ni hukumu itayodhihirisha, kuwa yale yote yalokuwa yakisemwa na akina sadiki ni batili.
Kwa vile wasadikika wanaamini katika historia, kuwa ni mwalimu wao mzuri, basi, huamini pia, kuwa wakati ni hakimu wao mwema.
Kihistoria, wasadikikika huwa na hulka ya kufanya mzaha kwanza, kisha huamka dakika za mwisho. Hata kama ni mzaha wenye hatari ya kupelekea maangamizo ya taifa lao la kusadikika.
Ndio, wasadikika ni wenye hulka ya kuitafuta fimbo baada ya nyoka kuwauma na kuwaachia sumu kali yenye kusambaa kwenye miili yao.
Naam, hakimu wakati anakaribia kukanyaga ardhi ya nchi ya kusadikika.
Nimeziona ishara...