Habari za kina udhuru, daily noise na tibii sii hii!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari za kina udhuru, daily noise na tibii sii hii!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by akili, Jan 3, 2009.

 1. a

  akili Member

  #1
  Jan 3, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UNAPOSOMA au kusikiliza habari zinazoandikwa na magazeti fulani fulani nchini ambayo yana wenyewe au kusikiza za redio za wenyewe au kutazama televisheni ya mwenyewe jiulize maswali kadhaa na hasa kama magazeti hayo yanaandika habari za wanasiasa wa vyama mbadala.

  Inavyoelekea VISHENI ya vyombo hivyo vya habari NI KUWA NA TANZANIA ISIYO NA DEMOKRASIA NA USHINDANI WA HAKI NA HALALI WA KISIASA.

  Na MISHENI ya magazeti haya ni kuandika habari za umbeya, uchochezi na unafiki chini ya mwamvuli wa watawala na kuhakikisha Watanzania wanabaki daima katika giza kuhusu faida na manufaa ya ushindani na demokrasia.

  Waandishi wake kwa maneno machachi ni WAHUJUMU WA DEMOKRASIA na misingi yote ya uandishi wa habari unaojali ukweli, haki na maslahi ya walio wengi.

  Kuna watu unaweza kuwatema mate, lakini hawa wanafaa kuwapengea kamasi popote pale utakapowaona.
   
 2. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hapa sijajua unataka kuongelea nini. labda unavyotoa tuhuma kama hizi, uje na mfano hai. lakini pia hivi vyombo sasa hivi ni mashirika tofauti yanayojitegemea
  1. UHURU ni chombo cha CCM hivyo huwezi kukilaumu kinapoipendelea CCM na kughandamiza vyama vingine ni kama ilivyo kwa TANZANIA DAIMA
  2. DAILY NEWS NA HABARI LEO nazo sipo chini ya TSN na ni shirika la habari la umma
  3. TBC nalo ni shirika lingine la umma

  Kwa maoni yangu TBC na dailynews zimebadilika kiasi fulani ni tofauti na zamani. Pia kila chombo kina vision yake na kina pendelea upande fulani "to be frank" sidhani kama utapata chombo ambacho kipo neutral vitakuwepo vichache sana. chamsingi hapa pokea taarifa toka vyombo vyote na wewe uvichuje.
   
Loading...