Habari njema: Kampuni ya Uganda yaleta boat ziwa Victoria

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Wakati wakazi wa Kagera na Mwanza wakisubiria ahadi hewa ya miaka mingi ya serikali ya kuletewa meli mpya baada ya kuzama kwa MV Bukoba, kampuni binafsi ya Uganda ya Equetorial Wild Safaris imeleta boat ya mwendo kasi ambayo kwa sasa ipo katika majaribio ziwa Victoria.

Boat hiyo itatatua kwa kiasi kikubwa adha ya usafiri ziwa Victoria na kuongeza chachu ya utalii kwa watalii wanaopitia Jinja,Entebe /Uganda kutembelea hifadhi ya Serengeti.

Boat Victoria.png
 
Wakati wakazi wa Kagera na Mwanza wakisubiria ahadi hewa ya miaka mingi ya serikali ya kuletewa meli mpya baada ya kuzama kwa MV Bukoba, kampuni binafsi ya Uganda ya Equetorial Wild Safaris imeleta boat ya mwendo kasi ambayo kwa sasa ipo katika majaribio ziwa Victoria.

Boat hiyo itatatua kwa kiasi kikubwa adha ya usafiri ziwa Victoria na kuongeza chachu ya utalii kwa watalii wanaopitia Entebe /Uganda kutembelea hifadhi ya Serengeti.

View attachment 441950

Asante sana, hebu tudonolee kidogo kuhusu route, ratiba na capacity yake, ili sisi wahanga wa tetemeko tutetemekee humo badala ya kuzunguka Chato!!!
 
Hili ziwa ni economical potential sana ukizingatia ni ukanda ulio na idadi kubwa ya watu na vitu lakini basi tu, kila mtu anakimbilia kuweka vyombo kama hivi dar wakati pesa ya kutosha ipo kwenye hili ziwa. Ukianzisha route za Jinja, Bukoba na Mwanza ni lazima upige pesa ya maana sana bila kusahau watalii kibao badala yake hili ziwa halijatumiwa vya kutosha, watu wanaigana na ubunifu ziro.

Waanze tu mapema ili niingie nayo likizo home mwezi huu, watapiga pesa sana
 
Mkuu Rweye ni kweli mkuu, Ziwa victoria lina pesa nyingi sana sema ndio hivyo serikali haijatilia mkazo. Wafanyabiashara wengi kati ya Bukoba na Mwanza wanalitegemea sana kusafirishia bidhaa.
 
Msijali vuteni subira, serikali sikivu ya ccm italeta boat kubwa na nzuri kuliko hiyo ya m7
 
Hili ziwa ni economical potential sana ukizingatia ni ukanda ulio na idadi kubwa ya watu na vitu lakini basi tu, kila mtu anakimbilia kuweka vyombo kama hivi dar wakati pesa ya kutosha ipo kwenye hili ziwa. Ukianzisha route za Jinja, Bukoba na Mwanza ni lazima upige pesa ya maana sana bila kusahau watalii kibao badala yake hili ziwa halijatumiwa vya kutosha, watu wanaigana na ubunifu ziro.

Waanze tu mapema ili niingie nayo likizo home mwezi huu, watapiga pesa sana
Ccm ni janga la kimataifa.
 
Bravo sera za Museveni, zimesaidia mambo mengi Mkoa wa Kagera.
Museveni ni mkombozi mkubwa wa ukanda huu na kusema kweli hana kinyongo hata kidogo na bifu za kishamba kama mijamaa mingine
 
Mkuu Rweye ni kweli mkuu, Ziwa victoria lina pesa nyingi sana sema ndio hivyo serikali haijatilia mkazo. Wafanyabiashara wengi kati ya Bukoba na Mwanza wanalitegemea sana kusafirishia bidhaa.
Viongozi wabaguzi wa Tanzania na roho za kwanini huwa wanahisi wanaikomoa mikoa ya ukanda huu kumbe wanalihujumu hata ziwa letu na uchumi wa nchi. Kuna nchi ambazo zinalia kuwa na 51% ya ziwa hili kama ilivyo kwetu ili walitumie kimaendeleo sema hawana, sie tuliopewa bure tumekaa dar ..kila siku kila kitu dar. Hivi tusingekuwa na bahari ina maana Tz tusingekuwa na uchumi wa maana?

Hili ziwa ukiamua kuweka meli mbili kwa gharama ya 70bn moja ya abiria moja ya mizigo ikawa ni route Tz, Uganda na Kisumu Kenya hakika return yake haiwezi kulinganishwa na bombadier za 130bn hata zingekuwa tatu. Kwa hesabu ya haraka haraka laiti ile pesa ingenunulia meli pale Victoria naamini pesa ingekuwa imerudi nyingi ya kutosha na kubadili maisha ya wananchi walio wengi zaidi kuliko tulivyojichanganya na mandege haya yaso na tija kwa sahivi

Huwezi ukaiangalia sekta ya usafirishaji na kusaidia uchumi wa wananchi kwa haraka na kwa quantity kubwa unaanza na ndege na kuàcha treni ama meli, akiri za hivi ni za Watanzania pekee chini ya CCM
 
Hili ziwa ni economical potential sana ukizingatia ni ukanda ulio na idadi kubwa ya watu na vitu lakini basi tu, kila mtu anakimbilia kuweka vyombo kama hivi dar wakati pesa ya kutosha ipo kwenye hili ziwa. Ukianzisha route za Jinja, Bukoba na Mwanza ni lazima upige pesa ya maana sana bila kusahau watalii kibao badala yake hili ziwa halijatumiwa vya kutosha, watu wanaigana na ubunifu ziro.

Waanze tu mapema ili niingie nayo likizo home mwezi huu, watapiga pesa sana

Mkuu Rweye, hapo naona Uganda itakuwa imefanya jambo la maana sana, wasi wasi wangu ni kuhusu maharamia wanao tumia speed boats kupora wavuvi na kuvamia visiwa, je, watashindwa kuvamia passengers watajao safiri na boat hiyo ya Uganda? wahusika wajipange vizuri jinsi ya ku deal na usalama kabla ya kuanza biashara, Ziwa Victoria siku hizi kuna uharamia mwingi hilo tusilisahau.
 
Hatujitambui.!ukiangalia hata tovuti ya bodi ya utalii kuna maeneo yenye vivutio vya utalii havijabainishwa na kuingizwa kwenye tovuti.
Sehemu na Upande wa kuanzia Mkoa wa Rukwa,Kigoma,Mtwara n.k vivutio vimeachwa,na hivyo kukosesha nchi mapato yatokanayo na utalii.
Ngoja tujifunze kutoka kwa wenzetu ambao fursa wanaziona kwenye himaya yetu!
 
Hili ziwa ni economical potential sana ukizingatia ni ukanda ulio na idadi kubwa ya watu na vitu lakini basi tu, kila mtu anakimbilia kuweka vyombo kama hivi dar wakati pesa ya kutosha ipo kwenye hili ziwa. Ukianzisha route za Jinja, Bukoba na Mwanza ni lazima upige pesa ya maana sana bila kusahau watalii kibao badala yake hili ziwa halijatumiwa vya kutosha, watu wanaigana na ubunifu ziro.

Waanze tu mapema ili niingie nayo likizo home mwezi huu, watapiga pesa sana

Said Bakhresa aliwahi kutaka kupeleka boti zake kule ziwa Victoria wakati ule Magufuli akiwa Waziri wa miundombinu akakataa kwa kusema kusafirisha boti hizo kutaharibu barabara zetu

Hivyo waliwahi kutaka kupeleka huko boti hizo wakazuiliwa naona Uganda inatumia fursa vizuri!
 
Jamaa ana PhD lakini kufikiri kwake wakati mwingine unaweza kufikiri labda ndo kamaliza elimu msingi juzi juzi
 
Hatujitambui.!ukiangalia hata tovuti ya bodi ya utalii kuna maeneo yenye vivutio vya utalii havijabainishwa na kuingizwa kwenye tovuti.
Sehemu na Upande wa kuanzia Mkoa wa Rukwa,Kigoma,Mtwara n.k vivutio vimeachwa,na hivyo kukosesha nchi mapato yatokanayo na utalii.
Ngoja tujifunze kutoka kwa wenzetu ambao fursa wanaziona kwenye himaya yetu!
Hivi mkuu unaelewa ni kwa kiasi gani ziwa victoria limesheheni beach za maana sana? ila kaangalie kama hata zinaongelewa. Sie miaka nenda rudi akili zetu zinaishia kwenye mbuga, bagamoyo na kilimanjaro, ni fitina na ubinafsi ndo vinawapa waganda nafasi ya kuja kuwekeza bongo wakati sie daily tupo na majungu yetu
 
Back
Top Bottom