Artificial intelligence
JF-Expert Member
- Jan 28, 2021
- 1,262
- 2,191
Historia ya Mkoa kabla ya Uhuru
Kabla ya Uhuru na hadi kufikia mwaka 1961, eneo la sasa la Mkoa wa Kagera, lilikuwa ni moja ya maeneo yaliounda jimbo lililoitwa “Lake Province”. Jimbo hili lilijumuisha Wilaya za Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora. Baada ya uhuru mwaka 1962 mkoa ulibadilishwa jina na kuitwa ‘West Lake Region’ (Ziwa Magharibi) na kujumuisha Wilaya 4 za Ngara, Biharamuro, Karagwe na Bukoba.
Kabla ya mwaka 1979, mkoa huu wa Kagera ulikuwa unaitwa “Ziwa Magharibi”. Jina hilo lilibadilishwa na kuwa “Kagera” mwaka 1979, mara baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda, ambapo mkoa, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, aliyekuwepo wakati huo, Capt. Peter Kafanabo, ulipendekeza uitwe “Kagera”. Pendekezo la kuubadlisha jina Mkoa wa Ziwa Magharibi na kuitwa Kagera lilitokana na Mto Kagera kugusa sehemu kubwa ya wilaya zote zinazounda mkoa huu ukiwa unatiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia kaskazini na kumwaga maji yake katika Ziwa Victoria.
MATUKIO MAKUU 1962 – 2021
Katika kipindi cha miaka sitini tangu tupate uhuru yapo matukio mengi ya kihistoria ambayo yametokea katika mkoa wa Kagera. Mtiririko wa matukio hayo ni kama yanavyoainishwa hapa chini.
Mwaka 1962
Mafuriko: Mvua kubwa ilinyesha na mafuriko kutokea sehemu kubwa ya Mkoa, ambapo wananchi waliipa jina la “Mvua ya Uhuru” kwa sababu mvua kubwa ya masika ilinyesha baada ya Tanganyika kupata Uhuru.
Mwaka 1966
Ukame: Ukame mkubwa uliodumu hadi mwaka 1970 watokea na kusababisha njaa kali katika wilaya ya Karagwe. Hali hiyo ilisababisha baadhi ya watu kupoteza maisha, kupungua kwa nguvukazi, baadhi ya familia kukosa matunzo kwa ukaribu baada ya wanaume kwenda maeneo ya mbali kutafuta chakula.
Mwaka 1978
Vita kati ya Tanzania na Uganda: Mwezi Oktoba 1978 kulitokea vita kati ya nchi ya Tanzania na nchi ya Uganda. Vita hii ilijulikana kwa jina maarufu la “vita ya Kagera” iliitwa jina hilo kutokana kwamba ilipiganiwa katika ardhi ya Tanzania mkoani Kagera.
Vita hii ilisababishwa na kitendo cha Majeshi ya Uganda, chini ya Nduli Idd Amin Dada, kuvamia ardhi ya Tanzania katika eneo la Missenyi na kudai kuwa eneo lote lililo kaskazini mwa Mto Kagera ni ardhi ya nchi ya Uganda. Vita hivyo vilimalizika mwezi April, 1979 kwa Majeshi ya Tanzania kushinda vita na kumuondoa madarakani Nduli Idd Amin.Vita hivi vya Kagera vilikuwa na athari kubwa kwa mkoa wa Kagera. Athari hizo ni pamoja na vifo, wananchi kunyang’anywa mali zao na uharibifu wa miundombinu ya majengo na barabara.
Mwaka 1983
Operesheni Uhujumu Uchumi: Kutokana na kukosekana kwa bidhaa muhimu katika jamii na kupungua kwa uwianao wa kipato kati ya walio nacho na wasio nacho serikali iliendesha operesheni dhidi ya wahujumu uchumi nchi nzima. Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera walitupa bidhaa zao kwenye Ziwa Victoria na mto Ngono ili kuhofia kukamatwa na Serikali.
Kugunduliwa kwa Mgonjwa wa UKIMWI: Ugonjwa ambao unadhoofisha kinga za mwili za kujikinga na maradhi ambao baadae ulikuja kujulikana zaidi kama UKIMWI (Ukosefu wa Kinga Mwilini) uligundulika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mkoani Kagera.
Mgojwa wa kwanza aligundulika kuwa na virusi vya UKIMWI alitoka katika Kijijini cha Kanyigo Wilaya ya Missenyi. Mwanzoni wananchi wa Mkoa wa Kagera waliuita ugonjwa huo “Juliana” au “Slim”. Uliitwa Juliana kwa sababu iliaminika kuwa ugonjwa huo uliingizwa nchini na vijana waliokuwa wakitokea Uganda wakiwa wamevaa mashati ya Juliana. Pia uliitwa ‘slim’ kwa sababu waathirika wa ugonjwa huo walikuwa wanakonda hadi kufa. Ugonjwa huu baadae ulienea Tanzania nzima na kuleta athari kubwa katika jamii. Mkoa wa Kagera ulikuwa wa kwanza kuathirika. Ugonjwa huu uliwakumba zaidi vijana, wanajamii ambao wanaotegemewa sana katika uzalishaji mali. Vijana wengi wakaangamia kwa UKIMWI na kufanya familia nyingi kubaki na wazee wakibeba mzigo wa kutunza watoto yatima. Pia muda mwingi wa kuzalisha mali ulipotea katika kuhudhuria mazishi na matanga ya ndugu na jamaa, kuuguza wagonjwa na kutunza yatima. Ugonjwa wa UKIMWI bado upo mpaka sasa katika mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla.
Mwaka 1994
Kuingia kwa Wakimbizi wa Rwanda na Burundi: Kutokana na mapigano ya kikabila nchini Burundi na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, inakadiriwa kuwa Wanyarandwa na Warundi laki sita (600,000) waliingia mkoani Kagera wakikimbia mapigano hayo. Ujio wa wakimbizi ulisababisha madhara makubwa kwa mkoa wa Kagera
yakiwemo uharibifu wa mazingira na kushamili kwa uhalifu mwingiliano wa utamaduni na kuzaliana.
Mwaka 1995
Mvua kubwa: Mvua kubwa ilinyesha na kusababisha mafuriko na uharibifu wa mazao na miundombinu.Mafurikoyaliathiri sana Wilaya yote ya Bukoba na Missenyi. Madaraja yalisombwa na maji hivyo kuathiri watumiaji na baadhi ya nyumba za watu ziliharibiwa.
Mwaka 1996
Kuzama kwa MV Bukoba: MV Bukoba ikiwa safirini kutoka Bukoba kwenda Mwanza, ilizama katika Ziwa Victoria kilomita nane kabla ya kufika bandari ya Mwanza. Inakadiriwa kuwa watu mia nane (800), wengi wao walikuwa wakazi wa mkoa wa Kagera, walipoteza maisha huku mali yenye thamani ya mamilioni ya shilingi ilipotea. Sababu za kuzama kwa meli hiyo kulisababishwa na ujazaji wa abiria na miziko kupita uwezo wake.
Mwaka 2016
12 Septemba 2016
Tetemeko la ardhi la nguvu ya 5.7 katika vipimo vya Richter lilitokea eneo la Bukoba, kaskazini magharibi mwa Tanzania na kusababisha maafa.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa takriban kilomita 44 kutoka mji wa Bukoba, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Kagera, kwa mujibu wa taasisi ya jiolojia ya Marekani.Nyumba nyingi ziliporomoka na kuwaacha mamia ya watu wakiwa bila makao.Tetemeko hilo ndilo mbaya zaidi kukumba Tanzania katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja.
Kwahiyo badala ya serikali kuendelea kuugawa mkoa wa Kagera, ni vyema ingekuja na mpango wa maendeleo katika mkoa yaani "Special Economic Rehabilitation program" ili kuchochea maendeleo zaidi katika mkoa huu unao kwamishwa na majanga zaidi licha ya wakazi wake kujitahidi kujikwamua kiuchumi.