Habari mbaya kwa watumiaji wa Tik Tok

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Tik Tok basi tambua kuwa Kuanzia sasa muziki wowote unaomilikiwa na Universal Music Group hautakuwepo kwenye orodha ya nyimbo za kutumia TikTok. Video za zamani zilizotumia nyimbo za wasanii wa Universal Music Group hazitakuwa na sauti tena.

Kwenye barua ya wazi iliyotolewa na UMG, hatua hiyo ilitakiwa kukamilika Januari 31, ambapo mkataba wa Universal na TikTok ulifika tamati.

Universal Music Group inamiliki muziki wa mastaa kama Drake, Taylor Swift, The Weeknd, Eminem, Nicki Minaj, Post Malone na wengine.

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1 ✍️
 
Huo mtandao ufutwe tu watoto wakiume waliojounga huko wamekua na mambo ya kidada
 
Back
Top Bottom