Imetokea umepata mgeni nyumbani kwako. Kama kawaida ya ukarimu kwa wageni, ukampatia Soda, Mgeni alipofungua soda, akaona ameshinda Tsh.1000,000/=. Halafu akakuonesha kwamba ameshinda, Then anaaga aondoke... Utamfanyaje?
Unakuta mgeni mwenyewe mbishi.... anang'ang'ania ya kwake peke yake
Basi hiyo kesi itaamuliwa polisi tuUnakuta mgeni mwenyewe mbishi.... anang'ang'ania ya kwake peke yake
Hio inagawanwa pasu pasu
Unakuta mgeni mwenyewe mbishi.... anang'ang'ania ya kwake peke yake
Namwachia kwani kama sio yeye nisingenunua soda
Chupa na kizibo ni vya mwenyeji. Mgeni chake soda tena ile iliyoko kwenye glass. Ebo!!
Haaaaa haaaaa haaaaaa!!! Dah! inaonesha jinsi gani unatafuta pesaWalahi hatoki na kitu mlangoni! Haki yake ni kubeba soda tena kwa tumbo aende zake. Hakuja kuchukua chupa wala kizibo. Hiyo bahati ni malipo ya Mungu kwa ukarimu wa mwenyeji. Ni cha aliyetoa hela akanunua soda. Promotion hizo huwa zinawalenga wanaotoa hela kununua soda si vinginevyo. Sasa kama yeye ni mbishi atachagua: aende na kizibo ila aache shingo!
Samahani wakuu, nimeandika hadi nimetoa povu utadhani ni kweli!