Miss Natafuta
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 26,581
- 48,735
Askofu Gwajima asema yeye ni mashine. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema yeye ni sawa na mashine ya kusaga na kukoboa ambayo ukiweka miguu unageuka sembe.
Gwajima amesema hayo leo asubuhi katika ibada inayoendelea kanisani kwake hivi sasa akieleza kuwa, "Baba wa familia amechokozwa kuwa anavuta unga watoto wamechachamaa wanataka baba ampige adui yake, nitaendelea kupiga bila kuogopa chochote."
"Watu wananiambia niache kumpiga mbona hawakumwambia yeye aache kunipiga, nitampiga tu na bado kazi inaendelea."
Anasema vita hii aliyochokozwa na hatimaye kuanzisha operation aliyoiita Operation 81..….. Yenye kauli mbiu ya Final Battle for total discipiline, itaisha huku ikiwaacha baadhi ya watu wakiwa katika hali isiyo ya kawaida