Askofu Gwajima adai kutumiwa ujumbe wa kutishiwa kuuawa

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,320
11,323
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ametishiwa kifo na kundi la watu asiowafahamu huku akidai kuwa watu waliomtumia ujumbe wa maandishi kupitia simu yake ya mkononi na kuusambaza kwa watu.

Askofu Gwajima ameyasema hayo katika ibada yake ya Jumapilii hii, amesema kuwa baada ya kuupata ujumbe huo alifanya maombi kwa ajili ya kuwafuta waliomtumia na kujua kinachoendelea.

“Kuna Askofu anajiita Nabii mdogo juzi alikuwa anasambaza meseji anasema naona Gwajima anamaliza mwendo wake,utamaliza mwendo wako mwenyewe, nimeapa kwa jina la bwana yeye anayesema nitamaliza mwendo kwa nguvu za giza atamaliza yeye kwanza na siyo mimi kwa jina Yesu na wiki ijayo ataumaliza mwendo yeye mwenyewe kwa jina bwana. Nimeapa kwa jina la baba kama yeye alivyotamani watu wamalize mwendo kwa maslahi ya mwendo wa giza na wewe umalize mwendo kwa maslahi ya ufalme wa Yesu kristo usiharibika kwa jina la Yesu kristo,” alisema Gwajima.

“Jana nilikuwa namsaka aliyetuma meseji hiyo kwenye makorido ya kiroho, nikamuona, mimi nina agano na Bwana kwamba adui zangu wakija kwa njia moja wataondoka kwa njia saba, silaha zote zitakazokuja kwangu hazitofanikiwa, yeye ndiye atakayekufa siku ile ile aliyoipanga, siyo mimi.”

Aidha Gwajima alisema kuwa yeye na waumini wake wataendelea kuwa imara kwani wanamjua wanayemwamini na hawatishiwi na vitisho vya kifo kwa sababu Mungu atawashindia.
2-GWAJIMA.jpg
 
Mchungaji mwehu huyu, anayetaka haswa kukuua huwa hasemi. Sana sana dakika unajua unakufa ndo utajua pia kumbe ulihitajika kuuwawa na baada ya hapo kweli hawakuachi, unatangulizwa kwa God.
 
Ben Saanane mlisema hivi-hivi alafu mwisho wa siku mka.....

Kweli mkuu, sasa tuna connect dot. Kila anayemsema fulani na fulani anatishiwa kisha anapotea. Sasa ni Gwajima na Ney naye katishiwa. Huku tunaambiwa aliyetaka kumfyatua Nape mpaka sasa eti hajulikani alipo.
Usalama ni mdogo sana kwa sasa na hili Mwigulu anapaswa kuwajibishwa maana analeta majibu ya kisiasa katika mambo mazito kama haya.
Mwisho watu wataanzisha vikundi vyao kama MUNGIKI kujilinda
 
Kuna nini kinaendelea tanzania wachungaji kutishiwa kuuawa wanasiasa kutolewa bastola hadharani kutishiwa kifo wasaniii nay wamitego kutishiwa kifo media kuvamiwa kuna nini jamani ole ole ole! Na hii ni ole ya mwisho kama Bwana wa majeshi aishivo hamtakufa bali hao adui wataoza wakiwa wanapumua
 
Dah nmekumbuka MUNGIKI ...
 
Ney wa mitego nay katishiwa na mchungaji naye katishwa nini kinachoendelea kwenye huu usiku wa kiza??????
 
Kuna nini kinaendelea tanzania wachungaji kutishiwa kuuawa wanasiasa kutolewa bastola hadharani kutishiwa kifo wasaniii nay wamitego kutishiwa kifo media kuvamiwa kuna nini jamani ole ole ole! Na hii ni ole ya mwisho kama Bwana wa majeshi aishivo hamtakufa bali hao adui wataoza wakiwa wanapumua
Hakuna pa usalama
amtaje tumjue huyo "nabii mdogo"
Halaf juz nay si alitoka.kwa mkulu
sasa mbona tunaunganisha dots hazikai
 
Hakuna pa usalama
amtaje tumjue huyo "nabii mdogo"
Halaf juz nay si alitoka.kwa mkulu
sasa mbona tunaunganisha dots hazikai
Mkuu hiv wauaj huwa wanatoa vitsho...? Wakawaulze waganda....naona ubuyu mpya umeanza baada ya bashite tym
 
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ametishiwa kifo na kundi la watu asiowafahamu huku akidai kuwa watu waliomtumia ujumbe wa maandishi kupitia simu yake ya mkononi na kuusambaza kwa watu.

Askofu Gwajima ameyasema hayo katika ibada yake ya Jumapilii hii, amesema kuwa baada ya kuupata ujumbe huo alifanya maombi kwa ajili ya kuwafuta waliomtumia na kujua kinachoendelea.

“Kuna Askofu anajiita Nabii mdogo juzi alikuwa anasambaza meseji anasema naona Gwajima anamaliza mwendo wake,utamaliza mwendo wako mwenyewe, nimeapa kwa jina la bwana yeye anayesema nitamaliza mwendo kwa nguvu za giza atamaliza yeye kwanza na siyo mimi kwa jina Yesu na wiki ijayo ataumaliza mwendo yeye mwenyewe kwa jina bwana. Nimeapa kwa jina la baba kama yeye alivyotamani watu wamalize mwendo kwa maslahi ya mwendo wa giza na wewe umalize mwendo kwa maslahi ya ufalme wa Yesu kristo usiharibika kwa jina la Yesu kristo,” alisema Gwajima.

“Jana nilikuwa namsaka aliyetuma meseji hiyo kwenye makorido ya kiroho, nikamuona, mimi nina agano na Bwana kwamba adui zangu wakija kwa njia moja wataondoka kwa njia saba, silaha zote zitakazokuja kwangu hazitofanikiwa, yeye ndiye atakayekufa siku ile ile aliyoipanga, siyo mimi.”

Aidha Gwajima alisema kuwa yeye na waumini wake wataendelea kuwa imara kwani wanamjua wanayemwamini na hawatishiwi na vitisho vya kifo kwa sababu Mungu atawashindia.
View attachment 490712
muongo huyo
 
Back
Top Bottom