Gwajima na siasa za Ubunge

Gwajima na siasa za Ubunge

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,494
Reaction score
33,052
GWAJIMA NA SIASA ZA UBUNGE

Mchungaji Gwajima alipotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM video zake nyingi ziliwekwa mitandaoni akizungumza mambo mbali mbali lakini mbili ndiyo zilionekana kupendwa zaidi.

Video ya kwanza kwa umaarufu ni ile anayoahidi kugeuza madrasa zote za Waislam kuwa Sunday schools.

Video ya pili ni hii ambayo anasema yeye kama mtumishi wa Mungu hawezi kutamani kushika nafasi kama ya ubunge au uwaziri.

Ile kauli yake ya kwanza ya kugeuza madrasa za Waislam kuwa Sunday Schools ukitaka kuielewa uzito wake kimantiki inabidi uigeuze iwe maneno yale kayasema sheikh kuwa anataka kubadili Sunday Schools zote makanisani ziwe madrasa.

Sasa hapo simama na utulie tuli uwaze nini kingefuatia kwa sheikh huyo.

Jaribu kufikiri kurasa za mbele za magazeti siku ya pili yangekuwaje?

Mimi naogopa hata kufikiri ingekuwaje.

Je, unaweza kufikiri Jeshi la Polisi lingesema nini na kuchukua hatua gani?

Hakuna kilichofanyika.

Magazeti yote yalikuwa kimya.
Jeshi la Polisi lilikuwa kimya.

Waislam walikuwa kimya.

Na hadi leo Waislam bado wako kimya na wataendelea kuwa kimya.

Lakini si kama kweli Waislam wako kimya.

Kuwasikia Waislam inahitaji uwe na masikio.

Waislam tumesema kwa ule ukimya wetu.
Kwani ukimya una sauti.

Ukiwa na masikio mazuri utasikia sauti ya ukimya.
Screenshot_20200721-225830.jpg
 
Huyu mtu na nabii tito utofaut ni kidogo tu, Gwajima ana miujiza ya mazingaombwe ila nabii tito hana ila matendo wote sawa tu.

Hamna alicho ongea kikatimia kila kitu lazima kiende kombo, 2015 team lowassa, 2020 team magufuri, 2025 team makonda

Samahani waumini wa Gwajima
 
Mohamed Said unakosea sana. Siyo kila Nabii, Mtume na Askofu ni Padri. Padri ni wadhifa wa kanisa katika dhehebu la Catholic na Anglican pekee. Ama umepotosha makusudi au kutokujua(siamini kama haujui).
 
Hili la matamshi ya Gwajima kuhusu kugeuza Madrasa kuwa Sunday Schools na Makanisa inabidi ulaumu utawala uliopo kwa kutomchukulia hatua na BAKWATA kwa kukaa kimya. Huu utawala unaupendeleo wa wazi ka kikabila, kikanda na kidini.
 
Ameuliza tamko hilo lingetolewa na Muislam kuzigeuza Sunday Schools zote nchini kua Madrasa ingekuaje?
Hakuna shida yoyote, hata wewe unaweza tu kutoa tamko hilo hapa
 
Back
Top Bottom