Uchaguzi 2020 Gwajima: Mbunge wa Kawe ni maarufu Mahakamani sio maarufu kwa watu wake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe, Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Josephat Gwajima amesema aliyekuwa Mbunge wa kawe sio maarufu kwa watu wa Kawe.

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha asubuhi cha mojamoja kwa moja Channel 10. Amesema Mbunge huyo ni maarufu Bungeni na mahakamani lakini hafahamiki kwa watu wa Kawe.

Jimbo la Kawe limekuwa chini ya Mbunge, Halima Mdee kwa tiketi ya CHADEMA kwa miaka kumi. Na katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, Mdee anatetea Jimbo lake kwa tiketi ya CHADEMA.
 
Gwajima hata mawakala wa kukusimamia vituoni umewakosa hizo kura utazipata wapi?

Yani mpaka wale waumini wako wamekupiga chini!

Bora uendendelee na mipasho yako tu, hiyo ndio fani yako.
 
Wewe Gwajima unajua kwanini Halima Mdee ana kesi nyingi zaidi mahakamani?

Ni kutokana na siasa za ukandamizaji wa serikali ya awamu ya 5 ya kuwabambikia makesi viongozi wa Chadema, nchi nzima

Hebu fikiria Tundu Lissu ana kesi ngapi, zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi huko Mahakamani?

Ukilipata jibu, ndiyo utajua namna gani serikali hii imekuwa ya kidhalimu, kutaka kuwaaminisha Umma wa watanzania kuwa viongozi wa Chadema, ni wavunjifu wa sheria za nchi
 
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe, Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Josephat Gwajima amesema aliyekuwa mbunge wa kawe sio maarufu kwa watu wa Kawe...
Hii ni kweli kabisa,miaka mitano alikuwa anashinda mahakamani
ADCE204C-7A3E-4153-9A62-4A19B50430ED-620x330.jpeg
 
Mzee una safari ndefu sana! Ngoja tuone mwisho kitatokea nini..lakini kama hizi ndio hoja zako na kuwaambia wajumbe "Mimi Nina hela" basi utasubiri sana maana wapiga kura wa Kawe sio wakazi wa "Kawe-Kata" wako maeneo mengine! Wape tu ulaji wakina "Black" na Pwoti Pwoti!
 
Back
Top Bottom