Askofu wa CHADEMA Josephat Gwajima. Mjumbe wa kamati kuu. Mtu mwenye nguvu ya ushawishi ndani ya CHADEMA. Mwanasiasa aliyejificha ndani ya joho la uchungaji. Kiongozi mwenye kauli kinzani, kwani wakati mmoja anamtukana Askofu Mkuu wa kanisa katoliki Tanzania Polycap Cardinal Pengo, halafu wakati mwingine anasimama kama mtetezi wake dhidi ya mpinzani wake kisiasa akimwagia sifa lukuki kwamba ni mwanzilishi wa Ukristo.
Askofu aliyejivika joho la kuwatetea mashekhe dhidi ya adui yake wa kisiasa Dr Slaa. Askofu anayepigania "ukombozi wa taifa" bila kueleza ukombozi dhidi ya nini. Askofu pekee ambaye anaweza kutoa siri za kiroho za muumini wake hadharani kwa ajili ya kulinda hadhi yake kisiasa. Askofu Josephat Gwajima