Gwajima amkana Lowassa: Apinga kuwahi kuunga mkono Mwanasiasa yeyote

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,824
WanaJF,

Wakati Lowassa akiwa zizini anachunga Ng'ombe, huku Dar wale marafiki zake wa karibu wakati wa kampeni wameanza kujitenga nae na baadhi wameenda mbali zaidi na kusema HAWAJAWAHI kumuunga mkono Lowassa!

Moja ya watu waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha Lowassa anaingia Ikulu ni Gwajima...ambae yeye alikuwa akimuunga mkono Lowassa toka akiwa ndani ya CCM na hata alivyotoka nje ya chama hicho na kutimkia CHADEMA, bado Gwajima alikuwa sambamba na Lowassa.

Lakini katika hali ya kushtua ni baada ya Gwajima kusema waziwazi kuwa yeye HAKUWAHI kumuunga mkono mtu anayeitwa Lowassa na watu wanaosema kuwa yeye (Gwajima) kuwa alikuwa upande wa Lowassa ni wapotoshaji wa mambo!

Gwajima ameeleza hayo alivyokuwa akifanya mahojiano na mtangazaji wa Azam TV na ndipo akaamua kuweka mambo sawa kwa kuwataka Watanzania waelewe kuwa HAJAWAHI kumuunga mkono mwanasiasa (personality) yeyote katika maisha yake kabla ya kuwa mchungaji na hata sasa amekuwa mchungaji.



My take,

Gwajima aache kuwa kigeugeu. Yeye na wenzake kama babu Kingunge walishasema waziwazi na Watanzania wote tukasikia kuwa mabadiliko ya kweli yataletwa na Lowassa (Hii ni wakati Gwajima na Lowassa wapo wote UKAWA). Kabla ya UKAWA, Gwajima alikuwa ana-support safari ya matumaini ndani ya CCM kwa kumuunga mkono Lowassa, tena ndani ya CCM! Leo iweje Gwajima akane maneno yake mwenyewe!?

Gwajima acha kuwa kigeugeu.
 
Last edited by a moderator:
Kama ni kweli basi hii ni hatari sana kwa mtu anayejiita mchungaji, kondoo wake wajitafsiri.
 
weka hiyo oudio au video na sisi tuiskie,maana nyie watu walumumba mara nyingi huwa mnauelewa mdogo sana.
 
Back
Top Bottom