GE2025 Gwajima amekata pumzi, anatafuta pa kushika

GE2025 Gwajima amekata pumzi, anatafuta pa kushika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kavulata isije kuwa wewe na genge lenu la akina Chiembe,Tlaltaaah na washirika wenu ndio mliokata pumzi tu?
Kelele ni za nini huko you tube, fanyeni tuone acheni vitisho. Hizo kelele za huyooo huyooo huyooo huyooo mchinjeee mchinjeee zilikuwepo tangu Nyerere hadi JPM na Sasa Samia. Kama mnaweza si mpimane nguvu na CCM kimyakimyaa? Kelele mitandaoni ni zanini? Tutawasambaratisha v
 
Unafiki kwa kwenda mbele, kama kuna mtu makini atuambie ni kosa lipi alilotenda Gwajiboy mpaka afungiwe makanisa, Let us be serious na tuache ushabiki maandazi.
Mnakera , sijui ni njaa, sijui ni ujinga. Gwaji boy amefanya kosa gani au amevunja sheria gani ya nchi,
Tuache kubwabwaja
 
Gwajima, Mpina na Polepole wote wanazo sifa zinazorandana. Wote ni wasukuma/wanyamwezi, ni waskristo na walipewa vyeo vikubwa na JPM (msukuma).

Wanachosahau ni kitu kimoja kuwa ndani ya CCM na serikali wapo wasukuma na waskristo wengine wengi sana bado. Hivyo, kama ukimkata Mpina kugombea kisesa yuko msukuma mwingine atagombea kisesa. Kama kanisa la Gwajima limefungiwa Yako makanisa mengine Yako wazi hayajafungiwa.

Akili za Gwajima ni kwamba kinachompata yeye kinawahusu wasukuma wote, waskristo wote na wanaCCM wote. Hivyo woote hawa watamuunga mkono yeye kwenye ugomvi wake na Samia.

Akili za kipuuzi kama hizí alikuwa nazo Gashagwa (mkikiyu) aliyekuwa naibu Rais wa Kenya aliyeondolewa kwa upuuzi wake wa kikabila. Rais Ruto alimteua mkikiyu mwingine kuchukua nafasi ya Gashagwa. Hivyo wakikuyu wachache tu wakamuunga mkono Gashagwa na wengi wakamuunga mkono naibu Rais mpya ambae ni mtoto wao pia.

Gwajima anahesabu idadi ya wasukama na idadi ya waskristo nchini na kudhani kuwa wooote wataungana nae kwenye ujinga wake na kusahau kuwa wapo wasukuma na waskristo wengine kama Biteko, Kasheku Msukuma na wengine wengi bado wanagombea na wako serikalini na ndani ya CCM. Eti Leo hii kanisa la katoliki na kanisa lake la uzima na ufufuo ni kitu kilekile tu. Anasahau kuwa watu wanakumbuka namna alivyomshambulia Kadinali Pengo.

Wanatapatapa, amekata punzi.
Kwamba wanatekwa Wasukuma?
 
Unafiki kwa kwenda mbele, kama kuna mtu makini atuambie ni kosa lipi alilotenda Gwajiboy mpaka afungiwe makanisa, Let us be serious na tuache ushabiki maandazi.
Mnakera , sijui ni njaa, sijui ni ujinga. Gwaji boy amefanya kosa gani au amevunja sheria gani ya nchi,
Tuache kubwabwaja
Kosa lake kubwa ni kufanya uchochezi kanisani na kuwatumia waumini kama ngao yake. Pili, Anasema mambo ambayo yeye kama mbunge na mnec wa CCM angeweza kujasema bungeni au kwenye vikao vya CCM, tatu huyu jamaa anachanganya siasa kwenye ibada.

Swali lingine?
 
Kwamba wanatekwa Wasukuma?
Ili uweze kunipa sumu mimi kavulata itakuwa rahisi kama utamtumia mwanangu judith kavulata au mtu wangu wa karibu. Unapoona mtu katekwa ni ama ni mhalifu au anasaidia uhalifu kutimia. Yaani mgoni au mshenga wake.

Wote tunajua namna Lumumba, Gadhafi, Saadam, Jerry, Karume, Neto, Masheli na wengine wengi walivyouawa. Zilikuwa nyama za wazungu kwa kuwatumia wazawa. hata nyerere alinusurika kwa njama hizi, hata mangula na JPM walinusurika kulishwa sumu kwa njia hizi za watu wa karibu. Bro unapoona mtu ametekwa au kuuawa chunguza kwanza kabla ya kutoa hitimisho juu ya nani kamteka. Tumia muda wako mwingi kutafuta kwanini ametekwa yeye na sio wewe au mkeo.

Kwahiyo msukuma anaweza kumtumia mkwere kumdhulu kavulata. Mkristo anaweza kumtumia mwislamu kumdhulu mwislamu na kinyume chake.
 
Gwajima kweli yupo katika Hali ngumu ila huyu Polepole nahisi ni kama muigizaji tu aliyetumwa na ccm wenyewe

Mtakuja kujua Baada ya uchaguzi atarudishiwa vyote alivyonyanganywa
 
Gwajima kweli yupo katika Hali ngumu ila huyu Polepole nahisi ni kama muigizaji tu aliyetumwa na ccm wenyewe

Mtakuja kujua Baada ya uchaguzi atarudishiwa vyote alivyonyanganywa
Gwajima na Polepole wako kwenye kambi moja na wanazungunza kilekile kwa lugha tofauti. Wote hawa wanae mgombea wao mmoja ambae walitaka awe Rais baada ya JPM kufariki na 2025 kupitia CCM, baada ya zoezi lao hilo kuelekea kugonga mwamba chaguo lao lingine lilikuwa kuhamishia nguvu zao zote chadema ya Lissu. Kelele zote hizi za Polepole, Gwajima, Kitimo, na yule Mchungaji Dr. Malisa ni reaction ya mazoezi yao yote 2 kukwamishwa na CCM. Yaani wamewekwa mtu kati kama nyoka aliyekatwa kichwa lakini bado anatembea kwa muda kwa kujizoazoa hadi pale atakapokata roho kaaabisa.

CCM ni mfumo(system), ni serikali ndani ya serikali, unapotaka kubishana nayo lazima ujipange sana.

Ushauri wangu hawa akina Polepole waachwe wasemeseme ili dunia ione kuwa Tanzania kuna uhuru wa maoni, ajibie tu kwasababu ni rahisa sana kumjibu Polepole na Gwajima bila kutumia nguvu nyingi. Urahisi huu unatokana na Polepole na Gwajima wote kuwa viongozi wakati wa magufuli waliomshauri Rais vibaya kwenye mambo mengi kama vile kuengua wagombea wote wa vyama vya upinzani, kuhusu covid-19 na chanjo ya covid-19, kufuta shughuli za vyama vya siasa na utekaji wa watu kama mo dewji na mauaji ya raia pamoja na Lissu kupigwa risasi. Mambo yote haya yanajulikana ndani na nje ya nchi, ndiyo maana kelele zake hazileti mwangwi wowote. hata kujiuzulu ubalozi wa Cuba alionekana kama chizi tu duniani kote.
 
Gwajima kweli yupo katika Hali ngumu ila huyu Polepole nahisi ni kama muigizaji tu aliyetumwa na ccm wenyewe

Mtakuja kujua Baada ya uchaguzi atarudishiwa vyote alivyonyanganywa
Kete ya mwisho ya Polepole ni kuweka hadhari eti walivyomuibia JPM kura hadi akashinda uchaguzi, anajidhalilisha. Sijui kama Samia atazihitaji mbinu za kishenzi kama hizo kuiba kura.
 
Back
Top Bottom