Gwajima Akifa, jeshi la Polisi linaweza ingia matatani

Gwajima Akifa, jeshi la Polisi linaweza ingia matatani

Sakata la Gwajima na Pengo na kile kinachoendelea kwa Gwajima na watu wake kumenifanya niwe upande wa Gwajima kuliko !
 
Kufa ni faida na sitarajii kama ask.Gwajima anaogopa kufa kama viongozi wa dini wanafiki wanapenda kula futari za bure.
 
Kesi ni kumtukana Pengo ambaye hajashitaki na alishasemehe hii ya passport cheque,tablet yanatoka wapi tena?????Kuna mkono wa CCM Hapo.
hapa Ndio washabik wa mzinzi na tapeli gwajima wanapo shindwa kufafanua.

POLISI WAMEPATA WAPI PASPORT NA BASTOLA VILIVYO SAJILIWA KWA JINA LA GWAJIMA????

HIYO CHEQUE BOOK NA TABLETS ZA GWAJIMA WAMEZIPATA WAPI?????

MBONA ALIPOANZA KUHOJIWA JUU YA UHALALI WA MALI ZAKE ALIZIMIA????


KAMA YOOTE ANASINGIZIWA, HUKO KUMKASHIFU PENGO NAKO WANAMSINGIZIA???


JIBUNI HAYO MASWALI IKIWA NYINYI NI WAKWELI.
 
Wewe nimeamini ni nabii wa uongo kabisa.
Gwajima akipona atadai ana ujumbe mzito kutoka Kuzimu . Atakua akijisifu yeye ni nabii pekee aliyekufa akafufuka baada ya YESU... Tuwe makini wakristo tusiupokee huu uongo kamwe, kwa mtu aliyemdhihaki mtu tunayemuheshimu.
 
Ni jambo la kawaida kuona watumishi wa Mungu wanafia mikononi mwa Vyombo vya dola? Sasa gwajima akifa italeta uamsho mpya,
 
Sio jambo la kuombea ili litoke,lakini endapo ikitokea Askofu Gwajima akaiaga dunia ghafla,jeshi la polisi litakuwa kwenye wakati mgumu kutoa ufafanuzi juu ya kifo chake.
Siamini kama polisi walimdhuru gwajima ila kwa imani ndogo iliyopo kwa wananchi juu ya jeshi hili usishangae waumini wa gwajima wakahusisha kifo hicho na jeshi letu.
Mungu akujalie upone mapema askofu Gwajima na akuepushe na umauti urudi kuhudumu kwenye madhabau ya mungu,Na amani ya nchi yetu iendelee kudumu.



Mimi natamani afe Flora mbasha apunguze kiburi! Ivi inaingia akilini mtu anaropoka ovyo afu unahojiwa tu una faint?? Angepelekwa Segerea uyu si tungekua tushamsahau na angekata gogo apo apo
 
Napata wasiwasi na utumishi wake. Maneno ya kuudhi na yaliyokosa staha hayakutarajiwa kutoka katika kinywa cha mtumishi wa Mungu kama anavyojiita kuwa yeye ni Askofu japo sina uhakika na uhalali wa uaskofu wake.Pengo alitumia busara kutoa maoni yake na yeye alipaswa kutumia busara kutoa maoni yake ila nguvu kubwa aliyoitumia imeuonesha upumbavu wake dhahiri.
 
Tangu lini Jeshi la Polisi huwa linaingia matatani kwa vifo vya raia wasio na hatia, wakiwa wao ndiyo watuhumiwa wakuu?

Tuliona jinsi Mwandishi Daudi Mwangosi alivyouawa kule Mufindi kwa 'maelekezo' ya aliyekuwa RPC wa mkoa wa Iringa, Kamuhanda, badala ya RPC huyo kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo za mauaji, ndiyo kwanza JK aliamua kumpandisha cheo kutokana na utumishi wake uliotukuka!
 
nadhani police walitumia uweledi wao wa hali ya juu sana ijapo siku nyingne hutumia matope, in actual sense hao hawakua wahudumu kwa nia ya kumhudumia mgonjwa bali walitaka kumtorosha mgonjwa askof Gwajima ambayo inanipa mashaka ni kwanini alitaka kutoroka? its a question that you can brainstorm this morning and come to a better opinion.
 
kwa nn watu mnakimbilia kusema kuwa polisi walitaka kumuua,wakamuwekea sumu?

auliwe kwani yeye ana hatari gani kwa tanzania?

mbona sio tishio hata kidogo,kuna watu ambao ukisema serikali au polisi inataka kuwaua unaweza kujenga hoja lakini sio gwajima.

na pia kama wangetaka kumuua wasinge tumia mbinu mbovu ya sumu kwenye mic.

kagame amekua anawaua watu wote ambao kwanjia moja au nyingine wametishia kuuporomosha utawala wake,sasa gwajima auliwe na polisi ana hatari gani kwa taifa?

waumini wake na wafuasi wake ni sehem gani ya taifa?ni wachache sana,ni kama tone tu.

kwa nn serikali imuue,yy anajulikana kua anaongea vitu kwa pupa, aliongea kuhusu dengue,kitu ambacho ni cha kitaalam yy akakiongelea kwa kijinga.

hii kusema kuwa kawekewa sumu ni kutafuta pa kutokea tu

labda yy kapata mshtuko tu,hakutegemea kua alivyokua anaongea vile kwa kujisifu na kutaka umaarufu na kushanguliwa vinge mgeuka.

mishtuko kama hii inawakuta wengi,sio yeye wa kwanza.na yy ni binadamu tu kama wengine,na pia inasemekana kua hakula chakula kwa mda mrefu.vyote vinawwzekana.

lakini kutaka kuuliwa NO

Ni vyema ukazingatia sheria mpya ya kutubana! Hapa unaweza ukabanwa kwamba umeandika habari tata- yaani unamtuhumu Kagame KUUA, unaweza ukapata shida maana ukitakiwa ushahidi sio rahisi kuupata. Aliyeleta mada yeye katoa tahadhari kutoka kwenye fikra zake, hajatuhumu. NI WAJIBU WETU KUJIKUMBUSHA KUHUSU HII SHERIA MPYA ILIYOPITISHWA NA BUNGE LETU PENDWA!
 
Kesi ni kumtukana Pengo ambaye hajashitaki na alishasemehe hii ya passport cheque,tablet yanatoka wapi tena?????Kuna mkono wa CCM Hapo.

Mfano imetokea mtafaruku baina yangu na ndugu yako, katika purukushani kwa bahati mbaya sana akapoteza maisha, lakini kwa kuwa wewe ndugu huna kinyongo ukaamua kutangaza umenisamehe, je! Serikali itaniacha huru kwa sababu muhusika umesamehe?
 
Back
Top Bottom