Gunman kills 26 at Elementary School in Connecticut

Gunman kills 26 at Elementary School in Connecticut

Vitendo vya watu wenye silaha (bunduki, visu na silaha nyingine) kuwaua Wamarekani wenzao vinaweza kuongezeka kama sera ya ubepari mkali inayoendeshwa Marekani haitabadilishwa. Mazingira wanayoishi wamerekani yanawachanganya (provocative) hata Wamarekani wenyewe. hii inaweza kuwa chanzo cha watu kuchanganyikiwa na kujikuta mtu akitafuta namna ya kuondokana na maisha yale. Kufanyakazi kwa muda mrefu kwa siku, upweke, kukaa sehemu moja ya Amerika kwa muda mrefu, ukosefu wa kazi, fulsa za elimu na matibabu ni vichocheo muhimu katika kuchanganyikiwa.
Vita inazopigana Marekani dunia nzima ama zinapoteza, kuacha majeraha ama kuwaweka askali na watumishi wengine mbali na ndugu na jamaa zao, hivyo familia zinaachwa zikiwa bila ya ndugu na jamaa zao muhimu sana kijamii. Wenye nafuu Marekani ni wale wenye uwezo wa kutoka nje ya marekani na kurudi angalau kila baada ya miaka 3-5 hivi. Wako wamarekani wengi ambao hawajui kama kuna maisha mengine zaidi ya Marekani, maana wao wanangalia TV, movies, CD, michezo, n.k za Kimarekani tu. Ukiwaangalia vijana wa Kimarekani utagundua kuwa wana dalili zote za kuchanganyikiwa kama vile kuvaa chupi tu na kuingia darasani ama kutembea barabarani, kuvaa nguo zilizotoboka, kuvaa viatu tofauti miguuni ama kuvaa viatu vya upande mmoja (kushoto ama kulia), kunywa pombe kupita kiasi na kutumia madawa ya kulevya hata kwa wenyewe umri mdogo, vitendo vya ushoga, n.k.

Watu wenye maisha kama haya ukiwaruhusi wamiliki silaha utategemea nini?


Umeishi Marekani au unaiona kwnye sinema zaidi na hizo music videos??? halfu vitendo vingi unavyo visema hapa Tanzania ndio vinara, Ushoga uko uswahili kama vila hakuna cha ajabu.
 
52b1254b6e5aef24240f6a7067003393.jpg

A variety of military-style semiautomatic rifles obtained during a buy back program

are displayed at Los Angeles police headquarters on Thursday, Dec. 27,2012.

2012-12-29T120534Z_1_CBRE8BS0XLD00_RTROPTP_2_USA.JPG

A small portion of guns that were turned in by their owners are stacked inside a truck
at a gun buyback held by the Los Angeles Police Department in Los Angeles, California, December 26, 2012


Nchi ya Marekani licha ya kuwa na serikali ya Federal, kila state ina serikali yake na bunge lake lenye kuamua wanayotaka kila state bila kuingiliwa na Federal kama ilivyo Zanzibari ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zoezi la kusitisha uhuru wa umilikaji silawa unakuwa mgumu kitaifa kutokana na utaratibu wa kila state kuamuliwa na congress yake, na pengine baadhi ya state ambazo hazijapata matatizo kama hayo kutoona umuhimu wa kutazama upya sheria ya umilikaji silaha nchini humo.

Jiji la New York ambalo lipo ndani ya New York State limeanza kuratibu orodha ya wamiliki wa silaha nyumba kwa nyumba kwa kuanzia na counties kama tatu hivi zilizo kaskazini mwa Hudson River karibu na jiji la NY, orodha ambayo ilimwagwa kwenye gazeti maarufu la
The Journal News, a Gannett Co. handgun permits. Pamoja na kulalamikiwa na wamiliki hao, jambo hilo laonekana kuanza kupata nguvu zaidi.

Jiji la Los Angeles watu kadhaa wameamua kusalimisha silaha zao kali za semi-automatic handgun ambazo hutumiwa na majeshi ya ulinzi ikiwa ni mwitiko wao wa kulinda amani ya raia inayoonekana kutoweka sababu ya umilikaji wa silaha hizo nzito kiholela. Silaha hizo zinarudishwa serikalini kwa utaratibu wa serikali kuzinunua toka kwa wamiliki, maana yake kurudishiwa pesa zao walizotumia kuzinunua.

10f43db387ac0524250f6a706700333f.jpg

In this Thursday, July 26, 2012 file photo, an AR-15 style rifle is displayed at the Firing-Line indoor range and gun shop in Aurora, Colo.

Matatizo ya umilikaji silaha kuna mengi yanayochangia, lakini pia uthibiti wake ni mdogo kwa vile kila mwenye akili timamu ana haki ya kuhodhi silaha hata kama hana umuhimu nayo kwa hoja tu ya kujilinda binafsi.

Maduka ya silaha kama inavyoonekana pichani humsaidia mteja kumpa maelekezo na namna ya kupata silaha bila matatizo na kisha kumfanyiza mazoezi ya kuitumia na kulenga shabaha.

Tatizo sasa ni jitihada za kupunguza umilikaji wa silaha papo wanasiasa wakishinikiza umuhimu wa raia kumiliki kwa sababu za kujilinda usalama wao. Mpaka nchi nzima wakubaliane wakati kila State ina nguvu ya kutunga na kutumia sheria zake kazi kwelikweli.
 
Ukimsikiliza huyu Morris, utaona huo ulikuwa ni mpango wa zamani ambao ulikuwa unatafutiwa "tukio" ili utekelezwe.

Na hii
 
Last edited by a moderator:


Mambo ya siasa yakiendekezwa matokeo ndo haya. Rahisi sana kubomoa lakini kujenga tena ipo kazi ya ziada. Tatizo hapa si silaha tu, kuna tatizo lingine ambalo linawafanya wengi wawe vichaa ambalo ni malezi ovyo, kudekeza watoto kama mayai vile bila kukemewa, matumizi ya madawa, serikali kuwafunga magerezani wazazi wanaowatiisha watoto wao. Kuna mengi tu basi kazi bado mbichi.
 
Last edited by a moderator:
Acheni dhabi ya ubaguzi iwatafune, wamewatesa sana wana wa mataifa mengine like Japani, Iraq, Libya etc... kwa silaha zizo hizo ..! Na mimi nasema dhabi hiyo inastahili iwatafune. Now they will have time to deal with their own problems, siyo kila siku Iran Iran..!
 
Mji wa Newton hapa Marekani unaanza kazi ngumu ya mazishi ya watoto 20 na watu wazima 6 waliouwawa katika mashambulizi ya bunduki kwenye shule ya msingi ya Sandy Hook huko katika jimbo la Connecticut.

Mazishi ya watoto wawili wa miaka 6 yatafanyika Jumatatu ya kwanza kwa wale waliopigwa risasi katika shule ya msingi ya Sandy Hook katika mji wa New town Connecticut. Watoto waliouwawa ijumaa walikuwa kati ya miaka 6 na 7.

Afisa wa Polisi alisema kwamba shule hiyo bado ni eneo la uhalifu na wapelelezi bado wanafanya kazi saa 24 kwa ajili ya kesi hiyo. Amesema watu wazima wawili walipigwa risasi lakini walinusurika kifo.

Rais Obama aliungana na waombolezaji huko New town Jumapili usiku , akiwaambia wale waliokusanyika kwenye ibada kuwa hawako peke yao kwenye kuomboleza na taifa limeachwa na maswali magumu.


Source: Voice of America
 
Mji wa Newton hapa Marekani unaanza kazi ngumu ya mazishi ya watoto 20 na watu wazima 6 waliouwawa katika mashambulizi ya bunduki kwenye shule ya msingi ya Sandy Hook huko katika jimbo la Connecticut.

Mazishi ya watoto wawili wa miaka 6 yatafanyika Jumatatu ya kwanza kwa wale waliopigwa risasi katika shule ya msingi ya Sandy Hook katika mji wa New town Connecticut. Watoto waliouwawa ijumaa walikuwa kati ya miaka 6 na 7.

Afisa wa Polisi alisema kwamba shule hiyo bado ni eneo la uhalifu na wapelelezi bado wanafanya kazi saa 24 kwa ajili ya kesi hiyo. Amesema watu wazima wawili walipigwa risasi lakini walinusurika kifo.

Rais Obama aliungana na waombolezaji huko New town Jumapili usiku , akiwaambia wale waliokusanyika kwenye ibada kuwa hawako peke yao kwenye kuomboleza na taifa limeachwa na maswali magumu.


Source: Voice of America





 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom