Gunman kills 26 at Elementary School in Connecticut

Gunman kills 26 at Elementary School in Connecticut

ht_Adam_lanza_sandy_hook_bug_121214_wmain.jpg

Kijana aliyefanya maangamizi haya huyu hapa, ni mdogo sana.

Tatizo la Marekani umilikaji wa silaha za moto ni kama vijana wa vijijini wanavyoshindana kuwa na manati ya kuulia ndege. Maduka ya silaha yako kila sehemu kama maduka ya nguo vile na sehemu za uswahilini. Hakuna cha pingamizi la pekee la umilikaji silaha Marekani isipokuwa kama mtu amethibitishwa na daktari kuwa na matatizo ya kiakili. Mara kadhaa nilipokuwa naongea na polisi walinishauri niende nikanunue silaha ya kujilinda, lakini dhamiri yangu ilikataa kwani sihitaji kitu hicho na pengine huweza kunifanya nisiishi kwa amani na nikawa windo la wanaotafuta silaha za maangamizi ambao wana bad credit kupata kwa halali.

Movie nazo huchangia, maana watoto wanaangalia hizo na kufanyia mazoezi, na wawapo katika magenge yao ya kuvuta weed, ikikolea majadiliano huwa ni maangamizi. Wanaangalia movie za kijasusi na hapo hujifunza namna ya kufanya, na hapo uzoefu wa matumizi ya unga huwaharibu akili zao na siku unga ukikolea na kitu kidogo kikimwuzi basi mbinu alizoona kwenye movie za akina Swazilneger zitatumika na kuishia kujimaliza mwenyewe, hapo yanabaki maombolezo na kesi imefungwa kwa vile mwuaji amejihukumu kwa kujiruhusu kutangulia mbele ya Mwenye haki.

Taifa la marekani katika utafiti uliofanywa kama miaka 7 iliyopita ni kwamba robo ya wamarekani ni waathirika wa madawa ya kulevyo. Sijawahi kuziona dawa za kulevya kwa macho yangu Tanzania, lakini nilipotia mguu tu Marekani, hoteli niliyofikia nikashtuliwa na mmoja ambaye aliungana nami kwenye elevator ambaye aliniuliza kama nahitaji, nikamjibu nini? Akanionyesha kipakiti fulani kina unga mweupe, nikamwuliza nini? Kaniambia ni Cocaine. Kwa vile nilishafikia flower nilikokuwa naenda basi niliishia kuachana na maongezi yale kwani kwangu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Kesho yake nikaamua kunza kutafuta nyumba baada ya kumweleza kisa hicho dean of studies. Akanishauri hama mara moja hapo si mahala panapokufaa na ni hatari. Nashukuru after a week nikapata nyumba sehemu iliyotulia hadi nilipoondoka kurudi zangu bongo.

Madawa ya kulevya Marekani huunzwa mitaani kama machinga bongo wafanyavyo kutembeza karanga vile. Bangi hata nashangaa wanaipata wapi. Kazini walifukuzwa vijana kadhaa kwa matumizi ya bangi wakiwa kazini.

Marekani siku hizi sharti la kwanza katika ajira ni kwenda hospitalini kwa wataalamu kupimwa uhakiki kama una matumizi ya madawa ya kulevya, vinginevyo ukipatikana hakuna ajira. Uzuri wa Marekani daktari anachukua vipimo na wenye kufanya uchunguzi ni kampuni nyingine ya maabara ambao hawamjui ni nani kwani wanapata maelfu ya order. Uchunguzi licha ya kupelekwa kwa mwajiri bila hungia kwenye record ya mhusika serikalini.
 
Tunatoa pole kwa msiba huo,na mungu azipokee roho za marehem

obama kwa tukia lake lile la jana kwenye press conference la kumwaga chozi lisiishie tuh kwa watoto wa kiamerica,,lazima atambue kwa jins alivoumizwa yeye ndivo wazazi wa watoto wasiokua na hatia iraq.afhganstan,libya na sehemu zingne wanaumia hivo hivo,
mkuki ni mchungu kote kote..
 
...Kama umechoka kuishi si ujimalize mwenyewe tu inahusu nini kwenda kuwaua watoto wadogo chungu nzima na kuwaachia wazazi wao, ndugu na jamaa majonzi makubwa na ya muda mrefu? Halafu bunduki aliyotumia/alizotumia huyu kichaa zilikuwa ni za mama yake ambaye naye kauwawa na huyu lunatic.
Ndiyo madhara ya kuruhusu bangi haya, yaani wamarekani wanavuta bangi hadharani tu na polisi wanapita mitaa hiyo hiyo wala hawafanyi kitu. Yaani kuwa marekani ni kuwa kwenye risk kubwa sana. Hasa wale wamarekani weusi ni kero tupu humo mitaani. Wanaboa kweli wanapovamia kila mtu ili awape dola moja ya kuvutia bangi. Kati ya nchi ambazo huwa naona ustaarabu wao una utata, Marekani ni mojawapo.
 
itakuwaje lini? Kwa sasa hivi na miaka yote ya nyumba hakuna vitu kama hivyo kwenye "nchi zetu hizi." Marekani ndio kuna utamaduni wa bunduki, usilinganishe maembe na machungwa, Tanzania hakuna kitu hicho!

Na huyo Obama unaemzungumzia nadhani antics zake zinaweza kuwa ndio mara ya kwanza kutokea katika historia, kwa kujiliza hadharani. Kwenye matatizo tunategemea kiongozi wa "dunia huru" akija hadharani atoe masuluhusho, sio machozi!
Hilo la obama kulia hadharani hata mimi niliona ni la kisiasa zaidi na halikuwa na mantiki kabisa. Ni upuuzi kwa kiongozi wa nchi kutoa machozi mbele za watu wanaokutegemea kwamba wewe ndiyo baba, utasimama imara na kutoa suluhisho la matatizo yanayoikabili nchi yako.
Lakini kuhusu Tanzania, ni kweli haijawahi kutokea, but ni rahisi zaidi kwetu kutokea. Sema tu bahati tuliyonayo ni kwamba hatuna mateja wengi humu nchini ukilinganisha na marekani. Ile nchi ni kama ya wendawazimu. Yaani ukiwa marekani, usalama wako ni mdogo kuliko ukiwa Tanzania. Maana Tanzania utakabiliana na vibaka tu, lakini marekani unakutana na mtu anataka kukuuzia bastola, au anakuomba dola moja ya kununulia bangi huku ameshika bastola, yaani ni shida tupu.
Hata hiyo utulivu tulionao hautoshi kutuhakikishia kwamba tupo salama refer wenzetu wa Uganda walioteketea zaidi ya 30 kwa bomu. So inawezekana huku kwetu isiwe ni kwa bunduki lakini ikawa ni mabomu kama ambavyo imetokea Uganda na Kenya. Ni vema kuchukua tahadhari wakati wote.
 
hii yote ni matokeo ya kukosa miongozo ya imani watu wanafikiria democracy ndo kila kitu... sote tutambue democracy bila kuwa na miongozo ya imani si chochote! Watakuja kurealize wakati tayari wameathirika vyakutosha na turning back haitokuwa rahisi kihivyo. Am sad for the situation and victims
 
Jana OBAMA alitoa fake tears sasa swali la kujiuliza haohao Wamarekani wanawapa silaha waasi wakiwemo Alqeeda na wanawaua kila raia wakiwemo watoto uko SYRIA bila kujari...Sasa mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu ...Nadhani hii liwe fundisho kwa kutokugawa silaha za moto au kuuza km PED
 
Hilo la obama kulia hadharani hata mimi niliona ni la kisiasa zaidi na halikuwa na mantiki kabisa. Ni upuuzi kwa kiongozi wa nchi kutoa machozi mbele za watu wanaokutegemea kwamba wewe ndiyo baba, utasimama imara na kutoa suluhisho la matatizo yanayoikabili nchi yako.
Lakini kuhusu Tanzania, ni kweli haijawahi kutokea, but ni rahisi zaidi kwetu kutokea. Sema tu bahati tuliyonayo ni kwamba hatuna mateja wengi humu nchini ukilinganisha na marekani. Ile nchi ni kama ya wendawazimu. Yaani ukiwa marekani, usalama wako ni mdogo kuliko ukiwa Tanzania. Maana Tanzania utakabiliana na vibaka tu, lakini marekani unakutana na mtu anataka kukuuzia bastola, au anakuomba dola moja ya kununulia bangi huku ameshika bastola, yaani ni shida tupu.
Hata hiyo utulivu tulionao hautoshi kutuhakikishia kwamba tupo salama refer wenzetu wa Uganda walioteketea zaidi ya 30 kwa bomu. So inawezekana huku kwetu isiwe ni kwa bunduki lakini ikawa ni mabomu kama ambavyo imetokea Uganda na Kenya. Ni vema kuchukua tahadhari wakati wote.

Lukolo Obama ni mwanadamu kama wewe, mara ngapi raia wa Marekani wameuwawa hajalia? Juzi balozi kauwawa huko Libya sikumbuki kumuona akilia. Kuwamaliza malaika kama wale bila sababu ni kitendo cha kinyama sana so binafsi simlaumu kwa kulia, I'm sure aliimagine kama yeye ni mmoja wa wazazi wa watoto waliopotezewa maisha. Na isitoshe kitendo cha kulia hadharani sidhani kama kinamaanisha kwamba hatua hazitachukuliwa, unaweza usilie na hatua usichukue pia. Na unaweza ukamwaga chozi na bado ukaplay part yako kama Commander in Chief.
 
Ninakubali kabisa mkuu. Ila nafikiri ukiwa kama baba, likitokea tatizo nyumbani kwako, watoto wakawa wanakuangalia wewe kama mbabe wa matatizo, kwa bahati mbaya wakakuona na wewe unalia nafikiri watakata tamaa kabisa. Kwa ajili tu ya kuonyesha ubaba wake, alitakiwa angalau aongee katika hali ya kuonyesha masikitiko na atoe way forward kwa ajili ya longterm solution. Matukio ya aina hii si mageni kabisa huko marekani, miaka miwili tu wanachuo waliuawa kwa style hiihii. kwahiyo ni suala la kuamua kwamba anafanya nini kahakikisha huu uhuni hautokei tena na si kutoa machozi kutafuta huruma za watu waliopoteza watoto wao. Katika hali ya kawaida, ni jukumu la serikali ya nchi kuhakikisha usalama wa kila raia ndani ya nchi. Kwa kushindwa kwake kuhakikisha usalama wa wale watoto anatakiwa ajiuzuru na si kulia.
 
Bado ana sura ya kitoto kabisa. Ndiyo madhara ya kugawa silaha kama karanga ukichanganya na action movies na computer games za mauaji.
 
Right wing nuts hawakubali,wanasema guns dont kill people,people do kill people.

Lakini ukweli ni kwamba people kill people with guns.Na hivyo madhara ya kutumia assault riffles ni makubwa zaidi.

Ila tatizo lilipofikia sijui kama wata lisolve vipi,guns ni kama culture ya wamarekani.Na ukishakuwa nayo(most of them have),hutopenda mtu akunyang'anye.

Hahaaa JMushi...sio wananchi tu hata Polisi Marekani wana hobby za GUN kila siku wanaua bila ya kibali tena cha kusikitisha zaidi wanaua weusi tu husikii weupe wameuliwa na polisi ni nadra sana.Juzi wamemuua kijana mweusi ktk nyumba yao akiwa hana hata silaha mkononi wamempiga risasi 11 sasa what goes round it will always comes around.
 
inasikisha sana kuua watu wasio na hatia. kuna binadamu wakatili sana duniani!!
 
ukichaa haijapita hata wiki,juzi tu kulikuwa na tukio la hivyo hivyo hapo USA.?

Oooops kwakuwa ni mweupe inabidi wampendelee watasema mengi mara ooh stress oohh alikuwa na matatizo ya kisaikolojia, sasa hapo angekuwa mweusi basi angelikuwa "gang star" na angekuwa ni muisilamu angeitwa"gaidi"Unajua hii hali inasikitisha sana huko tunakoelekea.Wanasema what goes aound comes aound juzi kauliwa kijana mweusi na Polisi kwa risasi 11 na hakuwa na silaha mkononi na yupo nyumbani kwao na hiyo ni kesi mojawapo za kesi zinazo wakabili polisi kwa kuua weusi na idadi inazidi kuongezeka kila mwaka.
 
Bado ana sura ya kitoto kabisa. Ndiyo madhara ya kugawa silaha kama karanga ukichanganya na action movies na computer games za mauaji.

Silaha zinatakiwa zihifadhiwe mahali salama ambapo si kila mtu anaweza kuzifikia.

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
Back
Top Bottom