Guinea-Bissau's President Assassinated | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Guinea-Bissau's President Assassinated

Discussion in 'International Forum' started by Mfumwa, Mar 2, 2009.

 1. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Guinea-Bissau president 'is dead'

  Renegade soldiers have shot dead the president of Guinea-Bissau, Joao Bernardo Vieira, reports say.

  Officials and residents gave news of the death just hours after that of the army chief of staff, Mr Vieira's rival.

  Gunfire is said to be resounding around the capital, Bissau, and it is unclear who is in control of the West African nation.

  Bissau is one of the world's poorest states. It has a history of coups and is a drug trafficking centre.


  Source: BBC NEWS | Africa | Guinea-Bissau president 'is dead'
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Haya mambo ya kupigana na kuuana tena ktk Africa yaani inakera!

  Halafu haya mapinduzi ni kwa nini ni zaidi West Afrika?

  Angalia Mauritania, Guinea na sasa Guinea Bisau!

  Afrika tutafika kweli?
   
 3. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni mfumo wa kisiasa unaompa kiongozi mkuu wa nchi mamlaka yasiyo na kikomo hadi raia wanamchoka.Ingwa siungi mkono hatua ya kumpiga risasi ni wazi kuwa wanajeshi na raia ndani ya nchi yake walikuwa wamemchoka yeye na sera zake.
   
 4. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Je sio wenye uchu wa madaraka wameamua kuchukua fursa ya udhaifu wa kiulinzi ndio wakamuua Presidentee?
  ICADON mkuu wa usalama waweza kutubandikia picha za hili tukia kule kwenye thread yetu kama zinapatikana?
   
 5. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #5
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Renegade soldiers kill Guinea-Bissau president


  By ASSIMO BALDE,
  Associated Press Writer

  [​IMG]

  Guinea Bissau's President Joao Bernardo 'Nino' Vieira talks to the media during a press conference at the EU Commission headquarters in Brussels.


  BISSAU, Guinea-Bissau – Renegade soldiers assassinated the president of Guinea-Bissau in his palace Monday, hours after a bomb blast killed his rival, but the military said that no coup was in progress in the fragile West African nation.

  The military statement broadcast on state radio attributed President Joao Bernardo Vieira's death to an "isolated" group of unidentified soldiers whom the military said it was now hunting down.

  Luis Sanca, security adviser to Prime Minister Carlos Gomes Jr., confirmed the president had died but gave no details.

  The military said the armed forces would respect the constitutional order, which calls for parliament chief Raimundo Pereira to succeed the president in the event of his death.

  It also dismissed claims that the armed forces headquarters was implicated in Vieira's killing as a retaliation for the assassination late Sunday of armed forces chief of staff Gen. Batiste Tagme na Waie at his headquarters in Bissau.

  Source: Renegade soldiers kill Guinea-Bissau president
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  1. Mimi naona ktk Afrika kuna nchi zingine zisingepata uhuru..zingekuwa chini ya mkoloni hadi leo.. kama Guinea, Gunea Bissau.

  2. sasa uhuru ulitafutwa wa nini? Wakati tunauwana wenyewe kwa wenyewe?

  Tuwaombe Purtugal/Ureno warudi waitawale tena Guinea Bissau hadi hapo watakapokuwa tayari kujitawala hata ikiwa baada ya 20 years!
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  So bad,, dunia ya sasa hivi bado watu wanauana tu!
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Mar 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Miafrika in action....
   
 9. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  natanzania yako je? hatuuani wenyewe kwa wenyewe through the looting of money for health, education, quality of life etc..afadhali waosio wa nafki hiding behind the so called democracy!! wacha wabaya wanaojuane wamalizane tuu kuliko kudanganyana kama nchi zingine za kiafirka Tanzania included!!
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  MIMI naunga mkono mapinduzi ambayo wananchi wamechoshwa na sera,ubakaji wa demokrasia,katiba ya nchi nk.

  Utawala ambao hauthamini raia wake,naam !Utawala usio wa 'WATU'.Utawala ambao hata kama uchaguzi ukifanywa,mbinu chafu na udanganyifu ndiyo nyenzo kuu ya ushindi.Africans we must get rid of all these thugs.

  Kama Demokrasia ndiyo ustaarabu wa mamlaka,kama tulidai uhuru ili tutawale kwa kura,na kama uchaguzi huru na wa haki haupewi kipaumbele,basi yeyote ambaye ni kikwazo cha hayo yote aondolewe kwa njia yoyote.Naunga mkono mapinduzi ya aina hii and i'm not ashamed to support this.

  Mungu Ibariki Africa! Ipo siku tutainuka juu ya paa la ulimwengu.
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ombi: Mods,naomba hii muiache hapa.
  Hata hivyo zingatieni utaratibu


  Kuna habari Rais wa Guinea Bissau amepigwa Risasi.Je sisi tunazo sababu za kuwalaumu wananchi wa Guinea Bissau,au askari waliofanya kitendo hicho?

  Je,tunazo sababu za kuwalaumu wananchi wanaochukua hatua hizo kwa kisingizio cha kusizitiza utawala wa sheria,au kumpindua mtu kwa sanduku la kura au kwa njia nyingine zozote za kidemokrasia?


  Ikiwa kiongozi mkuu wa nchi,anaongoza kwa manufaa yake bila kujali wananchi wake,bila kuzingatia sheria,demokrasia ya kweli iambatanayo na tume huru ya uchaguzi? Nadhani mara nyingi huwa tunakosea kutamka neno Demokrasia katika msitu wenye wanyama wakali ,wairaruayo demokrasia kwa maslahi binafsi.Huwezi kupiga kura katika mazingira magumu yasiyo na tume huru za uchaguzi.

  Kisingizio cha kutotambua mapinduzi ya kijeshi kinawapa uhuru mijitu isiyojali maslahi ya taifa kujinyakulia mamlaka kibinafsi hata bada ya kushindwa uchaguzi.Je tuendelee kulaani mapinduzi ya aina hii? Mapinduzi yaletwayo na watu baada ya kuona utawala wa kiimla hauna dalili ya kulegeza msimamo wa kuwa madarakani na sera mbovu zisizokidhi hitaji la waafrika kupigania uhuru toka kwa wakoloni?

  Je,Mapinduzi ya Mauritania,Guinea,na sasa Guinea Bissau yanatufundisha nini?

  Naombeni maoni kwa hili wakuu.
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ombi: Mods,naomba hii muiache hapa.
  Hata hivyo zingatieni utaratibu


  Kuna habari Rais wa Guinea Bissau amepigwa Risasi.Je sisi tunazo sababu za kuwalaumu wananchi wa Guinea Bissau,au askari waliofanya kitendo hicho?

  Je,tunazo sababu za kuwalaumu wananchi wanaochukua hatua hizo kwa kisingizio cha kusizitiza utawala wa sheria,au kumpindua mtu kwa sanduku la kura au kwa njia nyingine zozote za kidemokrasia?


  Ikiwa kiongozi mkuu wa nchi,anaongoza kwa manufaa yake bila kujali wananchi wake,bila kuzingatia sheria,demokrasia ya kweli iambatanayo na tume huru ya uchaguzi? Nadhani mara nyingi huwa tunakosea kutamka neno Demokrasia katika msitu wenye wanyama wakali ,wairaruayo demokrasia kwa maslahi binafsi.Huwezi kupiga kura katika mazingira magumu yasiyo na tume huru za uchaguzi.

  Kisingizio cha kutotambua mapinduzi ya kijeshi kinawapa uhuru mijitu isiyojali maslahi ya taifa kujinyakulia mamlaka kibinafsi hata bada ya kushindwa uchaguzi.Je tuendelee kulaani mapinduzi ya aina hii? Mapinduzi yaletwayo na watu baada ya kuona utawala wa kiimla hauna dalili ya kulegeza msimamo wa kuwa madarakani na sera mbovu zisizokidhi hitaji la waafrika kupigania uhuru toka kwa wakoloni?

  Je,Mapinduzi ya Mauritania,Guinea,na sasa Guinea Bissau yanatufundisha nini?

  Naombeni maoni kwa hili wakuu.
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Askari waasi wamemuua kwa risasi Rais Joao Bernardo Vieira, maofisa wa serikali wamesema. Habari hizo zilikuja jana saa chache baada ya mauaji ya mkuu wa majeshi ambaye alikuwa katika mtafaruku na Rais.

  Milio ya risasi ilisikika jijini hapa na mpaka leo hakukuwa na taarifa za nani anaiongoza serikali. Nchi hii ni moja ya nchi masikini sana duniani, na ina historia ya mapinduzi ya serikali na imekuwa njia kuu ya dawa za kulevya, hususan kokeni kwenda Ulaya.

  Taarifa ziliwakariri maofisa wa kijeshi na serikali waliosema Rais ameuawa. "Rais Vieira aliuawa na Jeshi alipokuwa akijaribu kukimbia makazi yake ambayo yalishambuliwa na kikundi cha wanajeshi watiifu kwa aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Tagme Na Waie, mapema asubuhi hii," msemaji wa Jeshi, Zamora Induta aliiambia AFP.

  Alimtuhumu Rais Vieira kwa kuhusika na mauaji ya mkuu wa majeshi. Jenerali Tagme aliuawa baada ya mlipuko kusikika juzi na kuharibu sehemu ya makao makuu ya jeshi. Msaidizi wake, Luteni Kanali Bwam Nhamtchio, alisema Tagme alikuwa ofisini mlipuko huo ulipotokea. "Alijeruhiwa sana asingeweza kupona.

  Hili ni pigo kwetu sote," alisema Nhamtchio. Takriban watu watano waliripotiwa kuuawa na mlipuko huo. Kutokana na mashambulizi hayo dhidi ya makao makuu ya Jeshi, maofisa waliviamuru vituo viwili vya redio kusitisha matangazo.

  "Kwa usalama wenu waandishi wa habari, fungeni kituo na kuacha kutangaza. Ni kwa usalama wenu," msemaji wa Jeshi Samuel Fernandes aliwaambia waandishi wa habari katika moja ya vituo hivyo. "Tunakwenda kupambana na wavamizi na kujilinda," aliongeza.

  Rais na Mkuu wa Majeshi inasemekana wamekuwa hawaelewani kwa miezi kadhaa sasa. Askari hao waasi Novemba mwaka jana walishambulia makazi ya Rais katika jaribio la mapinduzi ambalo halikufanikiwa. Haijajulikana nani kiongozi wa mashambulizi dhidi ya Jenerali Tagme, lakini inaonyesha jinsi amani ya nchi hii ilivyo tete bado, mwandishi wa BBC alisema.

  Baada ya mashambulizi ya Novemba mwaka jana, Rais alipewa kikosi maalumu chenye askari 400 kumlinda. Januari mwaka huu, askari hao walituhumiwa kujaribu kumuua mkuu wa majeshi na kikosi hicho kikavunjwa. Nchi hii imegubikwa na mfululizo wa mapinduzi na machafuko ya kisiasa tangu ilipopata uhuru wake kutoka Ureno mwaka 1974.

  Rais Vieira, kama walivyokuwa viongozi waliomtangulia, alikuwa akitegemea sana Jeshi ili kubaki madarakani. Guinea-Bissau ambayo imekuwa njia kuu ya kupitisha mihadarati kutoka Amerika Kusini kwenda Ulaya, imeathirika kwa kiasi kikubwa pia na biashara hiyo. Baadhi ya maofisa jeshini nao wanajulikana kwa kushiriki katika biashara hiyo, chanzo cha habarti kilisema.

  Marehemu Vieira ni mwanajeshi aliyeingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi, lakini akaondolewa pia na wapinzani wake wa kijeshi na akashinda uchaguzi mara mbili. Alipozaliwa mwaka 1939 nchi hii ilikuwa bado ikitawaliwa na Wareno na alijiunga na chama cha African Party for the Independence of Guinea-Bissau and Cape Verde (PAIGC) mwaka 1960 na kupigania uhuru.

  Uhuru ulipatikana mwaka 1974 lakini nchi hii imekuwa katika mgogoro kwa kipindi chote hicho chini ya utawala wa kidikteta. Aliingia madarakani mwaka 1980 kupitia mapinduzi ya kijeshi wakati akiwa mkuu wa majeshi, na miaka 11 baadaye aliondoa marufuku dhidi ya vyama vya siasa kabla ya uchaguzi wa mwaka 1994, ambao alichaguliwa kuwa rais.

  Lakini miaka mitano baadaye alipinduliwa baada ya kumfukuza kazi mkuu wa majeshi kwa tuhuma kuwa alikuwa akiwaunga mkono waasi waliokuwa Senegal. Alitimuliwa PAIGC kwa tuhuma za uhaini, kuunga mkono mapigano na vitendo vilivyokuwa vikikiuka kanuni za chama hicho.

  Katika mapinduzi ya mwaka 2003, alirejea nchini kutoka uhamishoni Ureno na kugombea urais na kushinda kama mgombea binafsi mwaka 2005. Katika kampeni zake, Vieira alikuwa akijitambulisha kama zawadi kutoka kwa Mungu kwa watu wa Guinea-Bissau-ili arudi kuwaongoza kupata maendeleo na maisha bora. Alishinda kwa asilimia 52 katika mzunguko wa pili wa upigaji kura katika uchaguzi ambao uliitwa mtulivu na huru na waangalizi wa Ulaya.
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Nimechoka na haya maswali ya kijifunza nini :confused: Watu wanapigana Somalia, wanatanzania tumejifunza nini :confused: Rwanda wanapigana, tumejifunza nini :confused:

  Hata siku moja sijawahi kuulizwa nimejifunza nini na waMarekani kwenda mwezini ???

  Kwa maoni yangu it's time to move on.
   
 15. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Huyu nae 1980 aliangusha serikali iliyokuwepo..na sasa wamemuua! Viera pia amehisika kumuua jana Mkuu wa Majeshi kwa hiyo askari waliompenda Mkuu wa majeshi ndo wamerevenge!

  Mapinduzi???? Yaani Beni unamaanisha mapinduzi gani ndugu?

  Amini nae alimpindua Obote, Nkrumah kipenzi cha wengi naye alipinduliwa!

  Sasa hapo Tz tunajifunza nini?

  Mapinduzi ya kura kama ilivyotokea Ghana rulling party ikampa opposition haya ndo mapinduzi ya kweli!

  Ila mapinduzi ya kuuana..hupandikiza mbegu mbaya..na huweka visasi kwa mda mrefu!

  Angalia Samweli Doe (Liberia), Idd Amin n.k
   
 16. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 929
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 180
  Jamani hata kuiba kura wakati wa uchaguzi ni mapinduzi sawa tu na anayetumia mtutu. Kwa hiyo mwizoi wa namna hiyo akiondolewa kwa mtutu ni kosa gani?
   
 17. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mapinduzi ndiyo njia sahihi iliyobaki africa, kwa kuwa watawala wanarewfusha vipindi vyao vya ukomo kwa kutumia rushwa, ukabila, kubadili katiba, alichofanya kibaki kuiba kura nisawa pia na mapinduzi alipaswa kupigwa risasi hadharani badala ya wakenya 1500 waliopoteza maisha kwa ajili ya zee lile.

  hapa kwetu, unafiki wa viongozi wa ccm umefikia mahali pabaya, wizi wa kura, wizi wa pesa kwenye taasisi za umma kwa nia ya kuhonga wapiga kura, ukabila na udini bila kusahau ukanda

  watawala kama hawa ndio wanaosababisha kuuawa kwa risasi kama viera! hatuna la kusikitika leo waganda wakiamua kumwondoa museveni kwa njia hiyo hiyoo

  mapinduzi ndiyo fikra na njia mbadala mpaka hapo tutakapokomaa kidemokrasia kama nchi za magharibi au nchi chache za kiafrika kama botswana
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Naona Mapinduzi ndiyo njia sahihi katika mazingira kama niliyoyataja hapo juu.Kuna haja gani ya kwenda kupiga kura kama hakuna tume huru ya uchaguzi? Kuna haja gani ya kupiga kura kama utaiba au utavuruga na hata kukataa matokeo?

  Kugawana madaraka ndiyo suluhisho? NO,LAZIMA WAJUE KWAMBA WANANCHI HAWAWATAKI.KUMKATAA MKOLONI MWEUPE<HAIKUMAANISHA KUWAKUBALI WAKOLONI NA WADHALIMU WEUSI.
   
 19. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Majanga kama hayo na mauti kama hayo ni sawa na ajali inayosubiri kutokea haitabiriki katika ulimwengu tunaoishi
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,070
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Nafikiri lingeamia afrika mashariki

  haya mambo ya ufisadi''''''''''''''''''''''''''''''mauaji ya albino'''''''yasingekuwepo kabisa

  wangetuletea baadhi ya waliorushiana wakawapeleka pale tarime

  hakika jk angekuwa na heshima na hii nchi

  hilo ni wazo tu uanruhusiwa kuungana namia ama kushiriki kwenye ufisadi na mauaji ya albino
   
Loading...