Konnie habari yako haina mushkeli wowote...
Mimba ya mtoto mmoja na isiyo na complications:
Kuna medical guidelines za IATA zinazowaruhusu wajawazito kusafiri kwa ndege kwa ujauzito usiozidi wiki 36 na wa mahesabu haya ya muda hutumia kigezo cha ESD 'Estimated Date of Delivery'.
Isipokuwa zaidi ya wiki 28, mama mjamzito anapaswa kuwa na vipimo kutoka kwa daktari mwenye uzoefu na safari za anga kwa mama wajawazito za kumruhusu kusafiri.
Mimba ya zaidi ya mtoto mmoja na isiyo na complications:
Medical guidelines za IATA zinazowaruhusu wajawazito wa namna hii kusafiri kwa ndege kwa ujauzito usiozidi wiki 32.
Isipokuwa zaidi ya wiki 28, mama mjamzito anapaswa kuwa na vipimo kutoka kwa daktari mwenye uzoefu na safari za anga kwa mama wajawazito za kumruhusu kusafiri.
Mwanamke aliyepatwa na miscarriage wakati au kabla ya safari, haruhusiwi kusafiri hadi atibiwe na masaa 24 yawe yamepita.
Ukiacha na haya kuna guidelines nyingine za idadi ya masaa ambayo mjamzito anapaswa kusafiri angani, special treatments n.k
Pia mashirika mbalimbali ya ndege hutofautiana masharti ya namna ya kuwahudumia wajawazito na ruksa za kumfanya wasafiri.
References:
IATA Medical Guidelines:
http://www.iata.org/whatwedo/safety/health/Documents/medical-manual-2013.pdf
Masharti ya Mashirika Mbalimbali ya Ndege:
Airline policies for pregnant women | Gurgle.com
nimekuita kama tbs, dr gugo haaminiki ukizingatia mie fundi mchundo.