GUARDIAN UK: January Makamba fighting corruption in Tanzania

Kinachowaumiza watu hapa ni chuki na wivu. Guardian UK hawaandiki bila research. Ni gazeti linalosomwa na kuheshimika kote duniani. Kama mtu anadhani kwamba mwanasiasa tena kutoka Afrika anaweza kujipigia pande au kupigiwa pande akaandikwa kwenye gazeti la kimataifa basi mtu huyo akili yake fupi. The Guardian hawawezi kuchukua risk ya ku-profile mtu wa hovyo. Wameangalia upuuzi Wote unaondikwa hapa kila siku juu ya JM, sijui Barrick sijui nini, wakaona ni majungu tu. Na hayo majungu ndio chanzo kikubwa cha ufukara wetu wa fikra.

Poa tu, kwa sababu hata BAE ni kampuni ya China!:A S confused:
 
Empathy my foot!
Badala ya kupoteza hela kufanya kampeni ya kukamata Petty corruptors, hao 6.9% wanaoripotiwa, wangapi wanapelekwa mahakamani, wanagpi wanachukuliwa hatua, na wangapi wanafilisiwa? Unatudanganya vijana wenzio, umesahau baba aliwadanganya wazee wenzie manake aliwazidi maarifa. And the useless journalists cant even ask the simplest question! Mliowapata mmewafanya nini hadi mnasaka wengine????

Na sms usiite exciting innovation, hata boutique uchwara za mtaani wanatutumia wakiwa na sale mzigo mpya from hong kong na thailand! Tigo na voda wako busy wanazichanga from all angles and walks of life

Mkuu kumbuka January sio serikali, Pili ripoti ya 6% nani anajua. Tofauti yake ni kwamba huu mpango utakuwa unaonekana dunia nzima kwa vile kila atakayetuma itaonekana kwenye ramani kwamba trafiki wa selanda kwa mfano ameomba rusha. Kama ripoti inaonekana duniani nzima pccb hawatawajibika?
 
So January is darling of the west now. They beleive through him their interest will be protected. They are to keep in minda that we able to handle our own thing now we do not need their opinion. January need to do a lot to his people of Bumbuli to win most Tanzania dead heart toward CCM. As part of ruling part he has to defect to win and prove western autocracy.

Yes this is the thinking of bongo politicians.They have to be loved first by the west so they can receive hongo from multinationals.Hamshangai hayo mabilioni yaliyoko uswizi.

What about the big fish?Makamba anafanya nini kuwaibua mafisadi wakubwa walio ndani ya chama chake?
 
Nawaambieni nyote JK anajuta juto kuu kwa uteuzi wa Prof Muhongo, miradi ya Luku za Riz Moko, miradi ya JMakamba na kubwa lao campaign manager itakuwa hadharani (Kinana kaa mkao wa kula )

Ataambiwa aache, yanashuhulikiwa na ngazi za juu. Hujui nguvu ya hawa mafisadi ee?
 
Kwani kuwa masikini Tanzania nikitu cha ajabu?Wao wenye "humble beggining",wamefanikiwa kipesa kwasababu ya siasa.Sasa ndo message gani hiyo kwa wananchi?Obama historia yake inamake sense since taifa la marekani ni tajiri na ni ajabu kiaina mtu kuwa na background kama yake.
Hatudanganyiki!

Usiseme tu humble beggining na wakati at the end umewageuka wale unaowareflect,yani the very same people that you're representing and leading.Yani you're living way different from them,kwahiyo ni kutoka kwenye humble beggining hadi kwenda kwenye "cowardness"
 
Gazeti la The Obsever siyo KIU au IJUMAA kusema kuwa unaweza ku-lobby au kutoa hongo kwa mhariri ili uandikwe.

Jambo kubwa ambalo mwanadamu mwenye uelewa anatakiwa kufanya kabla hajatoa maoni yake juu ya jambo lolote ni kufanya utafiti. The Observer, gazeti dada la the Guardian ya London ni gazeti lenye historia ndefu katika harakati za mapinduzi barani Afrika toka David Astor akiwa bado mhariri na mmiliki wa gazeti hilo. Ni gazeti pekee ambalo liliwasaidia wakina Mandela na wapiganiaji wengine wa uhuru kwenda Uingereza katika harakati hizo na kutoa mchango kuliko gazeti lolote ulaya na Marekani katika ukombozi huo. Kwahiyo, mimi sioni ajabu The Observer kuchapisha profile ya January makamba.

Lakini pia, ni muhimu wengi wetu tukajua kuwa kama alivyo Zitto Kabwe kwa Chadema, Kafulila kwa NCCR-Mageuzi na CCM ina January Makamba ambaye si mwanasiasa mjinga mjinga kama wengi wenu mnavyotaka tuamini hapa. Ni mtu aliyesoma vizuri na anajua anachofifanya. Na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, ndiye mwanasiasa aliyeanzisha shirika la maendeleo ya jimbo lake.

CCM kama vilivyo vyama vingine vya siasa, kina mapungufu yake na labda hatujaona mapungufu hayo kwakuwa vyama hivi havijashika madaraka. Wakati mwingine, mihemko yetu ya kisiasa inatufanya tushindwe kuviangalia kwa jicho pevu. Mbali na mapungufu hayo, bado chama hiko kina haki ya kuwajenga vijana wenye mawazo mapya ambao watasaidia kujenga Tanzania mpya.

Ndoto ya watanzania siku zote ni kuwapata vijana wenye mawazo mapya (regardless wanatoka chama gani cha siasa) ili watusaidie kujenga nchi. Mimi binafsi, sifikiri kuwa tunahitaji kumzomea January eti kisa anatoka CCM au ni mtoto wa Makamba. Tunahitaji kuweka chuki zetu za kisiasa pembeni na kum-judge kama yeye binafsi.

Mimi binafsi nampongeza kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania ili wenzetu waone kuwa vijana kama January wanamawazo mpya ya kuijenga nchi hii. Ni wanasiasa wengi wakongwe hapa nchini ambao hawajawahi kuandikwa hata kwenye magazeti ya Afrika Mashariki.
 
Gazeti la The Obsever siyo KIU au IJUMAA kusema kuwa unaweza ku-lobby au kutoa hongo kwa mhariri ili uandikwe.
Jambo kubwa ambalo mwanadamu mwenye uelewa anatakiwa kufanya kabla hajatoa maoni yake juu ya jambo lolote ni kufanya utafiti. The Observer, gazeti dada la the Guardian ya London ni gazeti lenye historia ndefu katika harakati za mapinduzi barani Afrika toka David Astor akiwa bado mhariri na mmiliki wa gazeti hilo. Ni gazeti pekee ambalo liliwasaidia wakina Mandela na wapiganiaji wengine wa uhuru kwenda Uingereza katika harakati hizo na kutoa mchango kuliko gazeti lolote ulaya na Marekani katika ukombozi huo. Kwahiyo, mimi sioni ajabu The Observer kuchapisha profile ya January makamba.
Lakini pia, ni muhimu wengi wetu tukajua kuwa kama alivyo Zitto Kabwe kwa Chadema, Kafulila kwa NCCR-Mageuzi na CCM ina January Makamba ambaye si mwanasiasa mjinga mjinga kama wengi wenu mnavyotaka tuamini hapa. Ni mtu aliyesoma vizuri na anajua anachofifanya. Na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, ndiye mwanasiasa aliyeanzisha shirika la maendeleo ya jimbo lake.
CCM kama vilivyo vyama vingine vya siasa, kina mapungufu yake na labda hatujaona mapungufu hayo kwakuwa vyama hivi havijashika madaraka. Wakati mwingine, mihemko yetu ya kisiasa inatufanya tushindwe kuviangalia kwa jicho pevu. Mbali na mapungufu hayo, bado chama hiko kina haki ya kuwajenga vijana wenye mawazo mapya ambao watasaidia kujenga Tanzania mpya.
Ndoto ya watanzania siku zote ni kuwapata vijana wenye mawazo mapya (regardless wanatoka chama gani cha siasa) ili watusaidie kujenga nchi. Mimi binafsi, sifikiri kuwa tunahitaji kumzomea January eti kisa anatoka CCM au ni mtoto wa Makamba. Tunahitaji kuweka chuki zetu za kisiasa pembeni na kum-judge kama yeye binafsi. Mimi binafsi nampongeza kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania ili wenzetu waone kuwa vijana kama January wanamawazo mpya ya kuijenga nchi hii. Ni wanasiasa wengi wakongwe hapa nchini ambao hawajawahi kuandikwa hata kwenye magazeti ya Afrika Mashariki.
Na kama ni umakini, na si self promotion, nafikiri Observer wangetambua kwamba John Mnyika anayo more fascinating story kuliko January Makamba. Au wenyewe wanaangalia wanasiasa wa CCM peke yake?
 
jmushi1

Mkuu, hapa ndipo mimi ninapotofautiana na baadhi yetu humu! Tunapaswa tuwe na genuine appreciation kwenye every good deed someone does, na kiukweli, this guy ni briliant na upstairs yuko fit sana!.

Niliwahi kusafiri nae same flight na baada ya hapo nikapanda lift yake na ndipo nilipokuja kumfahamu vizuri, kiukweli, he should have not supposed to be CCM kwa sababu anaelewa fika how CCM stink with rushwa, huyu alipaswa kabisa kuwa kwenye opposition, tatizo lake he is too genuine, anaijua vizuri Tanga, anawajua vizuri watu wa Tanga, ameamua kubaki CCM just not to waste the opportunities, ili watu wa type hii, 'young, vibrant reformists, wakiishika CCM vilivyo, nawahakikishia 2015, ikulu tutaishia kuisikia kwenye bomba tuu!. Thank God CCM is rot toka kwenye mizizi, anachotaka kufanya ni kukata tuu matawi ya rushwa kule kwenye ncha kwa kuibua hivi vijirushwa vidogo vodogo vya kiasi cha mboga, huku mashina na mizizi yenye grand corruption are untouchable na huu ndio mtaji mkubwa wa kifo cha CCM!.

Mushi, tuwe wakweli, Watanzania wangapi wanaweza ku secure international loan?, wangapi wanajua "bond" bussiness?, wangapi wanaweza kuwekeza "wall street? etc?. This is a good move na kama ni kweli, Chadema itachukua 2015, then 2020 ni January type watairudisha madarakani na itatawala milele!.
Mkuu hii umeshajibiwa,nakubaliana na majibu ya member kina Gagnija,Baba Desi et al.
 
Last edited by a moderator:
Yes this is the thinking of bongo politicians.They have to be loved first by the west so they can receive hongo from multinationals.Hamshangai hayo mabilioni yaliyoko uswizi.

What about the big fish?Makamba anafanya nini kuwaibua mafisadi wakubwa walio ndani ya chama chake?
Unauliza anafanya nini wakati anaanzisha mkakati wa wazi kwa watanzania kuripoti wala rushwa?
 
jmushi1

Mkuu, hapa ndipo mimi ninapotofautiana na baadhi yetu humu! Tunapaswa tuwe na genuine appreciation kwenye every good deed someone does, na kiukweli, this guy ni briliant na upstairs yuko fit sana!.

Niliwahi kusafiri nae same flight na baada ya hapo nikapanda lift yake na ndipo nilipokuja kumfahamu vizuri, kiukweli, he should have not supposed to be CCM kwa sababu anaelewa fika how CCM stink with rushwa, huyu alipaswa kabisa kuwa kwenye opposition, tatizo lake he is too genuine, anaijua vizuri Tanga, anawajua vizuri watu wa Tanga, ameamua kubaki CCM just not to waste the opportunities, ili watu wa type hii, 'young, vibrant reformists, wakiishika CCM vilivyo, nawahakikishia 2015, ikulu tutaishia kuisikia kwenye bomba tuu!. Thank God CCM is rot toka kwenye mizizi, anachotaka kufanya ni kukata tuu matawi ya rushwa kule kwenye ncha kwa kuibua hivi vijirushwa vidogo vodogo vya kiasi cha mboga, huku mashina na mizizi yenye grand corruption are untouchable na huu ndio mtaji mkubwa wa kifo cha CCM!.

Mushi, tuwe wakweli, Watanzania wangapi wanaweza ku secure international loan?, wangapi wanajua "bond" bussiness?, wangapi wanaweza kuwekeza "wall street? etc?. This is a good move na kama ni kweli, Chadema itachukua 2015, then 2020 ni January type watairudisha madarakani na itatawala milele!.

Mkuu,kuijua Tanga na watu wa Tanga is that enough? Je,umeshatembelea jimbo la Bumbuli ambako yeye ni mbunge? Umaskini,ujinga na maradhi ambavyo vinawasumbua watu wa huko,vimepungua au kutokomezwa kwa kiasi gani? Maana huwezi ongelea matatizo ya nchi wakati ktk constituency yako mambo bado hayajakaa uzuri.
 
Last edited by a moderator:
fishseller

Kwa hiyo kwa sababu guardian imeandika basi unaamini kila kitu.Unajua maana ya eurocentrism?Haya magazeti yote yapo kuwatumikia wazungu ambao wako ignorant na issues za hapa africa.Kwa mfano mbona hiyo article haijasema kwamba makamba ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe tanzania?Mbona hiyo article haikusema chama cha makamba is the most corrupt partyin Tanzania?
 
Last edited by a moderator:
Na kama ni umakini, na si self promotion, nafikiri Observer wangetambua kwamba John Mnyika anayo more fascinating story kuliko January Makamba. Au wenyewe wanaangalia wanasiasa wa CCM peke yake?

Kama John Mnyika angeanzisha mRushwa au BDC nina uhakika The Guardian NA The Economist wangemuandika.
 
Kama ripoti inaonekana duniani nzima pccb hawatawajibika?

Great thinker, seriously?!?

Unamaanisha kwa PCCB kufanya kazi yake ni mpaka dunia nzima ifahamu kuna rushwa Tanzania?
Kwani dunia haifahamu? Hujawahi kuona ripoti za Transparency International?

Kwa upande mwingine,mawazo kama yako ndiyo yanalifanya taifa letu kuwa tegemezi na shamba la bibi. Yaani taasisi zetu haziwezi kuwa fanisi mpaka 'wakubwa' wakorome? Kumbe ndiyo maana bajeti ya serikali usomwa kwa 'wakubwa' hao kabla ya hata raia kuisikia!
 
Na kama ni umakini, na si self promotion, nafikiri Observer wangetambua kwamba John Mnyika anayo more fascinating story kuliko January Makamba. Au wenyewe wanaangalia wanasiasa wa CCM peke yake?
Kwani Mnyika kazuiwa kutafuta self-promotion? Kumbuka kuwa opportunities hazikufuati ndugu, unazitafuta na kuzifuata katika kila eneo - siasa, elimu n.k. Mimi binafsi napenda watu aggressive, hata JF wangesubiri mtu aje kuwaanzishia JF leo hii tusingepata platform hii. Pia, kama rais Obama angesubiri aletewe urais mezani, historia leo isingeandikwa.

Navutiwa sana na wanasiasa vijana hapa nchini ambao wanasoma, wanafanya utafitia na wanajua wanachokitaka kama Lissu, Mnyika, Zitto, Makamba kwasababu wametufanya tupate matumaini kuwa siku moja nchi hii tabadilika.

Kama mtanzania mwenye kiu ya maendeleo, wanasiasa wenye mtazamo kama January Makamba nitawaunga mkono bila kujali itikadi za vyama vyao. Tanzania kwanza, siasa baadae.
 
huyu mtu mnafiki balaa. majungu babu kubwa

9k=
 
I think the man is brilliant and he turn some ideas into reality. The prob is how, in case he is given power, he would go against political giants in his party. hawa watu wanalindana kiasi cha gharama za maisha watanzania masking!
 
Mkuu kumbuka January sio serikali, Pili ripoti ya 6% nani anajua. Tofauti yake ni kwamba huu mpango utakuwa unaonekana dunia nzima kwa vile kila atakayetuma itaonekana kwenye ramani kwamba trafiki wa selanda kwa mfano ameomba rusha. Kama ripoti inaonekana duniani nzima pccb hawatawajibika?
Mkuu hivi dunia nzima ikiona then what ?, kumbuka mara nyingi mtoa rushwa na muomba rushwa wote huwa ni waharifu (mmoja anataka short cut na mwingine anajali tumbo lake) therefore wengi hawatatuma hizo sms, pili watakaotuma where is the proof ?

Au ni kutaka kuwa na millions of unsolvable cases without evidences..., na kama issue ni kujua tatizo la rushwa ni kubwa vipi nani hajui ?, na kama issue ni kusolve au kupata ushahidi nenda ofisi za PCCB kuchukua pesa zenye marks na ingia ofisi yoyote ya serikali kama hautapata mtoa rushwa na kuwa na proof kabisa.., Hapa huyu bwana na hii mbinu yake sio kusolve tatizo bali ni kupiga kelele na kuleta theories ambazo practically they are just hogwash
 
Hata siku moja sijawahi kuona wala kusikia mtu kathibitisha tuhuma za ufisadi dhidi ya Januari Makamba. Watu wametengeneza mabomu humu ndani JF juu yake lakini hakuna hata moja limemkamata kwasababu hakuna ukweli. Hata kwenye newsrooms za magazeti ya Bongo kumepelekwa mizinga wahariri wenyewe wameangalia wakaona ni majungu na wakaogopa kuzirusha hizo habari.
 
Back
Top Bottom