Gregorian chants; Kiboko dhidi ya mashetani na sonona (depression)

Gregorian chants; Kiboko dhidi ya mashetani na sonona (depression)

Mkwawe

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2016
Posts
3,210
Reaction score
5,680
Wakati mmoja nilikuwa na-scroll reels za Facebook ikatokea clip moja ikionesha watawa wa kikatoliki wakiimba Kwa ala za kuvutia sana (angelic voices). Hiyo clip ilikuwa ikimuonesha msanii wa kimarekani Kai Cenat akishangaa jinsi zile sauti zilivyokuwa zinavutia hata Mimi zikanishangaza sana, kupitia comments nikajua kumbe ule mtindo unaitwa Gregorian chant unaotumiwa na kanisa Katoliki katika Sala za tafakuri na maombi ya kina.

Nilipakua nyingi sana na chant ya kwanza kabisa ilikuwa inaitwa "Anima Christi" ya Marco Frisina ilikuwa fupi na niliipenda ilabidi nipakue extended yenye muda saa zima, Kila nilipokuwa nasikiliza nilikuwa najisikia utofauti wa Hali ya juu nikawa kama napokea kitu kipya ndani yangu. Na nyakati zote nikiwa najihisi kutotulia kiakili huwa nakaa katika utulivu Kwa angalau masaa mawili nikisikiliza Gregorian chant na wakati mwingi ninaambatanisha na kusali Rozari

Kwa atakayependa kutafakari na Gregorian chants atakuja kuleta mrejesho humu
 
Gregorian chant ni nini?

✅ Maana:
Gregorian chant (inayojulikana pia kama “Plainchant” au “Plainsong”) ni aina ya muziki wa kanisa la Kikristo, hasa Kanisa Katoliki, uliotumika sana katika ibada za karne za kati. Ni nyimbo za kidini zinazokaririwa kwa sauti moja (monophonic), bila ala za muziki, zikiwa na mtindo wa utulivu na wa kiroho.

✅ Sifa kuu:

Hutumika kuimba maandiko matakatifu (kama Zaburi na Injili).

Hauna midundo ya muziki wa kawaida; ni kama kusoma kwa sauti ya kiibada yenye mdundo wa maneno.

Una ladha ya utulivu na unatulia moyoni, hivyo hutumika sana kwa tafakari na maombi.

Mara nyingi huimbwa kwa Kilatini.

Unahusishwa na Papa Gregory I (kwa jina lake Gregorian), ingawa hakuiunda mwenyewe, bali ulipewa jina lake kwa sababu ya mchango wake katika kuupanga na kuueneza.


✅ Kazi yake:

Kuboresha ibada na maombi kwa kutoa hali ya utakatifu na utulivu.

Kutumika kama sehemu ya liturujia za kanisa (misa, maombi ya saa).

Kuwa msingi wa muziki wa kanisa na hata muziki wa magharibi wa baadaye.
 
Hebu ziweke hapa mkuu
Chant ni manuizi ya kiroho yenye kuleta matokeo kimwili.
Inategemea na Imani yako.
Unajua akili ni freewill vyovyote vile utakavyo ielekeza ndivyo.
Zipo na unaweza jitengenezea vyovyote utakavyo
.Nayaweza yote katika yeye anitiae nguvu.
.Tarudi kijijini either maiti au tajiri
.Atakaenianza atajimaliza mwenyewe.
.Mimi ni kichwa sio mkia.
Nk
 
Chant ni manuizi ya kiroho yenye kuleta matokeo kimwili.
Inategemea na Imani yako.
Unajua akili ni freewill vyovyote vile utakavyo ielekeza ndivyo.
Zipo na unaweza jitengenezea vyovyote utakavyo
.Nayaweza yote katika yeye anitiae nguvu.
.Tarudi kijijini either maiti au tajiri
.Atakaenianza atajimaliza mwenyewe.
.Mimi ni kichwa sio mkia.
Nk
Manuizi Hayo unakuwa unayasema moyoni au kwa sauti
 
Mh.mm ila akili ukitaka ikuletee illusion , hallucinations yoyote inaweza tu 🤔
🤣🤣kuna siku nilikuwa naplay movie
Unajua movie ikiwa inaanza zile Title kuna vimlio
Nikawa nachek mwanzoni naskia sauti
Kuja kushtuka hivi😳 Subwoofer ilikuwa haijawashwa alf hamna sauti
Nilikuwa nimeathirika na movie sauti zake hata kama ilikuwa haina sauti naskia
 
🤣🤣kuna siku nilikuwa naplay movie
Unajua movie ikiwa inaanza zile Title kuna vimlio
Nikawa nachek mwanzoni naskia sauti
Kuja kushtuka hivi😳 Subwoofer ilikuwa haijawashwa alf hamna sauti
Nilikuwa nimeathirika na movie sauti zake hata kama ilikuwa haina sauti naskia
Ubongo unaweza kuletea vitu usipo kuwa makini unaweza amini mambo ya ajabu.
 
Back
Top Bottom