Great thinkers mawazo yenu yanahitajika hapa.

Carla

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
398
Reaction score
331
Katika mazingira mengi (most cases) wanadamu tumeumbwa kuitikia (respond) matukio mbali mbali kwa namna tofauti. Hata hivyo jambo hili linatofautiana kwa mwanadamu mmoja na mwingine.

Mfano ikitokea watu kadhaa wamepata taarifa za msiba. Kuna watakaochanganyikiwa na kuweza kupata au kupatwa na ajali kama watakuwa barabarani.

Au ikitokea mtu amepoteza ajira aliyokuwa akiitegemea sana kwa maisha yake kuna atakaye chukua hatua au maamuzi ambayo asingeyachukua kama asingepatwa na janga hilo.

Mara nyingi katika matukio kama haya au mengine tumekuwa tukishauriwa kutohamaki(panic) badala yake tumekuwa tukiambiwa “calm down”, “relax”, “ take it easy “ tukiaminishwa kuwa kwa kufanya hivyo tutaweza kuamua kwa busara na kuepuka ajali au matokeo hasi ya matendo yetu kutokana na kuhamaki(panic)
Swali linakuja.
  • Je, haiwezekani kuwa kwa kujaribu ku-calm down tutakuwa tunakinzana na maumbile halisi ya kiuumbaji(nature)?
  • Nauliza hili nikiamini mwili wa mwanadamu ulivyoumbwa kuitikia vichocheo (stimuli) uko sahihi na hauwezi kukosea. Kwa kuthibitisha hili angalia irisi (iris) ya jicho inavyoitikia mwanga mkali au mwanga hafifu, kinywa kinapoitikia kwa kutoa mate pale unapolitazama limao au ukwaju kwa kuutamani.
  • Sasa iweje mtu akihamaki(panic) tunajaribu kumtuliza?
  • Je, kwa kufanya hivyo hatukosei?
Naomba mawazo yenu watu wenye ufahamu juu ya jambo hili.
Asanteni sana.
 
Kuhamaki ni sehemu ya viumbe karibu vyote vilivyo hai.ni uumbaji wa MUNGU,na inapotokea kiumbe hicho kika hamaki na kikatulizwa bado hiyo ni power iliyoumbwa ndani ya kiumbe hai inayokubali kutulizwa au kupanikishwa.mtu pekee asiyeweza kuhamaki kwa haraka sana ni yule asiyekula nyama nyekundu.maana kwenye nyama ya viumbe kama ng'ombe kuna kitu hua kinakua kama nyongo fulani hivi kinachoweza kutengeneza body vibration,na kile kitu kwenye nyama wala hua hakiishi,mfano ukimchinja mnyama ile hasira na kuhamaki kwake kunajaa mwilini na kudumu kwa muda mrefu kufanya msukumo wa kujitetea,unakuta mnyama keshakufa lakini mpaka unamchuna utaona nyama yake inaweka mitetemo fulani.unapoipika ile nyama na kuila baada ya muda kule mwilini mwako ile kitu kama nyongo inaamka na kukutengenezea mitetemo ndani yako.hiyo ndiyo inayoweza kusafili ktk mishipa yako yote ya fahamu na ubongo.sometimes inasinzia na ukishitushwa tu na kitu kama hata kumuona nyoka pembeni yako inaamka ghafla na kufumba na kufumbua unajikuta uko mbali pasipo wewe kujua.sasa kitu hichi ndicho husababisha hasira au hata kupigana.viumbe vyote hai tumeumbiwa hivyo na unapokula na nyama nyingine tena unaongezea kichocheo.sasa kitu hiki ukikasilishwa au ukitukanwa au ukipewa taarifa mbaya hua kinaamka fast na kukutengenezea kuhamaki,lakini pia kinaweza kutulizwa kwa kuombwa msamaha au kutokutendewa kitu kibaya ambacho hakikupangwa kitokee ghafla.
Hii ni kwa uelewa wangu japo naweza kua nimeongea kitu kigumu anaweza kuja mwingine akasema kiundani au akasema ajuacho

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Kuna wajuvi mkuu, ila nafikiri hisia zinaweza kushuka au kupanda (kujizuia) tofauti na macho, sikionk
Kitu kinapolikaribia jicho lako na jicho kujifumba lenyewe kwa haraka, hiyo ni automatic response ya jicho na hatuwezi kusema kuna makosa ya kimfumo. Vivyo hivo unapo-panic ni automatic response ya mwili sasa iweje tushauriane ku-calm down? Kwanini tusiache mtu katika hali ya kuhamaki na atakachokifanya mpaka mwili utulie wenyewe?
 
Kuhamaki ni sehemu ya viumbe karibu vyote vilivyo hai.ni uumbaji wa MUNGU,na inapotokea kiumbe hicho kika hamaki na kikatulizwa bado hiyo ni power iliyoumbwa ndani ya kiumbe hai inayokubali kutulizwa au kupanikishwa.mtu pekee asiyeweza kuhamaki kwa haraka sana ni yule asiyekula nyama nyekundu.maana kwenye nyama ya viumbe kama ng'ombe kuna kitu hua kinakua kama nyongo fulani hivi kinachoweza kutengeneza body vibration,na kile kitu kwenye nyama wala hua hakiishi,mfano ukimchinja mnyama ile hasira na kuhamaki kwake kunajaa mwilini na kudumu kwa muda mrefu kufanya msukumo wa kujitetea,unakuta mnyama keshakufa lakini mpaka unamchuna utaona nyama yake inaweka mitetemo fulani.unapoipika ile nyama na kuila baada ya muda kule mwilini mwako ile kitu kama nyongo inaamka na kukutengenezea mitetemo ndani yako.hiyo ndiyo inayoweza kusafili ktk mishipa yako yote ya fahamu na ubongo.sometimes inasinzia na ukishitushwa tu na kitu kama hata kumuona nyoka pembeni yako inaamka ghafla na kufumba na kufumbua unajikuta uko mbali pasipo wewe kujua.sasa kitu hichi ndicho husababisha hasira au hata kupigana.viumbe vyote hai tumeumbiwa hivyo na unapokula na nyama nyingine tena unaongezea kichocheo.sasa kitu hiki ukikasilishwa au ukitukanwa au ukipewa taarifa mbaya hua kinaamka fast na kukutengenezea kuhamaki,lakini pia kinaweza kutulizwa kwa kuombwa msamaha au kutokutendewa kitu kibaya ambacho hakikupangwa kitokee ghafla.
Hii ni kwa uelewa wangu japo naweza kua nimeongea kitu kigumu anaweza kuja mwingine akasema kiundani au akasema ajuacho

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Asante mkuu ila umejibu sehemu tu ya swali kwenye maelezo yako.
 
mkuu mfano ukiona mtoto wako mpendwa amevutwa na papa baharin kutoka kwenye boti ni wazo gani litakuja akilini haraka! je hilo wazo litafanikwa....

ukweli ni kwamba Hata siku moja uwezi kufanya maamuzi sahihi ukiwa umepanick
 
Kumwambia mtu asipanic wakati kishapanic tayari ni kazi bure,

Lakini kuna njia ambazo mtu akijifundisha na akajizoesha taratibu itamsaidia kuweza kuwa mtulivu kwenye mazingira tofauti ya hatari pia na afya,

Kwa mfano kuna mtu akisikia maaskari wamekuja kumkamata anaweza kupanic vibaya mno, lakini kuna mwingine ambaye labda kwa njia moja ama nyingine anaweza asipanic kabisa kutokana na mazoea yake kwa maaskari,
 
Mtoa mada umeuliza swali zuri japo mifano yako haihusiani na jambo ulilouliza. Katika mifano yako umetaja mboni ya jicho na kutoa mate ambazo ni reflex actions. Reflex actions nyingine ni kama kupiga chafya na kujikuna unapowashwa. Hayo ni matendo ambayo mwanadamu anayafanya bila kufikiria. Na yanaongozwa na central nervous system. Sidhani kama kuna kiumbe yoyote anayeweza kufikiria kuwa sasa nipige chafya. Ila inatokea pale mfumo wa hewa unapojisafisha. Kwa maelezo hayo basi tukirudi kwenye swali lako ni kwamba matukio kama kufukuzwa kazi au tukio lolote la kuitikia kichokoo linaongozwa na ubongo. Hivyo ni kweli kabisa kama utakuwa na uelewa wa kutokukurupuka katika kufanya maamuzi basi itakuwa rahisi kwako kuweza kufanya maamuzi ya busara bila kujidhuru wala kuathiri afya yako. Binadamu tumepewa akili na utashi. Na huo ndio hutuongoza katika mambo yote yanayotumia akili. Kikubwa katika yote ni kujua jinsi ya kukontrol mapigo ya moyo wako. Hili ni somo jingine. Namalizia kwa kusema Fikiri kabla ya kutenda.
 
Naona wadau wana subiri lkn ngoja mi ni-test kama sio kutoa wazo langu.
Ni kweli wkt mwingine ni vigumu kuzuia hisia kama ukiwa na mhamako (nikimaanisha kuhamaki sana) mkubwa lkn kuna mambo kadha wa kadha mtu anaweza kufanya hata kama ni kwa kujilazimisha ili mhamako huo usilete madhara yoyote. Kubwa ambalo mimi hulifanya ni kujizuia kwa nguvu zote kufanya maamuzi wakati nina hasira. Hii imenisaidia kuepuka mengi sana katika life yangu.. so kwa kujaribu wakuu just chukua hiki kiji point.. USIFANYE MAAMUZI PALE UNAPIKUWA MWENYE HASIRA
 
Mtu anatulizwa kuepusha kadhaa zaidi, kama ulivyoeleza mwenyewe.
Pia kumtuliza kutamfanya akubaliane na ukweli, kuwa limeshatokea lililotokea, iliyobaki ni kukubaliana na hali halisi ambayo haiwezi kubadilika.
 
Ni kitu ambacho unaweza kucontrol , nakumbuka wakati nina balehe swala la hasira na kuchukua maamuzi ya haraka kutokana na mambo mbalimbali ilikuwa kawaida kwangu lakini nashukuru Mungu nowdays i can control my self baada ya kupata several counseling , so tunashauri ku "calm down " as you said so as kuepusha madhara yatakayoweza kutokea as a result ya kufanya maamuzi kupitia mihemko so ni kitu kinachoweza kucontrol kabisa.
 
Katika mazingira mengi (most cases) wanadamu tumeumbwa kuitikia (respond) matukio mbali mbali kwa namna tofauti. Hata hivyo jambo hili linatofautiana kwa mwanadamu mmoja na mwingine.
Mfano ikitokea watu kadhaa wamepata taarifa za msiba. Kuna watakaochanganyikiwa na kuweza kupata au kupatwa na ajali kama watakuwa barabarani.
Au ikitokea mtu amepoteza ajira aliyokuwa akiitegemea sana kwa maisha yake kuna atakaye chukua hatua au maamuzi ambayo asingeyachukua kama asingepatwa na janga hilo.
Mara nyingi katika matukio kama haya au mengine tumekuwa tukishauriwa kutohamaki(panic) badala yake tumekuwa tukiambiwa “calm down”, “relax”, “ take it easy “ tukiaminishwa kuwa kwa kufanya hivyo tutaweza kuamua kwa busara na kuepuka ajali au matokeo hasi ya matendo yetu kutokana na kuhamaki(panic)
Swali linakuja.
  • Je, haiwezekani kuwa kwa kujaribu ku-calm down tutakuwa tunakinzana na maumbile halisi ya kiuumbaji(nature)?
  • Nauliza hili nikiamini mwili wa mwanadamu ulivyoumbwa kuitikia vichocheo (stimuli) uko sahihi na hauwezi kukosea. Kwa kuthibitisha hili angalia irisi (iris) ya jicho inavyoitikia mwanga mkali au mwanga hafifu, kinywa kinapoitikia kwa kutoa mate pale unapolitazama limao au ukwaju kwa kuutamani.
  • Sasa iweje mtu akihamaki(panic) tunajaribu kumtuliza?
  • Je, kwa kufanya hivyo hatukosei?
Naomba mawazo yenu watu wenye ufahamu juu ya jambo hili.
Asanteni sana.
Kuna maoni yanayochukua kukubalika kwa sana sasa katika nyanja za saikolojia kwamba, ni vizuri watu kuachia hisia zao.

Kwa mfano, habari za kwamba wanaume ni shupavu na hawatakiwi kulia, angalau hadharani, zinapingwa, na wanasaikolojia wanasemakwamba mtu akijisikia kulia, halafu akajizuia kulia, hilo linamfanya akosekutoa hisia zake na atazikusanya zikae ndanikwa namna ambayo inaweza kumletea madhara baadaye.Kuna ushahidi wa kisayansi ya kikemikali unaoonesha kwamba matendo kama kulia huwa yanaendana na kuachilia kemikali fulani ubongoni, mwilini, na hivyo, kama mtu anajisikia kulia na asipolia, anawezakuwa anazifungia kemikalihizi asizitoe.

Mimi binafsi hupenda kuangaliamambo kimantiki, na kwenye vitu kama misiba, nakuwa mgumu kulia. Kwa kitambo sasa, nimejifunza kutohuzunika sana mambo yanavyokwenda kinyume na ninavyotaka, na pia kutofurahia sana mambo yanavyokwenda vizuri sana, nafikiri falsafa za ki Buddha nilizosoma, zinazoelezea umuhimu wa kuwa na equanimity (kuchukulia mambo yote kwa usawa wa mawazobila kuhamanika au kufurahi sana) zimenisaidia sana kuwa hivyo.

Pia, mimihujiona kamamtu wa kusaidia, kwa mfano, sehemu kama msibani, mimi hujiona kama askari ambaye atadaka wale wanaolia na kuanguka, sasa askari mimi tena nikilia, watu wakilia na kuanguka nani atawadaka? Muda wote nakuwa busy kuangalia logistics,kuna chakula? kuna vinywaji? Kuna viti? Nini kinahitajikakufanyika? Mipango inaendaje? Nani anahitaji msaada? Watu muhimu wana habari? Wazee wanaohitaji kusaidiwa wamesaidiwa? Watoto wataendanaje na mazingira haya? Habari za usafiri zimetengemaa? Kuna hatari ya mifarakano? Kama zipo, usuluhishi na uzuizi unaweza kugfanyaje? Kuna wanaotaka kupiga picha? Hilohalitaleta mtafaruku? Kuna mgongano wa kitamaduni?Pombe itanyweka? Walokole watasemaje? Waislamu watakula chakula kilicho halal? Maji yakosalama?

Yani kwenye msiba akili inaenda spidi ya mwanga hivyo, hata kulia nasahau.

Nitakuja kulia peke yangu wiki mojabaadaye, mwaka mmoja baadaye, au hata miaka ishirini baadaye.

Nikimkumbuka mtu peke yangu.
 
Mambo mengi ya mwanadamu yanaanzia kichwani....ndio maana watu wanasema kichwa ndio Mtu.....

Mwitikio wa mwili mara nyingi hutegemea fikra za mwili wako juu ya jambo Hilo!!!!

Kuhamaki kutokana na jambo fulani kunategemea na namna mwili ubongo ulivyolipokea hilo jambo.....na chochote utakachofanya ni hatua za haraka za ubongo kuutuma mwili kushughulika na msituko huo......lakini uharaka huo unaweza usiwe na matokeo Chanya na wakati kuleta madhara.....hivyo basi unatakiwa kutulia au kutuliza akili ili mwili wako uweze kurudi katika hali ya kawaida na kutafakari kwa hekima juu ya tukio........
 
Kuhamaki ni sehemu ya viumbe karibu vyote vilivyo hai.ni uumbaji wa MUNGU,na inapotokea kiumbe hicho kika hamaki na kikatulizwa bado hiyo ni power iliyoumbwa ndani ya kiumbe hai inayokubali kutulizwa au kupanikishwa.mtu pekee asiyeweza kuhamaki kwa haraka sana ni yule asiyekula nyama nyekundu.maana kwenye nyama ya viumbe kama ng'ombe kuna kitu hua kinakua kama nyongo fulani hivi kinachoweza kutengeneza body vibration,na kile kitu kwenye nyama wala hua hakiishi,mfano ukimchinja mnyama ile hasira na kuhamaki kwake kunajaa mwilini na kudumu kwa muda mrefu kufanya msukumo wa kujitetea,unakuta mnyama keshakufa lakini mpaka unamchuna utaona nyama yake inaweka mitetemo fulani.unapoipika ile nyama na kuila baada ya muda kule mwilini mwako ile kitu kama nyongo inaamka na kukutengenezea mitetemo ndani yako.hiyo ndiyo inayoweza kusafili ktk mishipa yako yote ya fahamu na ubongo.sometimes inasinzia na ukishitushwa tu na kitu kama hata kumuona nyoka pembeni yako inaamka ghafla na kufumba na kufumbua unajikuta uko mbali pasipo wewe kujua.sasa kitu hichi ndicho husababisha hasira au hata kupigana.viumbe vyote hai tumeumbiwa hivyo na unapokula na nyama nyingine tena unaongezea kichocheo.sasa kitu hiki ukikasilishwa au ukitukanwa au ukipewa taarifa mbaya hua kinaamka fast na kukutengenezea kuhamaki,lakini pia kinaweza kutulizwa kwa kuombwa msamaha au kutokutendewa kitu kibaya ambacho hakikupangwa kitokee ghafla.
Hii ni kwa uelewa wangu japo naweza kua nimeongea kitu kigumu anaweza kuja mwingine akasema kiundani au akasema ajuacho

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
basi kwa muktadha huu " kuna umuhimu" sasa wakazi wa africa wakaongeza ulaji wa nyama ya ng'ombe kwa wingi" maana matendo wanayotendewa na viongozi wao wamevuka mipaka" huwenda wakila hizo nyama" zitachangia kuongeza ukubwa wa panic" na kufanya maandamano ya pamoja ya kuwatoa madarakani", viongozi " wanao waongoza katika nchi zao " wanazoishi" pindi wanapowatendea ndivyo sivyo"...
 
mkuu mfano ukiona mtoto wako mpendwa amevutwa na papa baharin kutoka kwenye boti ni wazo gani litakuja akilini haraka! je hilo wazo litafanikwa....

ukweli ni kwamba Hata siku moja uwezi kufanya maamuzi sahihi ukiwa umepanick
Unataka kusema kuwa uumbaji umekosea kutuwekea panic?
 
Kumwambia mtu asipanic wakati kishapanic tayari ni kazi bure,

Lakini kuna njia ambazo mtu akijifundisha na akajizoesha taratibu itamsaidia kuweza kuwa mtulivu kwenye mazingira tofauti ya hatari pia na afya,

Kwa mfano kuna mtu akisikia maaskari wamekuja kumkamata anaweza kupanic vibaya mno, lakini kuna mwingine ambaye labda kwa njia moja ama nyingine anaweza asipanic kabisa kutokana na mazoea yake kwa maaskari,
Kujifunza kuzuia hamaki siyo kwenda kinyume na uumaji(nature)?
 
Back
Top Bottom