mimi nilisoma mzumbe Bsc.applied statistics,huwa tukifika mwaka wa pili tunakuwa na likizo ndefu ya miezi sita,kipindikile cha likizo nilitafuta field halmashauri ya wilaya niliyozaliwa ili kuhakikisha nasave pesa yangu ya field nifanyie kitu cha maendeleo.Nilifanikiwa kuanzisha saloon yangu pale wilayani kwangu,saloon ile inanipa 10,000 kila siku ya mungu kwahiyo nilipomaliza chuo kwakweli machungu ya kutoajiriwa sikuyaona mimi,mpaka baada ya miaka miwili nilipopaka kazi nikaendelea na maisha.Tatizo watoto wa siku hizi wanachezea hela unamkuta na lisimu la 1mil mara ana IPAD mazaga zaga kibao afu akimaliza chuo hana kazi analalamika tu mtaani,tumieni fedha mnazopata vizuri jamani usingojee mpaka umalize chuo ndo uanze kuhangaika hii ni sawa na mtu kufanya kazi akajisahau akaja kushtuka wakati wa kustaafu NI HATARI,PUNGUZENI STAREHE PUNGUZENI KWENDA KUPOTEZA MUDA MLIMANI CITY,PUNGUZENI POMBE,PUNGUZENI NGONO HAKUNA AJIRA SIKU HIZI NDUGU ZANGU AJIRA YAKO NI UBONGO WAKO.