Grace Products (Zoa Zoa) yaja na Dawa ya Meno

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
IMG_2187.JPG


Grace Products (Zoa Zoa) yaja na Dawa ya Meno

Ile kampuni maarufu Bongo kwa utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za vipodozi, maarufu kwa jina la Zoa Zoa imepiga hatua nyingine mbele kwa kutoa dawa ya Meno iitwayo Zoa Zoa ya Meno.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Grace Products, Dk. Elizabeth Nyamizi Kilili, alisema Zoa Zoa ya Meno imetengenezwa kwa kutumia mimea ya asili na kuhifadhiwa katika vifungashio vya kisasa, hivyo inafaa kutumiwa na Watanzania wa rika zote.

"Zipo 'Zoa Zoa ya Meno' kwa ajili ya watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano. Pia tumetoa Zoa Zoa ya Meno kwa umri wa kuanzia hapo na kuendelea.

"Zoa Zoa ya Meno ni nzuri kwa kuswakia maana mbali na kuua wadudu kinywani lakini pia inaacha kinywa katika harufu nzuri na kuyafanya meno kuwa meupe sana, hivyo kumfanya mtumiaji kuwa na mwonekano mzuri hasa akicheka," alisema Dk. Elizabeth.

Aidha, Mkurugenzi huyo alitoa somo la namna watumiaji wa dawa hiyo wanavyotakiwa kuitumia.

"Nataka niwaambie wateja kuwa, kwa matokeo mazuri, dawa hii ya meno inatakiwa kupigwa kinywani kila baada ya mlo mkuu, siyo kabla ya mlo. Wapo watu hupiga mswaki kabla ya mlo, hapana ni baada ya mlo, kwa siku mara tatu," alisema.

Zoa Zoa ya Meno inakuwa bidhaa ya kumi na mbili (12) kutolewa na kampuni hiyo iliyojizolea umaarufu mkubwa nchini.

Mwisho.
 
Sijui quality ya hiyo zoa zoa ya meno, ila nina uhakika zoa zoa si jina sawa kwa dawa ya meno. Zoa Zoa ilibidi ibaki kwenye dawa za chinusi tu na sio dawa ya meno.
 
Back
Top Bottom