Habari wakuu!
Kutokana na tetesi zilizokuwa zimesambazwa na gazeti la Mtanzani toleo la tarehe 13.02.2013 na tarehe 20 mwezi huu imethibitika Aljazeera Islamic Centre kilichopo Nansio kwenye kisiwa cha Ukerewe hakijishughulishi na ugaidi. Gazeti la Mtanzania liliandika upotoshaji kwamba chuo hicho kilichojengwa kwa hisani ya nchi za kiarabu kinatoa mafunzo ya kushambuliana kwa silaha aina ya jambia.
Pia gazeti liliandika kuwa chuo hicho kina ushirika na Alqueda na Al shabaab wanashiriki ugaidi. Mwenyekiti wa chuo hicho,Sheikh Ramadhan Salum Mazige ambaye pia ni diwani wa Nansio (CCM) amekanusha vikali habari hizo na kulitaka gazeti likanushe haraka kwani ni uchonganishi wa wazi.
Pia mmoja kati ya waanzilishi Mzee Jabil Katula amesema chuo hicho hakitoa mafunzo ya kigaidi na sheria zote zilifuatwa katika kuanzishwa kwake, serikali pia inatambua na DC na RC kwa miaka tofauti wamehudhuria mahafali...
(Source:Radio Times Fm)