Government to sue NorConsult

Mkuu Morani!
Kuna thread humu watu wanamlalamikia Mheshimiwa Rais kwa kuchelewa kumteua Waziri mpya mbadala wa Chenge! Hakuna mtu anayeulizia kuhusu makatibu wakuu wa hizi wizara. Kwa mtazamo wangu mimi, makatibu wakuu kama accounting officers wa wizara ni wa muhimu zaidi kuliko hawa wanasiasa kwa maana wao ni watendaji. Huu msistizo wetu wa kukazania siasa badala ya kuhakikisha kuwa tuna institutions na technocrats makini in place ndiyo unaochangia yote haya ya wakina NorConsult, CarlBro etc. Watendaji wangewajibika ipasavyo, tusingefika hapa. Na bila kuzistrengthen hizo institutions huu mwimbo tutakuwa tuna'rewind' kila siku!
 
FM, Mkuu kama tulivyoshasema earlier inaonekana hapa nchini watu hawajui majukumu na vikomo vya majukumu yao wakiwemo viongozi wetu!!!
 



Lakini kumbe ndio wao wanazichukua hizo fedha back halafu waja kutudai na interest kubwa....HYPOCRITES


Hivi kweli ulikuwa ukitegemea nani awekeze kwenye hiyo sekta ya migodi kama siyo taifa la watu wenye maadili kama Wanorwei? Pieter Botha na Makaburu wenzake wa enzi zile za apartheid? Au labda tumfufue Ian Smith na kumrudishia Rhodesia aitawale halafu tumruhusu awekeze kwenye huo mgodi wa Bulyanhulu? Kila kitu mnalalamika tu na kukosoa wakati mara nyingi ni Watanzania wenyewe wana-mess up halafu wanasingizia Wadhungu. Hao Wanorwei wamewafanyia na wanaedelea kuwafanyia mangapi mazuri? Nani alaumiwe kwa kuzagaa rushwa na urasimu serikalini na mfumo dhaifu wa kukusanya kodi Tanzania (itakuwaje kampuni ishindwe kulipa kodi kwa miaka mitano mfululizo bila ya TRA kugundua na kuchukua hatua?)
 
Mkuu, inaelekea uliondoka zamani! Konoike ni contractors na sio consultants. H.P.Gauff GmbH, Carl Bro, Sweco waliishaondoka zamani! Nadhani makampuni ya kigeni ya uhandisi yaliyobaki ni Howard Humphreys na Cowi Consult.

Mazingira ya kufanya kazi nyumbani kwa makampuni ya kigeni ni magumu mno tofauti na tunavyodhania.
Kwanza, registration fees na subscription fees za consultancy firms za kigeni katika professional bodies ni kubwa mno.
Pili, wataalamu wa kigeni individually nao wanatakiwa kuwa registered na wao nao fees zao ni za juu sana ukilinganisha na zile kwa raia wa Tanzania.
Tatu, makampuni mengi haya yalikuja ili kutekeleza miradi inayofadhiliwa na nchi zao. Kwa muelekeo wa ufadhili umebadilika na kuwa multi-lateral (EU, World Bank etc) inakuwa vigumu kwa nchi moja moja kupigia debe kampuni zake.
Nne, baada ya soko kufunguliwa pamekuwa na ushindani mkubwa kutoka makampuni ya nyumbani (TanConsult, M-Konsult etc) ambayo wakati mwingine yanashirikiana na makampuni mengine ya nje.
Tano, mdudu rushwa umeingia mno katika utoaji wa contracts, eneo ambalo haya makampuni mengine yanabanwa na sheria za kwao.

Ili kuepuka mengi ya haya , makampuni mengine yamekuwa localised. Hii inawapunguzia mzigo wa fees maana as a local company fees ni ndogo na vile vile kuruhusu washirika wao wabongo kucheza mchezo tunavyojua wenyewe. Mara nyingi u'foreign company' unakuwa token tu, ili kuwawezesha kupata miradi michache inayotoka kwao na kubakiza veneer ya kuwa bado ni clean.

Kuhusu wafanyakazi katika makampuni kama haya yanayofunga virago, naamini kuwa wanalipwa terminal benefits zao vizuri tu. Na tusisahau kuwa kama kuna ulaji mara nyingi hata wale watendaji wasimamizi nao wananufaika! Wafanyakazi wakisha jua bosi kuwa ni mwizi basi nao huwa hawasiti kujichukulia pensheni yao mapema.

haya yote niliyoyazungumzia hapa ni general na si lazima kuwa NorConsult ikawa na yenyewe imo katika kundi hili. Siwajui kwa hiyo siwezi kuwazungumzia. Kinachoniuma mimi ni kuwa hawa mabwana kama sikosei ndiyo waliyotayarisha Environmental Impact Assessment report kuhusu mradi wa Soda Ash lake natron na kudai kuwa flamingoes hawatadhurika! kama kweli ni wachafu, na makampuni kutoka India tunayajua, nina wasi wasi hasa na genuineness ya hiyo assessment. kwangu mimi, mengine yote tisa ila kwenye hili kama walihusika inabidi washughulikiwe KIKAMILIFU.

Amandla!


Sometimes some other people act as idiots in the sense that There isn't any place whatsoever where I claimed Konoike to be consultants, my words are as stated above. Let Fundi Mchundo ascertain and prove that H. P. Gauff GmbH, Carl Bro have left Tanzania? Can he precisely tell us when did they pack and go? I never mentioned Sweco did I?

I think Fundi can be really Mchundo as he wants us to believe that, what he wrote is correct can he prove us wrong that Norconsult AS were not linked directly with NORAD? Can he prove that H.P. Gauff with partnership with Biwater were not linked with the dubious case of water project in Dar?

In regard to Engineers registration to different bodies those fees shouldn't be a problem as a normal practice they can be offset when tendering for different projects. In actual fact the amounts are peanuts comparing to the values of works they charge.
 
Sometimes some other people act as idiots in the sense that There isn't any place whatsoever where I claimed Konoike to be consultants, my words are as stated above. Let Fundi Mchundo ascertain and prove that H. P. Gauff GmbH, Carl Bro have left Tanzania? Can he precisely tell us when did they pack and go? I never mentioned Sweco did I?

I think Fundi can be really Mchundo as he wants us to believe that, what he wrote is correct can he prove us wrong that Norconsult AS were not linked directly with NORAD? Can he prove that H.P. Gauff with partnership with Biwater were not linked with the dubious case of water project in Dar?

In regard to Engineers registration to different bodies those fees shouldn’t be a problem as a normal practice they can be offset when tendering for different projects. In actual fact the amounts are peanuts comparing to the values of works they charge.


Haya, Mkubwa!

Nishakuwa idiot sasa! Hii mada inazungumzia kashfa ya Norconsult ambayo ni consultancy firm. Kampuni zote ulizozitaja isipokuwa Konoike zilikuwa ni engineering consultancy firms. Ndiyo maana nika'point out' hii aberration na wala sio kwa nia ya kukuumbua mheshimiwa kama wewe.

H.P.Gauff GmbH iliyokuwa engineering consultancy firm yenye ofisi Oysterbay kama sikosei ilifunga ofisi zamani. CarlBro waliokuwa na ofisi Posta Mpya nao waliishafunga ofisi na kama alivyosema Morani75, kuna watu waliambulia vijigari. Sweco, ingawa hukuwataja, nao walikuwepo Tanzania nao wamefunga ofisi. Mimi niliingiza Sweco kama mfano wa makampuni yaliyokuwa yaki'operate' kutegemea miradi inayofadhiliwa na nchi zao. Hao H.P.Gauff unaowazungumzia kuwa waliingia ubia na City water sio lazima kuwa walioperate kutoka Tanzania maana kufunga ofisi Tanzania hakuna maana kuwa ndiyo wameacha kufanya biashara au kuwa hawataweza kurudi tena katika wakati watakaoona kuwa una muafaka kwao. Morani75 amegusia hili kuwa CarlBro kupitia ofisi yao iliyoko Uganda wameanza tena kujipenyeza Tanzania. Hii hata hivyo haiondoi ukweli kuwa walifunga ofisi kitambo. Kama wewe unajua vinginevyo basi na iwe hivyo maana njia wala haja ya kukuthibitishia sina.Hivi,Mkuu, kweli unategemea nikutolee ushahidi gani kwenye world wide web? Hizi enzi za Photoshop. Kama unataka kuamini haya, kama hautaki, ewala vile vile.

Kwenye hilo la consultancy fee sina cha kukujibu maana mwenzangu kama consultant uliyebobea bila shaka unajua kama fees wanazodaiwa Foreign Consultancy firms ni tenable au la. Kwa mtazamo wangu, ambao nakiri kuwa ni finyu maana sijawahi kuwa consultant kama mwenzangu, mzigo huu ni mkubwa hasa ukiangalia kazi nyingi zinatolewa kwa competitive tendering ambako wanapambana na wakina TanConsult na M-Konsult. Tena kwa mtazamo wangu wa kifundi mchundo, ni aghalabu hizi international firms kutumia mapato kutoka branch moja kubeba nyingine. Kila branch inatakiwa ijitegemee na kupeleka faida makao makuu. Ikiwa gharama za kufanya biashara zikiwa kubwa Tanzania kuliko Uganda, hawatasita kuhamisha ofisi zao Uganda. Lakini tena inawezekana kabisa kama unavyosema hizi ni peanuts kwao kwa hiyo hawaoni tatizo kubeba ofisi zisizo na kazi (kazi nyingi walizokuwa nazo zilikuwa ni vipolo toka wakati ule wa neema wa monopoly.).

Mwisho, naomba siku nyingine utambue udhaifu wangu katika kuelewa hiyo lugha ya kisomi uliyotumia. Naomba unisamehe ninapokuwa nimeshindwa kukuelewa maana msamiati unaotumia is very difficult, I say, na umenipita kimo, mimi maimuna idiot Fundi wa Mchundo!
 
I think Fundi can be really Mchundo as he wants us to believe that, what he wrote is correct can he prove us wrong that Norconsult AS were not linked directly with NORAD?


Mkuu Dua,
Nilikuwa najaribu kuielewa pointi yako hapa! Hivi ni uhusiano gani kati ya Norad na NorConsult unaotaka mimi nithibitishe kuwa haukuweko. Norad kama mteja wa NorConsult au Norad kama shareholder wa NorConsult? Halafu baada ya kufanya hivi, itathibitishaje kuwa niliyoandika ni uongo? Mimi nilisema mashirika haya mageni mwanzoni yalikuwa yanapata upendeleo kwenye miradi inayofadhiliwa na nchi zao. Kwa mtazamo huu basi miradi iliyokuwa ikifadhiliwa na ufalme wa Norway kupitia shirika lake ya maendeleo la Norad mara nyingi ilikuwa inasimamiwa na makampuni kutoka Nordic Countries, NorConsult, Norplan, CarlBro, CowiConsult n.k. Sasa kipi unachopingana nacho, Mkuu Msomi?
 
Hivi unapoongelea kampuni kuondoka zamani una maana gani? Unafahamu kwamba kampuni inaweza kukaa domant kwa miaka kadhaa wakati jina lake limechafuliwa au kukosa kazi? H.P. Gauff bado wapo kwenye ile skendo ya mradi wa maji walipoungana na Biwater sasa hii ni ya zamani kweli?

Howard Humphreys kwa mfano walikuwa domant kwa miaka kadhaa kabla ya kuibuka tena. Anyways sina sababu ya malumbano ambayo siyo ya kumkoma nyani giladi. Hawa mafedhuli ni lazima washitakiwe na serikali ya CCM chini ya JK vinginevyo hatuwezi kuwaelewa.
 
Kuna tendency ya watanzania kuamini kuwa watu au kampuni za kutoka nchi za Scandinavia ni waaminifu kwa sababu ya misaada wanayotupa. Lakini na wao wana wajanja wao ambao hawachelewi kunyonya au kupindisha sheria. Nakumbuka kuna waliowai kuwekeza katika nchi moja lakini kiwanda kilikuwa cha madawa ya kulevya.

..carlbro walishindwa kutoa rushwa ikabidi wafungashe virago!
 
Mkuu! Francis Kifukwe ameishakuwa mzungu? Painful as it is, lazima tukubali kuwa ni sisi, ambao tuko mbele kwenye hii michezo michafu.

Nadhani ni hii ndiyo kampuni iliyofanya Environmental Impact Assessment kwa mradi wa Soda Ash Ziwa Natron.kama ni hivyo, kuna haja ya ku'suspend' mradi na kufanya EIA nyingine. Mnyakyusa atakuwa ametutosa![/FONT]

..latest infor ni kwamba study nyingine inatakiwa kufanywa. mradi umesimamishwa mpaka hiyo study ifanyike!
 
Hivi unapoongelea kampuni kuondoka zamani una maana gani? Unafahamu kwamba kampuni inaweza kukaa domant kwa miaka kadhaa wakati jina lake limechafuliwa au kukosa kazi? H.P. Gauff bado wapo kwenye ile skendo ya mradi wa maji walipoungana na Biwater sasa hii ni ya zamani kweli?

Howard Humphreys kwa mfano walikuwa domant kwa miaka kadhaa kabla ya kuibuka tena. Anyways sina sababu ya malumbano ambayo siyo ya kumkoma nyani giladi. Hawa mafedhuli ni lazima washitakiwe na serikali ya CCM chini ya JK vinginevyo hatuwezi kuwaelewa.

Hatulumbani, Mkuu. Hapa ni mahali ambapo wenzetu ambao madarasa yalipanda mnatusaidia kutuelewesha sisi tuliokimbia umande.

Kuondoka ninakozungumzia mimi ni kufunga ofisi, kuachisha wafanyakazi, kuuza assets na kuacha kulipia kodi na malipo yote yanayowawezesha wao kufanya kazi Tanzania.

Howard Humphreys hawajawahi kuondoka wala kuwa dormant. Wamehusika kwenye mradi wa jengo la Barclays Bank n.k. Wamekuwa wana miradi nchi za nje waliyokuwa wakifanyia kutoka ofisi yao ya Tanzania. Hawajawahi kuwa dormant hawa mabwana. Wengine pengine, lakini si hawa!
 
From the Norwegian media.

Corruption investigation for Norconsult

http://www.aftenposten.no/english/local/article1790242.ece

The World Bank is investigating Norwegian consultancy Norconsult on suspicion of corruption in connection with an aid project in Tanzania.
Norconsult chief John Nyheim confirmed that he notified special economic crime division Økokrim about the situation on Tuesday.

According to financial daily Dagens Næringsliv, USD 146,500 (about NOK 900,000) has disappeared from a Tanzanian project account belonging to Norconsult.

Norconsult is taking part in a development project to improved the water supply to 2.5 million inhabitants of Tanzania's financial capital Dar es Salaam, in cooperation with two smaller companies from the Netherlands and Tanzania.

The project is financed by the World Bank. Last September bank representatives appeared at the project office in Dar es Salaam due to suspicions that the money's disappearance was linked to corruption.

The World Bank also sent people to Norconsult's head office in Sandvika outside of Oslo but found nothing. According to Dagens Næringsliv, this was because relevant documents had been shredded.

Norconsult board chairman Per Kristian Jacobsen told DN that certain employees had seen something that is likely corruption, without reporting it via official channels.

Neither Økokrim nor the World Bank would comment on the matter.
 
Bwana, Allah, Jah asifiwe! Asante Mkulu!

..but my opinion is that,kama mradi ni endelevu kimazingira,why not have soda ash from the area?.

..it seems,kuna watu wana band wagon makundi yasiyotaka tanzania ifaidike na soda ash hiyo kwa hoja ya mazingira endelevu.
 
..but my opinion is that,kama mradi ni endelevu kimazingira,why not have soda ash from the area?.

..it seems,kuna watu wana band wagon makundi yasiyotaka tanzania ifaidike na soda ash hiyo kwa hoja ya mazingira endelevu.

Si ku band wagon. Mradi kama huu umefanyika Kenya na umeleta madhara sana kwa flamingoes wa kule. Sehemu pekee DUNIANI ambako hawa ndege wanazaliana kwa wingi ni ziwa Natron. Sidhani kama ni busara ku'risk' kubadili mazingira yanayowafanya wazaliane hapo. Hiyo Soda Ash si ya kudumu. Kuna wakati itakwisha na wakina Tata watafungasha na kuhamia nchi nyingine na kutuachia sisi tupambane na uharibifu watakaouacha. Miaka iliyopita palikuwa na juhudi za kuanzisha mradi wa kulima prawns katika Rufiji Delta. Wakubwa wakaupigia debe sana bila kujali athari iliyotokea kwenye miradi kama hiyo nchi za wenzetu. Bahati wananchi walisimama kidete kuuzuia ama sivyo tusingekuwa na prawns tena Rufiji. Hii shortsightedness ndiyo inayotufanya tupuuzie uharibifu wa mazingira unaofanywa na wachimba madini kwa ungalia malipo ya hivi karibuni. Mimi ningeshauri kuwepo na vipengele katika hii mikataba ambayo itamlazimisha mwekezaji ahakikishe baada ya kuvuna alichokifuata anarudisha mazingira kama alivyoyakuta. Hawa wakina Tata watuhakikishie kuwa sio tu kiwanda chao hakitaleta madhara bali kuwa kama yakitokea watahakikisha kuwa flamingoes wanakuwepo hata kama ni kuhatamia mayai wenyewe!
 
Yanga mlie hela za dezo za kutoka kwa Kifukwe zimeisha!!!!

Kwi kwi kwi kwiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!

Connection ya JK na Kifukwe ni Yanga , ina maana sasa JK mchezo huu aliujua pia lakini akaamua kumeza kaa la ama ?
 
..fundi,

..sikusemi weye!

..halafu,hiyo ash itaisha pale ambapo olidonyo lengai itakuwa imefutika katika ardhi hii.
 
..fundi,

..sikusemi weye!

..halafu,hiyo ash itaisha pale ambapo olidonyo lengai itakuwa imefutika katika ardhi hii.

Najua hiyo Mkuu. Kuwa hunisemi mimi. Nakushukuru hata hivyo kwa kunifahamisha kuhusu link ya Oldonyo Lengai na Lake Natron. Sikujua hilo. Hata hivyo hii taarifa ndiyo imenizidisha woga. Hawa mabwana wanataka kujenga Coalburning power plant, reli na barabara kuja kwenye kiwanda. Bila shaka pataibuka ka township kuzunguka kiwanda. Haya yote, bila shaka, ni lazima itakuwa na impact kwenye makazi ya hao ndege. Lake Nakuru imeathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na pollution iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na makazi ya binadamu. Sasa kama kiwanda kitadunda mpaka Oldonyo Lengai itakapozimika, basi hakuna hope ya kureverse damage. Tumeliwa jumla! Na ni kweli NorConsult ndio waliotayarisha hiyo EIA. Ukijumlisha kuwa sidhani kuwa India kama China gives a hoot kuhusu future yetu, ipo kazi kweli kweli.
Mungu ainusuru nchi yetu.
Amandla!
 
Let Fundi Mchundo ascertain and prove that H. P. Gauff GmbH, Carl Bro have left Tanzania? Can he precisely tell us when did they pack and go? I never mentioned Sweco did I?

I think Fundi can be really Mchundo as he wants us to believe that, what he wrote is correct can he prove us wrong that
.

Fundi Mchundo is right in claiming that Carl Bro, H. P. Gauff and the rest have for some years now discontinued their operations in Tanzania. End of the story.

Furthermore, its the most natural thing to expect that Norconsult AS will work intimately with NORAD in many of their contracts. Nobody needs any "proof" of that (and as far as I can see, FM never claimed anything to the contrary let alone mention the nature of this relationship). Same applies to H.P. Gauff-Biwater partnership in the DAWASA project (a simple search on Google is enough to "prove" there was such partnership - but again FM did not dispute this fact either!)
 
This is what I wrote:

Why did Norconsult AS left in a hurry ......


1. Assumption moja ni kuwa wamevunja cardinal rule ya serikali yao (Sheria kwao ni msumeno na wanafahamu what will be next) hivyo faini yao itakuwa kubwa na huenda wakapoteza billions sio Tanzania bali kokote wanakofanya kazi ulimwenguni.

2. Ili kutokuipaka matope serikali yao wameona bora wakimbie, Je ubalozi wa Norway wanasemaje pale Dar? Je, walikuwa hawalijui hili?

3. Wasingeweza kujikosha kwa maajabu yao na ni lazima Norwegian Embassy know what is cooking (I presume)

4. Je serikali ya JK itachukua hatua gani kwa kampuni hii (Norconsult AS ambayo kutokana na vitendo vyake inakubali kuvunja sheria) na zile ambazo hazikusajiliwa kihalali?



Je, Kampuni zingine kama Konoike, Cowiconsult, H. P. Gauff GmbH, Carbro na nyinginezo hawana matatizo kama yaliyowakumba Norconsult?

Mchundo came with:

Mkuu, inaelekea uliondoka zamani! Konoike ni contractors na sio consultants. H.P.Gauff GmbH, Carl Bro, Sweco waliishaondoka zamani! Nadhani makampuni ya kigeni ya uhandisi yaliyobaki ni Howard Humphreys na Cowi Consult.


1. Now can you show me where I said Konoike are contractors or consultants? That’s yours to judge, more so a company can remain dormant for years without operations that can be a case for Car Bro and others. I know for sure the representative of H. P. Gauff is still in Tanzania, now somebody is trying his best with his idiotic mentality. (Nadhani?) we don’t dhania here, we right facts as they happen.

2. Now the issue has changed in regard to the consultants who still operate in Tanzania, while somebody anadhania. Well nobody disputes the fact that Norconsult left in a hurry let alone Why JK Government is silent about this issue.

Mchundo and Nyama Hatari know the fact that either they are in Mafisadi’s pay role to silent all those who questions the rotten eggs within the government system and think that by attacking me the matter will rest.

Of course one idiot can support another. And only idiots can't prove anything as they are. They become loafers. Tanzania is bigger than few FISADI’S here and there and people like Mchundo and Hatari. BTW Mchundo can be Hatari for your safety..

Nyani ataendelea kukomwa tu hapa hata mkiwapigia madebe hadi kwenye vilima vya Giladi. We want the government to take stern measures for all those involved in this saga.
 
Back
Top Bottom