Google yahamia India

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
๐—ฆ๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐˜‡๐—ฎ ๐—š๐—ผ๐—ผ๐—ด๐—น๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ฒ๐—ป๐—ด๐—ฒ๐—ป๐—ฒ๐˜‡๐˜„๐—ฎ ๐—œ๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐—ฎ

Makamu raisi wa kampuni ya Google Mr Rick Osterloh amesema kampuni yao ya Google muda sio mrefu wataweza kufungua kampuni ya kutengeneza simu na vifaa mbalimbali vya Google nchini India.

Amesema ni furaha kubwa sana ikiwa kampuni ya Google kuweza kufungua kiwanda cha kuzalisha bidhaa mbalimbali nchini India. Kuanzia mwaka 2024 kuanzia simu za Google pixel 8 na kuendelea baadhi zitakua zinatengenezwa toka india.

Tutarajie vifaa hivi kuanza kuundwa na kutumika mwaka 2024 ambapo baadhi ya simu, saa za Google zitakua zimeandikwa "Made in India".

images%20(1).jpg
 
nadhani ukiondoa kwamba kuna mkakati wa makampuni ya magaribi kuhamishia uzalishaji kutoka china kwenda india Apple na sasa google,lakini kuna kamkono ka pichai sundai hapo,ameamua ukapigiwe nyumbani.
 
India ina skilled cheap labour wengi ambao wanakubali mishahara midogo.

Kuzalishia USA ni expensive sana maana hakuna cheap labour.

Hata kina sisi weusi tukiumwa tunakimbilia india sababu ya bei ni nafuu
 
Miaka 5 ijayo makampuni mengi makubwa ya magharibi yatakua yana viwanda ama yatakua yanazalishia simu zao ama vifaa vyao vya kiteknolojia ya haki ya juu India.

India ina skilled labour force ya kutosha na cheap.
 
India wenyewe wanamkakati mkali wa kuwa super power ktk teknolojia. Wanafanya uwekezaji mkubwa sana ktk tech mfano quantum comp. Space exploration , Chip fubrication , AI na general manufacturing and engineeering.
India ina expert wengi sana dunia nzima wamesambaa zaidi ya waislael, wazungu na waafrika. Hata bongo expert wa IT wengi ni
Indians.
Shida kubwa ya India ni mfumo wa UNDUGUNIZATION, rushwa na caste system.
Vinginevyo India ingekuwa mbali sana. Ina world class scientist kwa kila nyanja, but they learn from Chinese.
 
nadhani ukiondoa kwamba kuna mkakati wa makampuni ya magaribi kuhamishia uzalishaji kutoka china kwenda india Apple na sasa google,lakini kuna kamkono ka pichai sundai hapo,ameamua ukapigiwe nyumbani.
Gharama pia, kipindi Apple wanaanza wafanyakazi foxconn China walikua wanalipwa chini ya $200. Sasa hivi Foxconn mishahara inafika hadi $1000 ama zaidi.

India wao ndio wanaanza rs 10,000 na baada ya Makato wanapata kama rs 8000 hivi, kama 250,000 ya Madafu.

So kampuni zinahamia India, na simu zinazotengenezwa India ubora ni Mdogo kuliko China.
 
Miaka 5 ijayo makampuni mengi makubwa ya magharibi yatakua yana viwanda ama yatakua yanazalishia simu zao ama vifaa vyao vya kiteknolojia ya haki ya juu India.

India ina skilled labour force ya kutosha na cheap.
Kwenye suala la kumtoa China katika uzalishaji bado sana. Maana China amejiwekeza sana na pia anatamani kushika soko la semiconductor manufacturers kwa kuivamia Taiwan na ndio maana Marekani haiwezi ruhusu hilo kutokea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom