ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
20/03/2013
Google wametoa app mpya inayojulikana kama Google Keep. App hiyo ni kwa ajili ya kuandikia vidokezo (notes) kwenye simu au tableti za Android. Hii itasaidia watumiaji wa OS hiyo kuandika vidokezo kwa haraka na ufanisi kwa ajili ya fikra ambazo wanahitaji kuzifanyia kazi baadae. App hii ina njia nyingi za kuandaa vidokezo.
Njia ya kwanzani kwa kuandika, pia unaweza kurekodi sauti au kupiga picha ya matokeo ambayo ungependa kuyahifadhi kwa njia hii. Watumiaji wa app hii wataweza kubadili rangi ya vidokezo vyao kwa ajili ya kutenganisha aina ya vidokezo, mathalan vidokezo vya kikazi viwe na rangi moja, vidokezo vya masuala ya kifamilia viwe na rangi nyingine au kwa namna yoyote atayopenda mtumiaji.
App hiyo pia inaruhusu kutengeneza vidokezo vya aina ya orodha ya vitu, kwa ajili ya shughuli kama vile ununuzi wa bidhaa nyingi kwa pamoja, na pia unapotumia njia ya kurekodi, Google keep huandika maandishi ya maneno unayoyarekodi, lakini kama tunavyojua hii huwa inawezekana iwapo tu unatumia lugha zinazotambuliwa na OS hiyo kama vile Kiingereza.
App hiyo imetulazimu kui-install kwa kutumia kompyuta, kwa sababu ambazo tumeshindwa kuzielewa app hiyo bado ilikuwa haionekani kwenye Play Store ya simu na tablet, japokuwa Google wameshaitoa rasmi. Hivyo tulilazimika kutumia njia ya mzunguko ya kufanya cloud installation kwa kutumia Play Store ya kompyuta.
App hii huhifadhi vidokezo vyote kwenye cloud hivyo unapotaka kuvisoma kupitia kompyuta unatumia anuani yahttp://drive.google.com/keep, hii maana yake ni kwamba vidokezo utakavyoandika kwa kutumia keep ya kompyuta moja kwa moja vitakuwepo kwenye simu bila ya kuvihamisha, ili mradi uwe unatumia account ya google ile ile baina ya kompyuta na simu au tableti.
Google wamechelewa mno kutoa app rasmi ya OS yenyewe yenye kufanya shughuli hii tofauti na iOS ambayo ina app ya Notes tangu toleo la kwanza la OS hiyo. Hata hivyo ni faraja kubwa kwa watumiaji wa Android kwani bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa, ingawa zipo apps nyingi tu kwenye Play Store zenye kufanya shughuli hii, ni vyema app iwe sehemu ya app rasmi za Google kwa vile app za Google wenywe hupata muendelezo wa uhakika na kila muda unavyopita inaendelea kuboreshwa kwa haraka ukilinganisha na apps za developers binafsi.
Kwa watumiaji wa Android Jelly Bean 2.2 wataweza kuwa na widget ya app hiyo kwenye lockscreen ambapo matoleo ya nyuma ya Android ambazo sio Jelly Bean 2.2 watakosa uwepo wa widget hii, ingawa watumiaji wa Android Ice Cream Sandwich na Jelly Bean 2.1 wataweza kutumia widget ya kawaida.
Chanzo: http://www.gajetek.com/2013/03/google-watoa-app-ya-videkezo.html