Google Kutoa Kompyuta ya Miwani Mwaka Huu

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159

​

Google ni ulimwengu wa uvumbuzi wa bidhaa na majaribio ya teknolojia, katika baadhi ya mawazo na uvumbuzi ambao Google wanaendelea kufanyia kazi kuna mambo ambayo sio ya kufirika, gari inayojiendesha na kompyuta ya kuvaa kama miwani ni miongoni mwa teknolojia hizo, kwa mtazamo wa haraka unaweza kudhani kuwa itachukua miaka zaidi ya 10 Google kuweza kuziuza bidhaa hizo kwa watu wa kawaida.

​
Ukweli ni kwamba Google imeshatangaza kuwa Google Glass itaanza kuuzwa mwaka huu wa 2013. Google Glass ni kompyuta ambayo huvaliwa kama miwani na ina uwezo na matumizi mbali mbali kama vile kurekodi video na kupiga picha. Katika ongezo jipya la Google Glass ni kwamba kompyuta hiyo itaweza kutumia amri za sauti (voice command), kuanzisha amri ya sauti unatakiwa kuiambia miwani hiyo “OK Glass” na miwani itaanza kukusikiliza unataka ifanye nini kabla ya kuipa amri kama vile “record video”. Pia Google wameonyesha baadhi ya matumizi ya miwani hiyo ambayo ni ya kawaida kabisa mbali na yale ya kuchupa na parashuti kutoka kwenye ndege.

Chanzo na Makala kwa Ukamilifu:
http://www.gajetek.com/2013/02/google-kutoa-kompyuta-ya-miwani-mwaka.html#more
 
Wakitaka wani impress waje na miwani yenye choo kabisa.
 
Sayansi na teknolojia ndiyo hiyo Ndugu zanguni!

Tanzania yetu na miaka 51 ya uhuru!
 
Hawajatengeneza miwani yenye bastola?
Naitafuta sana iyo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
​

Google ni ulimwengu wa uvumbuzi wa bidhaa na majaribio ya teknolojia, katika baadhi ya mawazo na uvumbuzi ambao Google wanaendelea kufanyia kazi kuna mambo ambayo sio ya kufirika, gari inayojiendesha na kompyuta ya kuvaa kama miwani ni miongoni mwa teknolojia hizo, kwa mtazamo wa haraka unaweza kudhani kuwa itachukua miaka zaidi ya 10 Google kuweza kuziuza bidhaa hizo kwa watu wa kawaida.

​
Ukweli ni kwamba Google imeshatangaza kuwa Google Glass itaanza kuuzwa mwaka huu wa 2013. Google Glass ni kompyuta ambayo huvaliwa kama miwani na ina uwezo na matumizi mbali mbali kama vile kurekodi video na kupiga picha. Katika ongezo jipya la Google Glass ni kwamba kompyuta hiyo itaweza kutumia amri za sauti (voice command), kuanzisha amri ya sauti unatakiwa kuiambia miwani hiyo “OK Glass” na miwani itaanza kukusikiliza unataka ifanye nini kabla ya kuipa amri kama vile “record video”. Pia Google wameonyesha baadhi ya matumizi ya miwani hiyo ambayo ni ya kawaida kabisa mbali na yale ya kuchupa na parashuti kutoka kwenye ndege.

Chanzo na Makala kwa Ukamilifu:
http://www.gajetek.com/2013/02/google-kutoa-kompyuta-ya-miwani-mwaka.html#more

Duh!!
nimeipenda hii

Sent from my SGH-I897 using Tapatalk 2
 
Baadaye tutakuja kusikia miwani hiyo ina madhara, inasababisha saratani ya macho, au inatia upofu!
 
unaweza uakonekanaa chizi mttaani unapita unaongea mwenyewe `ok glass start recording for 5 minutes` stop it mara inastack haijastop unabaki stop it stop it i said stoooop it cant you hear me soooooooooooooooooooooop!!!!
 
waliipigia promo sana hii sijui mwaka jana ile au juzi, ikifika bongo nambie ili nimnunulie mwanangu azame nayo kwenye pepa yake akifika form 4 asije taga mayai buree
 
Ilikuwa mwaka jana morphine kwenye Developers Conference Google I/O walipotoa Nexus 7 na Nexus Q iliyofeli (mpaka sasa)
 
Last edited by a moderator:
Ilikuwa mwaka jana morphine kwenye Developers Conference Google I/O walipotoa Nexus 7 na Nexus Q iliyofeli (mpaka sasa)

kumbee ahsante sana kwa taarifa kamili mdau.

natilia shaka waeza kuta ilifanikiwa ila NECTA wakabana ili watoto wetu wasije wakadesa nazo class room. Hakuna ticha atastukia km sio miwani ya macho
 
Back
Top Bottom