Apple kuja na miwani ya kisasa kuleta ushindani na Meta

Apple kuja na miwani ya kisasa kuleta ushindani na Meta

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,359
Reaction score
2,787
1_20250529_073547_0000.png

Apple iko kwenye mpango wa mwisho wa kuleta miwani ya kisasa "Smart Glasses" ambayo itaweza kuleta ushindani na miwani bora kabisa ya Ray - Ban Toka Meta.

Kulingana na Ripoti ya Bloomberg chips iliyopo ndani itakua kama ile chip ambayo apple wanatumia kwenye bidhaa ya Apple Watch,

2_20250529_073547_0001.png

lakini cha kuvutia zaidi ni kuhusu Miwani hiyo kuwa na "Multiple Camera" yenye kutoa picha bora.

Apple inatarajia kuachia miwani hiyo ambayo itakua na Teknolojia ya AI mwishoni mwa mwaka 2026.

3_20250529_073547_0002.png

💡 CHAKUVUTIA ZAIDI:
👓 Miwani Inakuja ikiwa na kamera ndani yake
🎤 Ina microphone ambayo Utaweza kuzungumza
🔊 Speaker nzuri zenye kutoa sauti bomba wakati unasikiliza au kuzungumza na mtu.

4_20250529_073547_0003.png

⚡ Utakua na uwezo wa kupiga simu kupitia miwani, ku control Audio mbalimbali, live translation wakati unazungumza na mtu toka lugha moja kwenda nyingine.

⚡ Kutakua na Navigation yenye kukuongoza kupitia sauti ya Siri Voice commands nk. Miwani inatarajia kuleta ushindani na Meta Ray - Ban smart glasses ubora wa hali ya juu.

Je Utaweza kuinunua ? Tuachie maoni yako ??
 
samahani, naomba nivuruge uzi kidogo kwa vile mimi na teknolojia ni sifuri.
kwahio ukitembea huku unachati kwenye miwani kwa kutumia macho huwezi pata ajali barabarani?
 
Na mimi nauliza unakuwa unachatije? au ukiclick macho ndo herufi zinajiandika, hautopata adha ya kugonga watu na vitu?.
 
Apple wanajua ku-market sana. Meta Orion by far ndo glasses ambazo binafsi naona zipo more suited kuendana na maisha ya users wengi.
 
Hii itatusaidia kujibu na maswali kwenye mitihani kwa kutumua AI.
Hakuna ku fail interview.
 
samahani, naomba nivuruge uzi kidogo kwa vile mimi na teknolojia ni sifuri.
kwahio ukitembea huku unachati kwenye miwani kwa kutumia macho huwezi pata ajali barabarani?
Angalia muvi ya ya Spiderman Far from home na muvi zote za Iron man hayo yote ndio yalianza kuonyeshwa huko. Utaona hizo miwani zinatumikaje. Utakua unaongea na AI kisha yenyewe ndo inafanya kazi
 
Angalia muvi ya ya Spiderman Far from home na muvi zote za Iron man hayo yote ndio yalianza kuonyeshwa huko. Utaona hizo miwani zinatumikaje. Utakua unaongea na AI kisha yenyewe ndo inafanya kazi
AI yenyewe unaiambia call my wife, inasema tall knife, as long as lahaja yetu ya kimakonde ipo available sijui tufanyeje.
 
Samsung nao wameungana na Google kuleta Android Glasses.
 
Huku kwenye bixby ya samsung huwa najionea maajabu, unampa amri badala atii anakwambia sijui umetamka vitu gani.
Lugha Yetu kuna baadhi ya maneno Hawajaweka kwenye mfumo ili yaweze kutambuliwa hapo ndo ilibidi wizara ya habari mawasiliano na Teknolojia iweze kuongeza baadhi ya misamiati kwenye mifumo ya AI ili kutambuliwa zaidi maana system nyingi zinajua kiswahili kikuu kiko kenya sio Tz
 
Kweli kabisa mkuu, ila hata kikristo ukiongea kwa lafudhi yetu AI inagoma kunasa, au tuongeeje? sasa si itakuwa kituko mbele za watu.
 
Back
Top Bottom