Tatizo mnaongea kitaalamu sana wakuu, Sisi wengine tusio na utaalam tunapata shida kweli
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu kama una idea kidogo na mambo ya uchumi benki kuu ndio inasimamia mambo yote ya fedha kwenye nchi, huu mfumo ni centralised.
Kutokana na madhaifu ya mifumo ambayo ni centralised watu wakaamua kutengeneza mifumo ya hela ambayo sio centralized. Mfano ni hizi cryptocurrency kama bitcoin.
Hizi bitcoin zenyewe zinatumia sana resource za computer hasa cpu na gpu. Matumizi makubwa yapo kwenye mambo mawili.
1. Kuzipata hizo hela za bitcoin kwa kufanya mahesabu makubwa
2. Kusimamia mzunguko wa hela baina ya watu na watu
Sababu ya uhitaji huo mkubwa wa computing power ulisababisha hadi bei ya graphics card kupanda sana.
Kila penye hela hapakosi wahalifu, hivyo kukatokea watu ambao wao hawatumii computer zao kutafuta hizo coin bali wanatumia computer za wenzao.
1. Unafungua website fulani computer inakuwa slow kumbe kwenye ile website kuna script ya kuchimba hizo coins mfano thepiratebay
2. Unadownload software kumbe ndani ina malware anaechimba hizo coins.
Tena siku hizi kuna malware wapo smart wanatumia cpu/gpu asilimia 30 mpaka 50, hivyo usipokuwa mjanja unaweza kuishi nae miaka kibao usijue.