Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 21,247
- 36,300
Habari za mwisho wa mwezi mabibi na mabwana.
Kuna taarifa za msiba wa jamaa zimenifikia zikanipa tafakuri ya maisha. 🤔🤔🤔
Pindi tunapoondokewa na wapendwa wetu tunapatwa na huzuni sana. Tukitamani warudi tuendelee kuwa nao karibu hata kama tulikuwa hatuwasaidii au hawatusaidii kwenye maisha.
Wengi hutumia huu msemo pale wanapoondokewa na wapendwa wao.
Gone Too Soon.
Huu msemo yafaa/inafaa utumike kwa marehemu aliye na rika gani?
Namaanisha uishie kwa watoto hadi miaka 18 pale wanapofariki?
Uendelee hadi kwa vijana wa miaka 30 au anayefiwa na mzazi wa miaka 60 nae aseme mzazi wake ameenda mapema?
Ni yupi aliyeondokewa na mpendwa wake akasema gone at a right time? Au gone too late?
How does it sound, umefiwa na mke/mume wa miaka 70 halafu useme gone too late, we're suppose to go te years ago...😁😁😁
It's a joke right? No one says that in public but deep in people's hearts they say it and some we see through their actions.
Kimjazacho mtu, ndicho kimtokacho.
Well bado unabaki kuwa msemo wa lugha ya kimalkia sijajua kama una maana zaidi ya kulalamika mpendwa amewahi kuondoka kabla ya muda, ilifaa aendelee kuishi.
Kwa lugha mojawapo ya mkoa wetu pendwa wa Tanga, kwenye msiba huwa wanalia.
Kaita Mgima mgima. wakimaanisha kaondoka mzima mzima yaani na nguvu zake.
Kiafrika nimekuwa nikiaminishwa wazee ndo wanatakiwa wafe wazikwe na watoto wao na si wazazi kuzika watoto wao.
Inaumaaa, kuna bibi mmoja alizaa watoto 5 au 6 sikumbuki vizuri.
Hadi dakika hii tunapoongea amezika watoto wake wote na yeye amebaki mzee mwenye nguvu zake.
Ila huzuni aliyonayo moyoni mwake, anaijua yeye na Mungu wake.
Waswahili wanasema usithubutu kukutwa.
Pole kwa wote walioondokewa na wapendwa wao wiki hii na mwisho huu wa mwezi.
Alamsiki bin tafakuri za Bi Kasinde.