VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Kila linalopangwa kuelekea ushindi wa kishindo linakwenda ipasavyo. Michoro isiyo na kihoro inachorwa na kuchoreka. Vyombo vya habari vimeshakamatika. Vimekuwa wachoraji bora kabisa wa taswira chanya ya CCM kwa wananchi. Wananchi hawatashangaa kuona CCM ikiibuka kidedea. Watawashangaa wapinzani wetu watakaobishia matokeo. Maandalizi yanakwenda vizuri.
Mnaweza kubeza sisi kubeba wananchi kwenye malori wakati wa mikutano yetu. Mnaweza kubeza barua za kuandaa wahudhuriaji wa mikutano ya wagombea wetu hasa wa Urais. Mnaweza kubeza hata matumizi ya mabavu kuwalazimisha wanafunzi,walimu na wafanyakazi wengine kuhudhuria mikutano ya kampeni. Lakini, sisi tunajua utamu wake. Wananchi wanaona luningani, kusoma magazetini na kusikia redioni kuwa tunakubalika.
Mtawaponda TWAWEZA,REDET na hata SYNOVATE, lakini sisi tutakuwa tumepiga hatua ya kutosha. Siasa ni maigizo, ulaghai na utapeli pale inapolazimu. Na CCM ndicho Chuo kikuu cha mambo hayo miaka na miaka. Hakuna zaidi yetu. Sisi tuna uzoevu na mambo hayo ya kisiasa. Wananchi wakishauwa na michoro ya kukubalika kwetu machoni mwao, mioyoni mwao na akilini mwao, mbinu za kufunga goli la mkono zitatumika bila bughudha. Kitaeleweka tu.
Tuoneni hamnazo tu. Mtatuelewa Oktoba 25. CCM mbele kwa mbele!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam