CHADEMA Arusha. Kuna nyakati historia huwaita watu wake si kwa maneno, bali kwa dhamira. Jumamosi tarehe 24/01/2026, Tengeru Arusha haitakuwa tu mahali pa mazishi ya Mzee Edwin Mtei, itakuwa mahali pa kuhoji dhamiri zetu kama wanachama wa CHADEMA.
Mzee Mtei na wenzake hawakuanzisha CHADEMA kwa ajili ya madaraka, bali kwa ajili ya haki na heshima ya utu wa Mtanzania. Pamoja kuwa niko nje ya nchi kwa masuala ya kifamilia, lakini dhamira yangu hainipi nafasi ya kunyamaza. Natoa wito kwa wanachama wote wa CHADEMA hususani Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini kusimama upande wa historia kwa kujitokeza kwa wingi sana Tengeru kutoa heshima ya mwisho kwa Mzee Edwin Mtei, muasisi wa CHADEMA. Mzee Edwin Mtei anastahili heshima kubwa, si kwa maneno, bali kwa matendo.