Godfather kawaharibia Yamoto Band Video

Godfather kawaharibia Yamoto Band Video

Atlantis

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2015
Posts
383
Reaction score
514
Sijui lakini kwa upande wangu naona kama hii video storyline yake haina pirpose vile, coz ukicheki unaona kama wazazi wanardi home wanakuta nyumba iko hovyo kutokana na nahisi ni watoto wao kufanya party fulani hivi so wazazi hao naona wanaishia kushangaa tu na watu waliofanya party hiyo hapo kwenye nyumba yao wakiwa bado wamelala na hawajielewi.

whats funny is, hakuna confrontation ya wazazi hao dhidi ya uharibifu uliofanywa na vijana hao, so storyline kama imeishia kati hivi.

Click here to watch the video

Ni mtazamo wangu tu
 
Wamekariri kila kitu kwa Gofather.
He's saturated.
 
maudhui ya wimbo yanaongelea shangwe za kawaida zinazo fanywa na watoto wa kitaa uswahilini za tanzania(dizaini ya singeri na kigodoro),lakini kinacho onekana ni shangwe zinazo fanywa na watoto wa kishua.mambo ya house party si jambo la kawaida kwa mitaa kama ya manzese,tandale,tandika,kigogo,mwananyamala,mbagara,nk.
 
Now Justin Campos ndo habari ya mujini!
 
Halooooow ngoja nimuite chige atuambie
 
Last edited by a moderator:
maudhui ya wimbo yanaongelea shangwe za kawaida zinazo fanywa na watoto wa kitaa uswahilini za tanzania(dizaini ya singeri na kigodoro),lakini kinacho onekana ni shangwe zinazo fanywa na watoto wa kishua.mambo ya house party si jambo la kawaida kwa mitaa kama ya manzese,tandale,tandika,kigogo,mwananyamala,mbagara,nk.

asante mkuu kula tano za nguvu....
umetishaa
 
Umuhimu wa Godfather ni kwa channels zilizo base South Afika kama MTV
wanam favour video zake...so msanii anapata airtime zaidi
 
Alichokiongea the big boss ndiyo dhana sahihi zaidi,,,wameamua kusacrifice maudhui na idea ya audio na kufanya video na godfather kwa ajili ya kufanya vizuri kimataifa,,airtime mtv,channel o and the like
 
Halooooow ngoja nimuite chige atuambie
Mkuu Shark, thanx kwa kunikaribisha kwenye mjadala! Hii video nimejaribu kuifungua mara mbili, lakini window inakuwa blocked.

Hata hivyo, nikiangalia maoni ya watu naona wame-base kwenye story line! Na kwa sisi, ukisia story line tunamaanisha video iandane na maudhui ya wimbo kama unavyotafsiri movie script into images! Hata kama video nyingi zinakuwa na story line lakini sio LAZIMA... na hata ukiangalia video za mbele, no one care about story line! Music video is all about visual creative art! Sasa kama lyrics zinasema kwa mfano "baby unaniumiza, nakukimbiza najikwaa... nainuka nazidi kukukimbilia...!" halafu tena na wewe unatuletea video inatuonesha mtu anamkimbiza demu, anajikwaa, anainuka anaanza tena kumkimbiza...!" eti unataka kutafsiri maudhui ya wimbo... where's visual creative art hapo?

Anyway, nisiseme sana manake sijaiangalia lakini ngoja nigusie hoja ya kadoda11. Audio ya ule wimbo nishaisikia lakini sioni kama inazungumzia house part ya kawaida ya Uswahilini; sana sana naona ni party iliyovamiwa na Waswazi! Chukulia verse ya kwanza kwa mfano, Dogo Aslee anazungumzia alivyo-struggle kufika kwenye party... manake ilibidi atembee kwa mguu! Mto wa Kiswazi hawezi kulalamika kutembea kutoka Temeke hadi Tandika au Buguruni hadi Kigogo... hii party watu waliifungia safari!!!! Kufika kwenye party, anakuta Wamasai na marungu... haya mambo ya Wamasai na marungu ni huko huko kwenu watoto wa kishua manake wanawalinda... huku kwetu wanakuwa na dawa za asili! Kuna mchizi kuingia kwenye party analazimika kuruka ukuta...! Huku kwetu na mambo ya ukuta wapi na wapi? Huku kwetu ukipata matofali, unaangalia kama kuna kinafasi kimebaki, kama kipo unaongeza kabanda hata kama ni kadogo unajua utapata mtu wa kuongeza hela ya mboga, na kama kanafasi hakuna kabisa, unayangiza sokoni! Party imejaa madaktari kibao... huku kwetu kabla hujaenda chuo unaulizwa "huo udaktari unasomea miaka mingapi" In short, tunaukwepa manake hatuwezi kukaa tena miaka 6 masomoni wakati ndugu wanatuangalia tuwasaidie; kwahiyo ukiona party ina madaktari wengi namna hiyo basi ni ya kwa akina kadoda11 na mpwa warumi... sijui kafia wapi huyu na yeye!

Sasa description ya huo wimbo hata kama party yenyewe itakuwa ni ya uswazi kama anavyosema Mkuu Kadoda, basi ni Uswazi kwenye familia bora! Si unajua watoto wa kishua pamoja na mbwembwe zao zote, baba zao wakistaafu wanakuwa hawana ubavu wa kujenga Masaki au Mbezi Beach na badala yake wanakuja huku huku mitaani kwetu... wanawahamisha wazazi wetu na kutuletea utamaduni wao wa kizungu!!!!
 
Last edited by a moderator:
Alichokiongea the big boss ndiyo dhana sahihi zaidi,,,wameamua kusacrifice maudhui na idea ya audio na kufanya video na godfather kwa ajili ya kufanya vizuri kimataifa,,airtime mtv,channel o and the like

wenyewe huwa wanasema almradi godfather ana connection nzuri na watu wa chennel O,trace tv na mtv base,video atakayo-shoot,hata kama haita reflect kinachoimbwa,si neno.

ila mimi naona hili haliko sawa.godfather alichangia kwa kiasi fulani kuharibu video ya mwana daresalaam ya ali kiba.kuna haja ya management za wanamziki wa bongofleva kuwapa misimamo ma-director wa nje juu ya nyimbo wanazo zifanyia shooting.

chige
asante kwa ufafanuzi.
 
wenyewe huwa wanasema almradi godfather ana connection nzuri na watu wa chennel O,trace tv na mtv base,video atakayo-shoot,hata kama haita reflect kinachoimbwa,si neno.

ila mimi naona hili haliko sawa.godfather alichangia kwa kiasi fulani kuharibu video ya mwana daresalaam ya ali kiba.kuna haja ya management za wanamziki wa bongofleva kuwapa misimamo ma-director wa nje juu ya nyimbo wanazo zifanyia shooting.

chige
asante kwa ufafanuzi.
kadoda11,
Kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe kuhusu video ya Kiba... tatizo hatufahamu what's behind the scene kuhusu ile project wise. Mosi, Mwana Dar es salaam haikuwa na tatizo in terms of technical wise lakini haikubeba ladha ya kisanaa! What's behind the scene kuna mambo mawili... mosi, budget! Je, Kiba aliwasilisha bajeti ya kutosha! Nilisoma kitabu kimoja How to Make $10,000 movie... hii sio kibongo bongo, bali huko huko ambako movie ya $10 million inaitwa low budget movie! Tukiachana na hilo la bajeti ambalo producer/director watakutengenezea basing on your budget, issue nyingine kwa Kiba ni ikiwa Mwana waliitafsiri vizuri into English kiasi cha Godfather na timu yake kufahamu ni nini hasa kinatakiwa! But in addition, chukulia video za Diamond kwa mfano! Hata kabla hajaanza kufanya kazi na Godfather, tangu hapo video zake za tangu zamani zilikuwa na ladha fulani ya kisanaa, drama za hapa na pale! Kutokana na hilo na kama nipo sahii, basi inawezekana hata hizi kazi anazofanya kwa Godfather, mwenyewe kama mwenyewe (Diamond) na timu yake inaelekea wanachangia sana katika ku-develop concepts na kuchangia ideas na kuleta ladha ya kisanaa... na hili linaweza kuonekana hata kwenye video ya Nana ambayo ame-modify tu na ku-expand idea ya Moyo Wangu! Je, Kiba na yeye alifanya jitihada za kuchangia ku-develop concept na kuchangia idea kwenye ngoma yake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom