Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Kamanda hawa watu sio kama wanajitoa bali wanajaribu kuwashauri nini cha kufanya.
Ukweli ni kwamba mazingira ya kudai haki ni magumu sana na wananchi wanaelewa hivyo kwani ingawa tuko katika mfumo wa vyama vingi, lakini kiuhalisia bado tunaishi katika taratibu na sheria za mfumo wa chama kimoja.
Kwa mfano, hata ndani ya Bunge Spika bado anatokana na chama cha siasa na bahati mbaya aliepo sasa anatoka chama tawala hivyo hata mkipeleka hoja zenu za kudai Katiba mpya au kudai Tume Huru bado mnaweza kukabiliwa na changamoto lakini ni bora mkajribu ili mpate uhalali wa kufanya maamuzi mengine.
Raisi anaetokana na chama cha siasa bado anateua watu wanaopaswa kusimama haki kwa vyama vyote kama vile Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Msajili wa Vyama vya Siasa,Katibu wa Bunge,Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria,n.k
Tatizo lingine ni nyinyi kuwa wachache ndani ya Bunge hivyo inakuwa vigumu kufanya mabadiliko yoyote bila support ya walio wengi.
Kwakweli mazingira ni magumu sana na watu wanaelewa hivyo ndio maana mnaona watu wameanza kushawishi vinginevyo.
Vile vile tambueni humu mitandaoni si wote wanasema mjipange ni wana-CHADEMA bali baadhi ni vijana kutoka upande wa pili wanaotaka kutumia matokeo ya uchaguzi huu kuivuruga CHADEMA kwa kujidai nao ni mashabiki wa CHADEMA