Godbless Lema nadhani hujaelewa ni nini wananchi wanamanisha wanaposema mjipange

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,985
144,312


Kamanda hawa watu sio kama wanajitoa bali wanajaribu kuwashauri nini cha kufanya.

Ukweli ni kwamba mazingira ya kudai haki ni magumu sana na wananchi wanaelewa hivyo kwani ingawa tuko katika mfumo wa vyama vingi, lakini kiuhalisia bado tunaishi katika taratibu na sheria za mfumo wa chama kimoja.

Kwa mfano, hata ndani ya Bunge Spika bado anatokana na chama cha siasa na bahati mbaya aliepo sasa anatoka chama tawala hivyo hata mkipeleka hoja zenu za kudai Katiba mpya au kudai Tume Huru bado mnaweza kukabiliwa na changamoto lakini ni bora mkajribu ili mpate uhalali wa kufanya maamuzi mengine.

Raisi anaetokana na chama cha siasa bado anateua watu wanaopaswa kusimama haki kwa vyama vyote kama vile Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Msajili wa Vyama vya Siasa,Katibu wa Bunge,Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria,n.k

Tatizo lingine ni nyinyi kuwa wachache ndani ya Bunge hivyo inakuwa vigumu kufanya mabadiliko yoyote bila support ya walio wengi.

Kwakweli mazingira ni magumu sana na watu wanaelewa hivyo ndio maana mnaona watu wameanza kushawishi vinginevyo.

Vile vile tambueni humu mitandaoni si wote wanasema mjipange ni wana-CHADEMA bali baadhi ni vijana kutoka upande wa pili wanaotaka kutumia matokeo ya uchaguzi huu kuivuruga CHADEMA kwa kujidai nao ni mashabiki wa CHADEMA
 
Mtatapatapa sana
Lakini mwambieni Mugabe wa Bongo (Mbowe)
Chama kimemshinda
Uwezo wake uliishia 2010
Hana jipya aachie chama wenye uwezo
Sikuzote Akili ndogo haiwezi ongoza Akili kubwa
Wacheni kuficha kubarini kukosolewa
Mwambieni Chama sio Kabila kuongoza kitemi
apeleke utemi wake Uchagani.
 
Kibaya serikali iliyopo imeshasema kuwa katiba mpya na tume huru sio vipaumbele. Kilichoonekana juzi ukijumlisha na kiwango cha usaliti kinachochochewa na vyuma kukaza inakuwa ngumu sana kuitegemea CHADEMA pekee kubadilisha mawazo haya ya serikali.

Nadhani diplomasia ya kimataifa ndio pekee inaweza kutunusuru kwa kuunganisha na nguvu kiasi zilizopo!
 
Kibaya serikali iliyopo imeshasema kuwa katiba mpya na tume huru sio vipaumbele. Kilichoonekana juzi ukijumlisha na kiwango cha usaliti kinachochochewa na vyuma kukaza inakuwa ngumu sana kuitegemea CHADEMA pekee kubadilisha mawazo haya ya serikali.
Nadhani diplomasia ya kimataifa ndio pekee inaweza kutunusuru kwa kuunganisha na nguvu kiasi zilizopo!
Katiba duniani kote haijawahi kuletwa na watawala
 
Chadema ni chama imara la msingi kupitia ukawa lazima vyama vyote viungane kudai tume uhuru then katiba mpya ya wananchi iboreshwe na kumalizia mchakato wa ile katiba ya jaji warioba iwe na meno zaidi na bora zaidi.

Ili kufuta hiki kivuli cha tume inayoteuliwa na rais, na kufikia hatua ya kukiri waziwazi eti mkurugenzi nisikie unatamtangaza mpinzani kashinda wakati serikali inakuhudumia....

Tume iliyipo siyo huru na imethibitika waziwazi kwa chaguzi za karibuni hasa uchaguzi wa madiwani juzi Arusha ni vitu vya ajabu walifanya nje ya sayari ya tatu.

Na Mungu azidi kuwalaani vizazi vyao vya kwanza hadi vya nne wale wote waliyopanga na kutekeleza hujuma iliyofanyika uchaguzi wa madiwani na chaguzi zote za Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mtatapatapa sana
Lakini mwambieni Mugabe wa Bongo (Mbowe)
Chama kimemshinda
Uwezo wake uliishia 2010
Hana jipya aachie chama wenye uwezo
Sikuzote Akili ndogo haiwezi ongoza Akili kubwa
Wacheni kuficha kubarini kukosolewa
Mwambieni Chama sio Kabila kuongoza kitemi
apeleke utemi wake Uchagani.
Hivi una Cheo au mzazi wako ana wadhifa au unalipwa na CCM? maana huwez shabikia CCM kama katika hivi vitatu hunufaiki navyo
 
Katiba duniani kote haijawahi kuletwa na watawala
Ndio maana wengine wanawacheka cdm huku wakisahau uhuru tunaouongelea leo wameupigia sana kelele hapo kabla na hata ufisadi wote unaoshughulikuwa (????!!!) waliupigia sana kelele wakati unatengenezwa!
 
Wanaowashauri Chadema wajipange leo wanaonekana machizi. Haya machizi tupo wengi.

Chadema mjipange. Kama toka 1995 mpaka leo hamjafahamu chama kilichoko madarakani kina dola kweli hamjajipanga.

Kama toka 1995 hamjafahamu viongozi na watu wenu mashuhuri kama kina Dr Amani Kaborou wanaweza Ku cross floor kweli mnatakiwa mjipange.

Kama mlikuwa mnafikiri kwenda mahakamani kwa makundi kumtetetea mtuhumiwa wa kosa la uvutaji bangi kutawaletea wapiga kura wavuta bangi wengi mjipange, wavuta bangi huwa hawapigi kura.

Kama mlidhani wabunge wenu wakitoa matusi ya nguoni bungeni basi watanzania watawaona mashujaa wa matusi kweli mkajipange.

Kumuacha na kutomuwajibisha mwenyekiti wenu kwa tuhuma za rushwa na ufuska hata kumtaka tu atoe maelezo ya kueleweka kwa nini alipewa mamilioni na Kinana, Rostam na Mkono watu wa ccm na kama kweli Joyce Mukya in mkewe wa pili na ndio sifa ya kupewa ubunge viti maalum, kweli mjipange.

Chadema mjipange, mjipange. Pamoja na kuwa na ufahamu kuwa 'power' hamuwezi kukabidhiwa kirahisi kama unavyoagiza sahani ya ugali hotelini, lakini pia mjitathmini ninyi wenyewe je mnatosha? Bado mnabeba ndoto na mategemeo ya watanzania wanyonge? Ninyi bado ni watetezi wa wanyonge au watetezi wa makahaba matajiri wavuta bangi, wauza madawa ya kulevya, madhulumati waliowaonea watanzania wanyonge miaka yote hiyo iliyopita?

Chadema ijipange, chadema sio wananchi. Chadema wale wenye mikono yao inayofika kwenye posho za ruzuku mnazopokea. Chadema wale wanaoweza kubadilishia gia angani ndio mjipange.

Hata kuitwa chagadema nako mnahitaji mkufanyie tathmini na kweli mjipange.

Chadema kweli jipangeni na muhimu ni kujua hasa ni jinsi gani ya kujipanga.
 
Ndio maana wengine wanawacheka cdm huku wakisahau uhuru tunaouongelea leo wameupigia sana kelele hapo kabla na hata ufisadi wote unaoshughulikuwa (????!!!) waliupigia sana kelele wakati unatengenezwa!
Ila watu wanazo hoja.. Cdm ile iliyokuwa inaweza kupiga kelele Sio cdm hii ya sasa
 
Mtatapatapa sana
Lakini mwambieni Mugabe wa Bongo (Mbowe)
Chama kimemshinda
Uwezo wake uliishia 2010
Hana jipya aachie chama wenye uwezo
Sikuzote Akili ndogo haiwezi ongoza Akili kubwa
Wacheni kuficha kubarini kukosolewa
Mwambieni Chama sio Kabila kuongoza kitemi
apeleke utemi wake Uchagani.
Polisi anaweza kukufikisha stendi lakini hatokulipia nauli .
 
Kuna kazi kubwa sana ya kufanya kulikomboa taifa hili. Na watu shupavu wanahitajika sio lelemama. Siamini kama mtu hanufaiki na CCM atakua punguani akianza kukisifia. CDM ijirekebishe mapungufu yake na ioneshe nia ya dhati kutaka kushika nchi na sio kuwaza ruzuku nina imani wananchi wengi wanaiunga mkono
 
sometimes tuwe tunakubali ukweli....kwa sasa tumepoteza moral authority kwenye mambo mengi

Pia ni shida kwa mwananchi wa kawaida kututofautisha na CCM
Ukweli upi hapo ? Kama hii yako ni hoja kwanini waliagiza mauaji kwenye uchaguzi wa kata tu ? Hizo porojo za akina polepole zisikupotoshe , njama zote walizopanga hadharani hakuna asiyezijua .

Huwezi kuwa na uchaguzi wa aina hii na ukauita uchaguzi , vita katika nchi nyingi huanzishwa na ujinga kama huu , hawa wakubwa wanaoagiza haya hukimbia nchi maana nauli wanazo.

Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayeunga mkono yaliyotendwa kwenye uchaguzi huu .
 
Back
Top Bottom