Godbless Lema kunyang'anywa jimbo la Arusha

Godbless Lema kunyang'anywa jimbo la Arusha

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2013
Posts
7,877
Reaction score
5,694
KUMEKUCHA! Duru za kisiasa katika Jimbo la Arusha Mjini zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mbunge anayeliongoza jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Jonathan Lema kuangushwa katika uchaguzi mkuu ujao baada ya mfanyabiashara mkubwa (bilionea) mmoja (jina kapuni) jijini hapa, kudaiwa kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili kuumaliza ufalme wa Lema

Wapiga kura mbalimbali wa jimbo hilo waliozungumza na Uwazi Mizengwe, wamebainisha hilo. Kuna wachache ambao wamesema Lema hawezi kung’oka lakini wengi wao wamesema atang’oka kutokana na nguvu kubwa ya ushawishi aliyonayo mfanyabiashara huyo ambaye atagombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Lema hawezi kurudi bungeni tena maana jamaa (bilionea) kajipanga sana na ukizingatia ni mzawa wa Mtaa wa National Milling ambaye amewekeza katika biashara mbalimbali, anakubalika katika jamii kwani anajitoa sana, hakika atamng’oa nakuhakikishia,” alisema mkazi mmoja wa Arusha kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.

Mkazi mwingine wa jimbo hilo ambaye pia hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema licha ya kufanikiwa kutimiza baadhi ya ahadi zake lakini Lema ameshindwa kutekeleza ahadi nyingi likiwemo suala la jengo la Machinga Complex ambalo aliahidi kulifanikisha.
“Kuna mambo mengi tu ya msingi ambayo wapiga kura tumeona hajakamilisha hususan suala la Machinga Complex, bado ni kitendawili, sidhani kama atapenya uchaguzi ujao na ukizingatia kuna mfanyabiashara maarufu ambaye tayari ameonesha nia ya dhati ya kutaka kumaliza kero nyingi za Arusha Mjini,” alisema mkazi huyo.

Kuhusu madai ya kutokamilisha ahadi ya kujenga jengo la Machinga Complex, kwa nyakati tofauti Lema amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akisema ameshindwa kuikamilisha ahadi hiyo kwa kile alichodai ni kuwekewa mizengwe na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
 

Attachments

  • 1426859733553.jpg
    1426859733553.jpg
    34.9 KB · Views: 2,284
Mnaota kabla hamjalala, ni aina mpya ya muujiza.
 
Amka uendelee na mishe zako, au lala tena uote ndoto zingine!
 
Mimi huwa nawashangaaga nyie binadam mnaposema jamaa kajipanga mno...ooh mara anahela sana...inamaana atahonga hizo hela kwa wapiga kura wote arusha?Hizo ni hela zakuhonga ili jina lake lipitishwe agombee..lazma tutofautishe hayo mambo mawili..kuhonga ili agombee na kuhonga wapiga kura....na kibaya zaidi wapiga kura wa Arusha hawaongeki sasa.!!!
 
Mnapendaga saana kujipa moyo ccm,endeleeni Tu lakini.Hata angekuja Obama kugombea Arusha asingepata mbele ya Lema
 
Nasema hiv Lema Mbunge wangu Asiporud Bungen baada ya Uchaguz wa OCTOBER naham Arusha!
 
Yaani habari ya kwenye magazeti ya UDAKU ndiyo unaleta hapa kwa GT forum. Kweli JF siku hizi ni balaa. Kesho tutaletewa story ya ile mimba ya Zari kuwa imechomoka...just watch.
 
nilivoanza kusoma story yako nilidhani una kitu kipya cha kuueleza umma kumbe ni pumba....eti bilionea anagombea kupitia ccm.....tumesema Arusha mkiweka ccm na bundi tunapigia kura bundi...
huyo bilionea apelekee familia yake hela zake.
 
Yaani habari ya kwenye magazeti ya UDAKU ndiyo unaleta hapa kwa GT forum. Kweli JF siku hizi ni balaa. Kesho tutaletewa story ya ile mimba ya Zari kuwa imechomoka...just watch.

Nenda jukwaa la celebrity utakuta au we mgeni hapa?
 
Back
Top Bottom