Godbless Lema kuiteka Dodoma leo

Godbless Lema kuiteka Dodoma leo

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mjumbe wa Kamati kuu Chadema Godbless Lema leo anatarajiwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Wajenzi mjini Dodoma saa 8 mchana leo.

Kamanda Lema ambaye pia ni mbunge wa Arusha mjini anatarajiwa kuelezea mambo kadhaa kuhusiana na wizi wa Tegeta Escrow,maazimio ya bunge na utekelezaji wake.

Mjumbe huyo wa kamati Kuu anatarajiwa pia kuwashukuru wananchi kwa kuiunga mkono Ukawa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Akihojiwa Lema amesema anakwenda kuzungumza mambo makubwa ya nchi na kuwataka wakazi wa Dodoma wakae tayari kusikia mambo ambayo huenda hawajayasikia.

Godbless Lema alikuwa amemtaka aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo kujiuzulu kabla ya kikao cha bunge kinachoanza kesho vinginevyo angemtoa kwa nguvu bungeni.

Lema anatarajiwa kufuatana na Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje na wabunge wengine kadhaa wakiwemo viongozi wa Kanda wa Chadema na mkoa wa Dodoma.
 
Huyo Lema hana akili ya kueleza mambo ya Escrow ,labda awaeleze kuhusu wizi wa magari. Lema aage kabisa huko bungeni Dodoma harudi tena Arusha tumemchoka hakuna chochote alichofanya Arusha zaidi ya kurusha nabomu soweto, vurugu na maandamano

Kweli Arusha ni kubwa!? Hata wewe wa Nduruma kumbe mpo Arusha!? hah hah hah....
 
Alikuwa ametulia kama maji ya mtungi, bado hatujasahau kilichomkuta Gerezani tutamvua nguo tena asituchezee Machalii wa ARUSHA.
 
lumumba wakiona mada imeandikwa lema watajaa hapa sasa hivi kwa matusi wakiongozwa na msalani
 
Tumewashika lumumba bora mbwa koko mzururaji kuliko mtembea patupu mitandaoni
 
Alikuwa ametulia kama maji ya mtungi, bado hatujasahau kilichomkuta Gerezani tutamvua nguo tena asituchezee Machalii wa ARUSHA.

Hopeless zero brain.Huna hata aibu
 
Lema Kiboko kweli....Yaan Muhongo aliposikia Lema Atamtoa kwa nguvu bungeni akaona Booora aibu kuliko fedheha.......
 
Lema Kiboko kweli....Yaan Muhongo aliposikia Lema Atamtoa kwa nguvu bungeni akaona Booora aibu kuliko fedheha.......

Ndio vilaza wa Chadema mnavyojidanganya hivyo. Nyie ndio mnasubiri Chadema ichukue nchi mlipwe mishahara bila kufanya kazi teh teh teh teh
 
Ndio vilaza wa Chadema mnavyojidanganya hivyo. Nyie ndio mnasubiri Chadema ichukue nchi mlipwe mishahara bila kufanya kazi teh teh teh teh

Una kichaaa wewe,,Hakuna hata kamanda mmoja wa CHADEMA asiyepata hela yake kwa jasho....tunaona Uchungu na ugumu wa maisha unaosababishwa na nyie mafisadi....Mwisho wenu October....CCM wezi wakubwa wa ESCROW.
 
Kweli Arusha ni kubwa!? Hata wewe wa Nduruma kumbe mpo Arusha!? hah hah hah....

Ametufanya jasiri mpaka tumechukua halmashauri ya jiji. Awamu hii tutamsaidia kurejesha mali za jiji zilizoporwa na ccm na mafisadi km uwanja wa sheikh Amri Abeid, uwanja wa Szimio Sakina na uwanja wa hospitali Njiro kontena.
 
Back
Top Bottom