Godbless Lema katika kashfa ya kuiua CHADEMA Arusha

mama porojo, hufiki popote mwishi hata wanokulipa posho watachoka, kwa taarifa yako humu Jf walikuwepo akina MS, lakini walishindwa baada ya kuona kuwa wanalipwa posho za bure.

walioandaa hiyo document ni masalia. umeingia choo cha kike
 
Mm ni mmoja wa wanachadema ambaye nilimpa kura Lema mwaka 2010, lakini kiukweli mwenendo wa Lema ni wa kutia mashaka sana, Hana maadili ya kiuongozi wala mipango thabiti ya kumkomboa mwana arusha, ndio maana hili swali halijibiwi "LEMA KAFANYA NINI ARUSHA TOKA ACHAGULIWE?" kuna siku alipaki lile benz lake old model pale Pembeni ya NMB Clock tower Arusha halafu akafungua mlango mmoja akaweka mguu kwenye Dashboard na kuanza kusoma Gazeti! dah! Mbunge???
 

Barua hiyo inashindwa kuaminika kweli kama imetoka kwa makada wa CHADEMA na uongozi wa Arusha maana hakuna logo ya Chama. Lakini kama majina hayo yanayoonekana ni ya wanachama kweli wa CHADEMA jibu lako hili limekuwa jepesi mno. Ifike mahali tusilewe unazi unless kama na wewe una malengo ya kuiua CHADEMA.

Watu tumepiga kelele hapa jamvini mara nyingi. Hivi inakuaje Chama kinachangisha mamilioni ya fedha za Wananchi bila mrejesho wowote? Hizi fedha kamati kuu ya CHADEMA ina taarifa nazo? Zinaratibiwa vipi? Kuna tatizo gani slaa au akina John Mnyika kuja public na kueleza mapato na matumizi ya M4C? Kama hilo tu linashindikana itakuaje kwa kodi za wananchi baada ya hiyo 2015? Let us be serious jamani.

Hata kama kilicholetwa na MAMA POROJO ni porojo kama lilivyo jina lake lakini ukiunganisha dots na michango iliyokwishapitiswa bila mrejsho unafanya watu makini waanze kupata wasiwasi.
 
Last edited by a moderator:

Porojo nyingi za nini? Kama unajua kweli kinachoendela jibu swali rahisi tu. Je, Dr. Slaa amepokea barua hii iliyoandikwa kamati kuu ya Chadema?
 
Is this how you inspire confidence? With brouhahas and hullaballoo?
 

Kamanda siwezi kuchotwa akili kirahisi hasa kwa wanajf ninao wajua vizuri.Hoja ya kujenga taasisi badala ya watu ipo pale pale na ninavyoijua Arusha( nimeishi kule nusu ya umri wangu) ni wapinzani toka zamani lakini wanapenda watu wa aina fulani na wenye misimamo haswa.

Lema anapendwa sana ARUSHA lakini tusijisahau na kuwekeza kwake badala ya Chama!!! Mkuu Ngongo najua anasimama wapi nafahamu vizuri sana!
 
Namwona Invisible yupo, ngoja niende zangu nisije pigwa ban
 
Mkuu Munyangaa utashanga hautojiwa sana sana utaambulia matusi na kupachikwa majina ya ajabu ajabu mara msalia mara msaliti hapa bado hawajachukua nchi hawataki kujibu hoja bali viroja ha ha ha ha.

[1] Tunataka kujua kwanini kiwanja cha Hospitali kimeandikwa jina lake na mke wake ?

[2] Tunataka kujua michango ya M4C anayokusanya inafanyiwa audit mara kwa mara ,Tayari kuna fedha zimeshatafunwa ingawa zipo juhudi kubwa za kuficha huu wizi kwania ya kutowakatisha tamaa wachangiaji

[3] Tunakataa uhuni wa Lema kutumia jina la wajane kwaajili ya kujipatia trecta kwa faida zake.

[4] Tunataka wasomi wajitokeze kugombea nafasi katika ngazi mbali mbali badala ya kuwapiga vita kwa hoja hafifu kwamba ni wanausalama wa taifa.

[5] Tunataka michango kwaajili ya waanga wa mauaji ya Arusha ziwafikie walengwa bila kupungua hata ndururu.

Naomba kuwasilisha.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu,
Wewe umesema.

Tatizo kuu hapa jf kumetokea kuwa na kikundi cha watu ambao wamelishwa dictatorial propaganda ambazo zinawafanya baadhi ya viongozi kuwa kama hawagusiki katika lolote lile huku viongozi wengine wakiwa kama punchbag.

Mambo kama haya yanachangia kuleta matabaka na Unfairness kwa viongozi na wanachama matokeo yake ndiyo kuwepo kwa makundi ndani ya chama.

Tabia ya ukweli ni kugusa kila mtu na kama unafichwa basi utaendelea kujitanua mpaka hapo utakapojipambanua.
 
chadema kwanini haipendi kukosolewa??
Hii inaleta ukakasi etii,,
 
katika haya malalamiko baadhi yaliyoorodheshwa ni kama ifuatavyo, kwa wale ambao hawawezi kufungua hili file.

1.Lema anavunja katiba ya chama kwa kuwafukuza uanachama baadhi ya makamanda na viongozi ambao walikuwa ni nguzo kwa ustawi wa chama bila kufuata kanuni na taratibu za chama mfano kamanda MBOYA alifukuzwa kwa maagizo ya wadhifa wake akiwa mbunge, pia katibu wa wilaya KREDO ADAM alivuliwa ukatibu wa wilaya kwa maelekezo ya Lema. CHAMA KICHUNGUZE
 



(1)kwan lema ana mke??
 
kwa wakati huu ambao barua imetolewa inaonyesha ni mkakati wa waliokataliwa kuonyesha kuwa malalamiko yapo dhidi ya wengine ila hayashughulikiwi. kwa mwendo huu CDM mnachelewa kuchukua hatua dhidi ya wanaokisaliti chama pendwa. hivi huyu lema anaetuhumiwa ndio yule yule aliyefunga barabara ya moshi arusha kwa masaa matano?
 

Kamanda BEN acha mahaba mkuu, be objective....utachekwa na watu na utapoteza heshima yako...soma kwa makini hoja zilizoainishwa na wana wa arusha dhidi ya lema kabla hujarukia keybord na kupost.
 
Mods,

Msaada sisi wenye simu za mchina tuweze japo kusoma.
Mkuu Ritz,nimeamini hiki chama kina wenyewe Lema anapiga watu jukwaani halafu uongozi,wakombozi na wanajiita makamanda ndio kwanza wanapiga makofi na vigelegele mkutanoni.
 
duh, hii ndo siasa, kusifiana na kushambuliana!
 
Mtu anapitishwa kugombea Ubunge bila kufaynika kura za maoni!!! Kweli wenzetu demokrasia mnaielewa tofauti sana...
 
Kamanda BEN acha mahaba mkuu, be objective....utachekwa na watu na utapoteza heshima yako...soma kwa makini hoja zilizoainishwa na wana wa arusha dhidi ya lema kabla hujarukia keybord na kupost.
Wala usihangaike nae huyo baada ya kuomba radhi amepewa probation ndio maana anatetea kila upuuzi anatumika kama kingamuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…