Godbless Lema hamia Dar es Saalam kwa muda

Godbless Lema hamia Dar es Saalam kwa muda

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,792
Reaction score
2,421
Unajua Namwona mwanasiasa huyu ni Chachu ya mabadiliko.

Kwa Arusha umeshafanikiwa kuinyoa CCM kwa zaidi ya 70%. Kwasababu nakubali sana Hotuba zako kwenye mikutano na mbinu za kueneza Chama kama cd na hotuba Zilizojaa hamasa ambazo zinauwezo wa kumbadili mnyonge kuwa mtu Jasili Sana na Anayejiamini nakushauri Sasa harakati Hizo Ziamishie Jiji la Dar es Salamu kwa siku kama 100 mfululizo. Muhakikishe chadema inaota mizizi huko. Ungana na wanasiasa vijana wanaopendwa Kama Mr II, Halima, Joseph Haure, Na wengine Wakongwe Kama Profesa safari na matangazo yenu yadokeze mada zitakazozungumziwa

Zingatia vitu viwili.


1. Lazma kuwe na elimu ya uraia ambayo raia wengi hawana wananchi wajue nchi ni yao na viongozi wako pale kutekeleza wananchi wanachotaka.
2. Vipato vya taifa, wizi ndani ya taifa, uwekezaji asa kwenye madini usio na tija, Manunuzi na bei za vitu kwa serikali. Mikataba kama ya tanesco inavyowatesa wananchi.

Naamini kitu kimoja Dar Ikibadilika niRAHISI TANZANIA YOTE KUIGA NA KUBADILIKA HATA KWA MKUMBO. Dar hupokea na kutoa zaidi ya watu laki 3 kwa siku

*please kama inawezekana uzi huu urudishwe kwenye jukwaa la siasa upate wachangiaji wanasiasa*
 
Kwa siasa za Lema atakuwa anapoteza muda wake bure.
 
Dar es Salaam sijui wamelaaniwa? Wako busy na vitu vingine. Alafu ndo jiji linaloongoza kwa uchafu, foleni, mgawo wa umeme, shida ya maji, Elimu duni (kasoro shule za private) na mengineyo. Lakini watu kama wamefumbwa macho
 
Tatizo watu wa Dar wengi wanajifanya busy halafu vilevile hawapendi vurugu
 
Kwa Arusha umeshafanikiwa kuinyoa CCM kwa zaidi ya 70%. Kwasababu nakubali sana Hotuba zako kwenye mikutano na mbinu za kueneza Chama kama cd na hotuba Zilizojaa hamasa ambazo zinauwezo wa kumbadili mnyonge kuwa mtu Jasili Naamini kitu kimoja Dar Ikibadilika niRAHISI TANZANIA YOTE KUIGA NA KUBADILIKA HATA KWA MKUMBO. Dar hupokea na kutoa zaidi ya watu laki 3 kwa siku
Nani anastahili pongezi za mafanikio ya CHADEMA mkoani Arusha? Samson Mwigamba ambaye alikuwa mwenyekiti wa CHMA wa mkoa aliyetengeneza mikakati ya ushindi wa CHAMA? Mwigamba ndiye aliyemuibua Godbless Lema na kumfanya mgombea kwa ticket ya Chama, na kumsadia kimkakati nyuma ya pazia. Mwigamba amekuwa na Chama muda mrefu zaidi na anawafahamu wanachama wengi zaidi na wanachama wanamfahamu Mwigamba vizuri kuliko Lema?? Nadhani Mwigamba anastahili pongezi kwa kuifikisha CHADEMA hapa ilipo.
 
Akaongoze Kimara, Dar watu hawatumii bange kufikiri wala gongo kuelewa,

Wapo lakini wa kuhisabika hao awatakao ama afananao akili.
 
Nani anastahili pongezi za mafanikio ya CHADEMA mkoani Arusha? Samson Mwigamba ambaye alikuwa mwenyekiti wa CHMA wa mkoa aliyetengeneza mikakati ya ushindi wa CHAMA? Mwigamba ndiye aliyemuibua Godbless Lema na kumfanya mgombea kwa ticket ya Chama, na kumsadia kimkakati nyuma ya pazia. Mwigamba amekuwa na Chama muda mrefu zaidi na anawafahamu wanachama wengi zaidi na wanachama wanamfahamu Mwigamba vizuri kuliko Lema?? Nadhani Mwigamba anastahili pongezi kwa kuifikisha CHADEMA hapa ilipo.

....tumeshatupa njee hatukai na vitu used!!!!
 
Akae ukouko magari ya watalii mengi mi nina kagari tena ka mkopo akikaiba ntakuwa mgeni wa nani mana jamaa anatisha
 
Lema kafanya nini Arusha?
Au kuweza kufanya mobilization ya wasio na uwezo wa kufanya reasoning ni mafanikio?
Dar hilo atashindwa,vichwa vingi vinahitaji manual operations,sio vya remote kama Arusha
Arusha ukiwa Kenya unaweza kuwapigia simu na kuwaeleza waandamane bila sababu na wakaandamana,wanaendeshwa na hisia zaidi ya akili kumkichwa!
 
Back
Top Bottom