Godbless Lema...Dakika za mwisho za Ubunge.

Wakimwengua itakuwa vizuri saaaana. Ili kampeni zianze tena, halafu CCM ishindwe kwa kishindo na kuzidi kuwashushia hadhi.
 
Wakubwa,
Baada ya kusoma habari hii nimejaribu kumpigia mtu fulani maarufu kwa masuala ya siasa na sheria, anasema hali ni ngumu kidogo kwa Lema...
Yeye anadai kuwa kwanza Lema alidanganya kuhusiana na Elimu yake, na mahakamani hilo lilidhihirika wazi!...Na alipobanwa juu ya hilo akasema kuwa alishaandika barua kwa katibu wa Bunge ili warekebishe kipengele hicho cha elimu kwenye taarifa zake za kibunge, ziendane na ukweli,..hivyo hapo pana substance kubwa ya kumuumiza!

Mkuu PJ,

Mimi nadhani hapa kuna vitu viwili umeyachanganya pamoja ambayo ni Matusi na Elimu ya Lema.
Kesi ya Msingi inahusu matusi. na kuhusu Uchaguzi, na kama Matusi yalitumika kuathiri matokeo ya uchaguzi, Mlalamikiwa namba moja alitakiwa awe Mgombea Mama Batilda, ambaye hata kujisumbua hakujisumbua. Vile vile katika ushahidi uliotolewa mahakamani hakuna ushahidi wa sauti uliowasilishwa mahakamani kuonyesha kwamba Lema kayatamka hayo maneno.
Kuhusu Elimu yake alieleza wazi kuwa there were typing errors, na ameijulisha ofisi ya bunge. hata hivyo kwani wasiwasi wa sheria upo wapi kuhusu elimu kuwa serious hivyo? kama tujuavyo sifa ya mgombea ubunge ni kwamba ni lazima awe mtanzania mwenye akili timamu, aliyetimiza umri wa miaka 21 na kuendelea. sijabahatika kusoma sehemu inayoelezea kuwa mgombea ubunge ni lazima awe amehitimu degree au elimu fulani.
 
  1. Katika Ushahidi uliotolewa mahakamani hakuna kielelezo kilichowasilishwa kwa hakimu kukazia ushahidi. Hakukuwa na ushahidi wa sauti wala wa maandishi zaidi ya bla bla nyingi.
  2. Sina kumbukumbu sahihi kama mbwembwe za uchaguzi zilishawahi kutengua matokeo ya uchaguzi.
  3. Batilda Buriani hajawahi kuhudhuria mahakamani kukazia ushahidi wa wapiga kura walioathirika kisaikolojia mpaka wakampigia Lema kura badala ya Batilda.

Nimesikitishwa sana na uwezo mdogo wa uwelewa wa kisheria aliouonesha Paka Jimmy kwenye topic hii, sina mengi ya kueleza uliyoyasema ndio ukweli wenyewe, siku ushaidi wa walalamikaji wanafunga ushahidi wao nakukumbuka vyema kwamba Jaji aliwauliza mbona shahidi muhimu ( Batilda Buriani ) katika kesi hii hamjamleta kutowa ushahidi wake! maana ni yeye ndiye alitukanwa!!....

Kesi hii haiitaji mtu kuwa na degree ya sheria kujuwa kwamba Lema alishashida hii kesi tangu siku ya kufunga ushahidi, ninachokiona hapa wapenzi wa CHADEMA mnaandaliwa kisaikolojia na hii big hoax ili Jaji akikubali kuingizwa mkenge na Magamba mpigwe goli la sudden Death.

Paka Jimmy kumbuka katika kesi ya msingi ya Lema hakuna swala la Elimu yake lilipohojiwa swala la Elimu lilikuwa katika mwenendo wa Kesi na si kesi ya msingi na ndio maana kama utakumbuka Kihiyo hakufunguliwa mashtaka ya kugushi vyeti kwa sababu Mahakama ilikuwa haijakaa kusikiliza kesi ya kughushi vyeti bali ilikaa kusikiliza kesi ya Uchaguzi wa Jimbo la Temeke.
 
Ushauri wangu,wasijaribu kutengua matokeo sababu uchaguzi ukirudiwa ccm ikashindwa hataweza kukubalika kwa asilimia kubwa tenda ktk uchaguzi mhimu sana 2015.
 
Inadaiwa kuwa Lema alitumia lugha ya matusi na ya kudhalilisha wakati wa kampeni, na ushahidi umeonyesha hivyo...dai kuu ni hilo
Huyo mama x mbunge enzi hizo hataki hata kuja kutoa ushahidi anasema yeye ni barozi hivyo hayo mambo ya ubunge wa Arusha hayamhusu!!!!! Hivyo hicho ni kiherehere cha wapambe wa CCM waliopewa fedha kwenda mahakamani kuleta mashitaka fake dhidi ya Mheshimiwa Lema!!!!

 
hakika hakuna watu wanaotoa matusi kama wa ccm iweje leo mtu hajatukana apatikane na hatia?siku zote haki haiwezi kuzikwa kamwe,na nguvu ya umma itaonyesha nguvu yake,kweli serikali ina hela za kuchezea kwenye chaguzi wakati wanajua hawatashinda.yetu macho wanajamii.
 
Baba,
Hukumu ya Lema imepata shinikizo kubwa sana kutoka kwa watu mbalimbali!
Kuna shinikizo toka kwa EL, serikali(kumbuka skendo bungeni ya Pinda na uwongo) na Bunge lenyewe, kuanzia spika na watu wa ccm.
Hizo ni ndoto zako kwani EL ni nani hasa mbona Arumeru hakufua dafu bado tuu una imani na umaarufu wa mwizi???? Tungoje hukumu itolewe lakini hakuna ground zozote za Lema kushindwa kesi, kwani hakuiba kura wala hakuna aina yoyote vurugu na incidence za kutengua ubunge wake!!!!!!!!!! Pole saana Lema atendelea kuwa Mbunge wa Arusha, ndoto zako hazina ukweli!!!!

 
Hizo ni ndoto zako kwani EL ni nani hasa mbona Arumeru hakufua dafu bado tuu una imani na umaarufu wa mwizi???? Tungoje hukumu itolewe lakini hakuna ground zozote za Lema kushindwa kesi, kwani hakuiba kura wala hakuna aina yoyote vurugu na incidence za kutengua ubunge wake!!!!!!!!!! Pole saana Lema atendelea kuwa Mbunge wa Arusha, ndoto zako hazina ukweli!!!!

Nina wasiwasi kuna mtu amehack ID ya Paka Jimmy leo.......sidhani kama Paka Jimmy is too low like today he shows!!.....
 
Kama Matusi wanayodai yalitukanwa kwenye kampeni, walitakiwa kupeleka malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi. cha ajabu hawakufanya hivyo. na kama hayo matusi yalitukanwa, na yakaweza kutengua matokeo ya uchaguzi, tutawaomba akina Musa Mkanga na wenzake kufungua kesi dhidi ya Lusinde, Mwigulu, Wassira na Mkapa kwa kutumia lugha ya matusi.
 
Nina wasiwasi kuna mtu amehack ID ya Paka Jimmy leo.......sidhani kama Paka Jimmy is too lowa like today he shows!!.....
Mkuu, jana nilipita mahala nikakuta watu wanakunywa Konyagi, mimi nilikuwa nakunywa soda ya passion, nikaathiriwa na harufu ya ile konyagi, nadhani imenipa maluweluwe hadi leo kudadadeki!
 
huyo Mbwiga ni Mzushi.. mimi sidhani kama kuna Muda wa Kudiscus Uzushi.. Usalama wa taifa Hakuna Hicho Unachokiongelea wewe .. Mkuu wa usalama unamjua wewe.. miwatu mingine kuzua na Kutunga..
 
Ni aibu na fedheha kwa watu wa Arusha kuongozwa na Mbunge ambaye ni MWONGO.

Mji umedorora kwa sababu tumemchagua mbunge mbumbumbu, asiye mwadilifu (ex-fugitive) na hana elimu hata ya kidato cha nne.

Kuvuliwa kwake ubunge na ikitokea akakatazwa kugombea tena ni jambo la faraja kwetu wana Arusha.

Tunaisubiri kwa hamu kesho 4/4/2012 tumwone kilaza akipigwa chini.
Mkuu si afadhali ya Mheshimiwa Lema je umeona CV ya Mheshimiwa Joseph Lusinde wa CCM??????
Hebu cheki CV yake hapa chini

EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
Mbigili Primary SchoolPrimary Education19801987PRIMARY
CCM College IhemiCertificate20072008CERTIFICATE


Source: Bunge

EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From DateTo Date
The Parliament of TanzaniaMember - Mtera Constituency20102015

POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
Chama Cha Mapinduzi, CCMSecretary - Tarime District20062010
Chama Cha Mapinduzi, CCMAssistant Secretary/Accountant20062007
CHADEMAMember - National Executive Board1995
Civic United Front, CUFSecretary - Kawe Constituency19921995
Chama Cha Mapinduzi, CCMSecretary



Source Bunge website



Nimejiuliza kwa watu kama hawa tutafika kweli





 
Kuruhusiwa au kutokuruhusiwa itategemeana na hukumu. Endapo gender based violence ikizihirika ni mpaka chaguzi tatu zipite.
 
Jamani mtaniua kwa Presha tarehe 5/4/2012 naona kama mwakani. Jembe la ukweli litolewe????!!!
 
Baba,
Hukumu ya Lema imepata shinikizo kubwa sana kutoka kwa watu mbalimbali!
Kuna shinikizo toka kwa EL, serikali(kumbuka skendo bungeni ya Pinda na uwongo) na Bunge lenyewe, kuanzia spika na watu wa ccm.

Acha utopian thinking.
tarehe 5 ni kesho kutwa na utaenda kuwalaumu hao wanasheria waliobebea kwa nini wanakudanganya hivi.
Baada ya kutoka mahakamani tutasherekea pale NMC kama kawaida CDM faraja tu.
 

Acha utopian thinking.
tarehe 5 ni kesho kutwa na utaenda kuwalaumu hao wanasheria waliobebea kwa nini wanakudanganya hivi.
Baada ya kutoka mahakamani tutasherekea pale NMC kama kawaida CDM faraja tu.

Na je mmeshapeleleza kama hao walalmikaji wana mali zisizohamishika ili kesi ikiisha tukamate mali zao kufidia gharama za kuendesha kesi alizoingia Lema? nadhani hii ndiyo njia sahihi ya kuwakomesha machakubimbi.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom