SI KWELI PreGE2025 Godbless Lema ametangaza kustaafu siasa

SI KWELI PreGE2025 Godbless Lema ametangaza kustaafu siasa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Barua inasambaa Facebook na WhatsApp.

LEMA.24JUL2025.jpg
LEMA24JUL2025.jpg
BARUALEMA24JUL2025.jpg
 
Tunachokijua
Godbless Lema awali aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Msajili wa vyama vya siasa, na kisha baadaye kuteuliwa tena kwa ajili ya kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.


Madai kuhusu Lema kustaafu siasa

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook kuanzia Julai 23 wamekuwa wakisambaza taaarifa iliyonukuliwa kutoka kwenye barua inayodaiwa kutolewa na Godbless Lema kuwa ametangaza kustaafu siasa.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani, barua iliyonukuliwa haijatolewa na Lema bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji.

Vilevile grafiki zilizotumika kunukuu na kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi kwani hazijachapishwa na Jambo TV na Mwananchi, bali wapotoshaji wametumia utambulisho wa vyanzo hivyo ili kusambaza taarifa potofu.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, Lema aliweka ujumbe uliowataka Mwananchi kujitenga dhidi ya utambulisho wao kutumiwa na wapotoshaji kusambaza taarifa isiyo ya kweli ambapo baadaye chombo hicho kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram walikanusha grafiki na kwamba hawahusiki nayo.​
Back
Top Bottom