Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,279
- 105,481
Uko vizuri sana mkuu! Nakuelewa!
Naomba msaada wako kwenye hili:
1. Tukiamua au kukubaliana kutumia FACTS kujadili uwepo au kutokuwepo kwa "MUNGU", Source/Origin ya izo FACTS ni ipi?! Tuna imani gani na iyo source/origin ya izo FACTS?? Namaanisha ivi...kama FACT ni "SAYARI KULIZUNGUKA JUA" Je, source/origin ya FACT hii unaiamini kiasi gani??!
Mimi hupenda kujadili mambo kwa kitu kinaitwa "immanent critique".
Immanent critique ni nini? Kwa kifupi, ni namna ya kuchambua hoja kwa kuanza kwa kutomkatalia anayekuhoji, unaaanza kwa kusema "hebu nichukulie kwamba upande wa pili uko sawa na mimi nimekosea, nianzie hapo, halafu nitake kukubaliana na upande wa pili kwa mawazo makunjufu kabisa, lakini, nisikubali kijinga tu, niulize maswali yangu yote mpaka niridhike"
Kihesabu hapondipo unaona habari za "let x =...", yani unapofanya "let x=..." unakuwa hujakubali "x=..." ila unaanza kutafuta jibukwa mfumohuo.
Tukirudi kwenye habari yako.
Umeeleza kuhusu facts. Kuongelea "facts" tu bila framework ni umasikini wa mawazo.Facts zinahitaji framework.
Kuna mfano mmoja wa injinia aliyepewa kazi ya kujenga daraja, akasema siwezi kujenga daraja.
Kwa nini? Akasema, kwa sababu sijaweza kuipata valie of pi in decimal nikaimaliza. Kama unaelewa pi, katika decimal ni irrational number ambayo as far as we can tell hai terminate.
Injinia akagoma kujenga daraja. Akasemaanaweza kujenga daraja halafu kikavunjika, hataki lawama.
Kumbe, kiukweli, value ya pi inayohitajika kujenga daraja inatakiwa kuwa na only four significant figures, huko mbele ni mbwembwe tu.
Ukianza ku question fact, bila kutoa framework, nitakwambia sawa, fact zote ni provisional, kwa sababu kwanza hatujakamilisha framework ya muda,kuna kesho, sasa kesho tukigundua tofauti fact zetu si tutazitupa?
Ukisom Godel's Incompleteness Theorems utaona hakuna fact isiyo provisional na isiyo relative na framework
Ukisom Einstein's Relativity utaona hakuna fact isiyo provisional na isiyo relative na framework
Ukisom Wave Particle duality utaona hakuna fact isiyo provisional na isiyo relative na framework
Ukisom Hegelian Dialectics utaona hakuna fact isiyo provisional na isiyo relative na framework
Ukisom Schrodinger's Cat's experiment utaona hakuna fact isiyo provisional na isiyo relative na framework
Ukisom double split experiment utaona hakuna fact isiyo provisional na isiyo relative na framework
Sasa unapouliza facts,unauliza kwa framework gani? Kwa epistemology gani? Kwa cosmogony gani?
Halafu, nikikwambia facts haziaminiki,tusiziamini, hilo halithibitishi Mungu yupo. In fact habari hizi zinaweza kukupeleka usiamini kwamba wewe mwenyewe upo, kwa sababu wewe mwenyewe unaamini upo kwa kutumia namna fulani ya facts.
Sasa kamawewe hupo, dunia haipo, habari nzima ya kwamba Mungu yupokwa kuwa kakuumba wewe na dunia inakosa msingi.
Utaona kwamba hata ukiishambulia fact na kuisambaratisha, hilo hali prove Mungu yupo, sanasana unaongeza ushahidi kwamba Mungu hayupo.
2. Tukiamua au kukubaliana kutumia LOGIC kujadili uwepo/kutokuwepo kwa "MUNGU". Nini itakua Standard Scale ya kui-qualify hio LOGIC as meaningful??! Kwasababu wote tunajua kwamba when it comes to LOGIC, everybody becomes a LABOUR to His/Her LOGIC (LOGIC becomes a master...the same applies to one's Opinion!). Kwa kusema hivi, nilikutana na Phylosophy ya Einstein, ambayo alitumia this equation (6-3=6) to logically argue in favour of his phyllaophy.!
Mimi nimetumia logical consistency na contradictions kutenga uongo na ukweli.
Hata uki discredit logic, hilohalithibitishi Mungu yupo! Unachotakiwa kufanya ni kuthibitisha Mungu yupo.
Uki discredit logic una establish chaos kwamba hakuna yeyote anayeweza kuthibitisha lolote kwa njia yoyote popote.
Hapo hujathibitisha Mungu yupo. Kinachotakiwa ni uthibitisho kwamba Mungu yupo.
I am doing this by examples to illustrate my concerns about GIVING much EMPHASIS on other people's opinions/logic, and FACTS generated and amplified by "People" to directly affect "Lifestyle"-Religion
Unaelewa kwamba hata wewe hapa umeandika mawazo yako kwa logic ya alphabet ya watu wengine mpaka nikakuelewa?
Mimi natumia logoical consistency na contradictions,na test vitu, sikubali tu.
Mpaka sasa naona logic ya alphabet, kwa kiasi fulani, inafaa kwa matumizi ya majadiliano, kwa sababu nimeitumia kuelewa unachouliza nikakujibu.
Kamaunasema tusitumie kitu chenye logic iliyowekwa na wengine, acha kutumia simu, acha kutumia computer, acha kutumia lugha, acha kutumia alphabet, anzisha kila kitu chako.
Utaweza?
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo kwa namna yoyote? Hata tukisema tusitumie logic kwa sababu logic haiaminiki?
Utawasiliana vipi nami hapa kuendeleza mjadala bila kutumia logic japo ya lugha na alphabet?