Glaser Hepatitis B Healthcare Initiatives

Glaser Hepatitis B Healthcare Initiatives

navah

Member
Joined
Feb 27, 2023
Posts
7
Reaction score
3
Guys iyo initiatives wana afa ajira vitengo tofauti lakini changamoto inakuja pale ambapo wanataka ufanye IQ Test ambayo pia ni Paid almost 55Usd na wanakupa link ufanye wapi? kweli hii sio scams?

gp.PNG
 
Guys iyo initiatives wana afa ajira vitengo tofauti lakini changamoto inakuja pale ambapo wanataka ufanye IQ Test ambayo pia ni Paid almost 55Usd na wanakupa link ufanye wapi? kweli hii sio scams?
Ili ujuwe kwamba unaibiwa unapaswa kuibiwa kwanza?!
 
Yaani me mwenyewe nashindwa kuwaelewa
wezi hakuna hata siku moja kazi halali itakutaka ulipie chochote kabla ya kuipata fungueni maskio yenu mnaenda kupigwa mchana kweupeee
 
ila wanakuambia pia ruksa kufanya huyo test kokote unakotaka
Kokote unakotaka ndio gia usiwashtukie mm nlikutana nao 2017 nlipiga interview online wakanipa mkataba mshahara million 5. Ila natakiwa kufanya hio test ilikua dola 300 enzi zile. Sema nilitafuta mawasiliano ya huo mradi head office ilikua Chicago, walinijibu Wana branch Kenya na Zimbabwe tu Africa. Kwahio nakushauri watafute website ya huo mradi nenda contacts waulize ni utapeli wa zamani sana
 
Hii ndo website walotumia
Mbona kama legit?
 
Hii ndo website walotumia
Mbona kama legit?
Sio legit, ila ni matapeli wenye akili kidogo ndio maana unaona wameweza kutengeneza hiyo website ya mchongo. Why nasema sio legit?
Sababu:
1.Uki google jina la organization yao, taarifa pekee ambazo zinatokea kuhusu wao ni za website yao (www.ghvhi.org), pamoja na haya matangazo yao ya kazi. Hakuna taarifa nyingine yoyote kuwahusu ambayo unaiona kuhusu wao. Eg taarifa kuhusu miradi yao, etc. Hii ni tofauti na organization za aina hii za ukweli ukiingia google unakuta taarifa nyingi nyingi kuwahusu. Hawa jamaa hata hawana LinkedIn page, twitter wala Facebook.
2.Ukiingia kwenye website yao, watu ambao wamewa list kama directors na team members wao, asilimia kubwa hawapo LinkedIn, mtandao mkubwa wa professionals. Wawili ambao wamekua listed as directors wapo LinkedIn, ila ukiangalia profile zao za LinkedIn hazisemi chochote kile kuhusu kuwa viongozi wa hii organization.
3.Kwa kawaida nafasi kama hizi huwa zikitangazwa na organization kunakua na details mfano: Je mradi husika unatekelezwa mikoa ipi na wilaya zipi? Mradi husika ni wa miaka mingapi? Mradi husika umekua funded na nani? Hizo details zote hakuna kwenye hili tangazo lao. Pia, hakuna taarifa zozote kuhusu ilipo ofisi yao kwa Tanzania.
Conclusion: Hawa ni matapeli, ila wamejitahidi sana kufanya high level, hadi uwe na level fulani ya exposure kujua kuwa hawa ni matapeli.
 
Back
Top Bottom